TANZIA Mwenyekiti wa tawi la Simba Kiwalani Amefariki Dunia kisa Simba

TANZIA Mwenyekiti wa tawi la Simba Kiwalani Amefariki Dunia kisa Simba

AFARIKI KISA SIMBASC .

[emoji419] Mwenyekiti wa tawi Kiwalani Jijini Dar es salaam Amefariki Dunia Jana kwa presha Baada ya Simba kufungwa Na Yanga Dakika Za Jioni .

Bwana alitoa Bwana Ametwaa ,Pumzika salama Majidi Pembe.

Mazishi ni Leo Mchana .

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
kama ni kweli huko anapoenda akifika anachapwa fimbo kwelikweli ndio mambo mengine yaendelee..!
 
RIP

Derby ya kariakoo ni vizuri ifutwe kama ndo hayo, Yanga baada ya kunywa supu leo tutangaze mpinzani wetu ni Real Madrid maana Simba haituwezi tena, hii si haki kwa Simba kujilinganisha uwezo na kuivimbia Yanga yenye ubora mkubwa sana.

Sasa kitimu kidogo ila kila tukikifunga kinaona tumebahatisha wakati level zetu na wao si sawa tena kwasasa, wao Simba wako kombe la mademu shirikisho sisi tuko kombe la wanaume klabu bingwa Africa wapi na wapi .
samahani mkuu jana sijaangalia mechi goli la yanga kafunga nani?
 
Goli lilianzia mbali kama treni ya Kigoma , mambo yalianzia faulo kali ya Mzee Chama akamning'iniza Camara, Camara akaleta mbwembwe za kutaka kuudaka mpira kama nyani eti afanane na Kipa wa Jupiter Diarra, basi badala ya kuupangua mpira utoke nje Camara akauzuia na ukaangukia ndani , ukakutana na Max Nzengeli , mchezaji wa kiwango cha dunia akaupiga tena golini kwa shuti kali lililomshinda Kapombe na kwa kiwewe Kelvin Kijiri akajifunga. Kama kawaida goli la Max Nzengeli huwa limetumwa na mizimu ya kwao Congo DR kuja Kwa Mkapa huwezi kurudisha kamwe!!
Ni kweli mkuu..,.Yanga ni mafundi

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom