Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilimahewa Wazo anusurika kupigwa na wapiga kura wake. Akimbilia karandinga la Polisi kuokoa maisha yake

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilimahewa Wazo anusurika kupigwa na wapiga kura wake. Akimbilia karandinga la Polisi kuokoa maisha yake

Wananchi wana haki ya kumfukuza, kumzomea na hata kutii agizo lolote la mtu ambaye hawakumchagua.

Kwanza viongozi wengi tunawafahamu kuoitia kampeni na zoezi la uchaguzi. Sasa mtu unaona anakuja tu kukuambia kuwa yeye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, anaomba mchango wa ujenzi wa madarasa, utakuwa na uhakika gani kuwa siyo tapeli?
 
Hii ni kali wakazi wa Kilimahewa huko Wazo Tegeta wamemshambulia kwa kipigo Mwenyekiti wao wa mtaa ambaye alilazimika kukimbilia karandinga ya polisi.

Mwenyekiti huyo anatuhumiwa kubadili mipaka ya viwanja vya wakazi hao kinyemela na baadaye kuwadai rushwa.
Wakazi wamedai hawamtaki mwenyekiti huyo kwa kuwa aliletwa tu na CCM wao hawakumchagua.

Source ITV habari

My take; Kwanini hawa viongozi mafisadi hupendelea kuvaa sare za CCM?

Maendeleo hayana vyama!
Nawapa 'A top' lazima viongozi wachaguliwe na wanainchi na siyo chama dola kwani wananchi ndiyo wanawajua viongozi wanaofaa
 
Back
Top Bottom