TANZIA Mwenyekiti wa tawi la Simba Kiwalani Amefariki Dunia kisa Simba

TANZIA Mwenyekiti wa tawi la Simba Kiwalani Amefariki Dunia kisa Simba

RIP Mwenyekiti
Simba itakuwa imara one Day
 
Kweli makaburi Yana watu wengi sana waliokwenda kabla ya wakati wao
 
samahani mkuu jana sijaangalia mechi goli la yanga kafunga nani?

GaRQR0bXAAAQU80.jpeg
 
Goli lilianzia mbali kama treni ya Kigoma , mambo yalianzia faulo kali ya Mzee Chama akamning'iniza Camara, Camara akaleta mbwembwe za kutaka kuudaka mpira kama nyani eti afanane na Kipa wa Jupiter Diarra, basi badala ya kuupangua mpira utoke nje Camara akauzuia na ukaangukia ndani , ukakutana na Max Nzengeli , mchezaji wa kiwango cha dunia akaupiga tena golini kwa shuti kali lililomshinda Kapombe na kwa kiwewe Kelvin Kijiri akajifunga. Kama kawaida goli la Max Nzengeli huwa limetumwa na mizimu ya kwao Congo DR kuja Kwa Mkapa huwezi kurudisha kamwe!!

Naamini kolo umeridhika kujua goli lilivyofungwa maana ulikuwepo kwa Mkapa jana badala ya kuangalia magoli ya Yanga we kazi kubishana tu na refa, refa anakwambia Ateba kaotea japo kashindwa kufunga, wewe unabisha tu hata baada ya Azam TV kukuchorea mstari wakionesha Ateba yuko offside na kibendera katangulia mbele kusubiri Ateba akose yeye amalizie kufunga
kwahiyo goli ni la max au kijili?
 
AFARIKI KISA SIMBASC .

[emoji419] Mwenyekiti wa tawi Kiwalani Jijini Dar es salaam Amefariki Dunia Jana kwa presha Baada ya Simba kufungwa Na Yanga Dakika Za Jioni .

Bwana alitoa Bwana Ametwaa ,Pumzika salama Majidi Pembe.

Mazishi ni Leo Mchana .

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Hana jina wala maelezo ya dakitari
 
Goli lilianzia mbali kama treni ya Kigoma , mambo yalianzia faulo kali ya Mzee Chama akamning'iniza Camara, Camara akaleta mbwembwe za kutaka kuudaka mpira kama nyani eti afanane na Kipa wa Jupiter Diarra, basi badala ya kuupangua mpira utoke nje Camara akauzuia na ukaangukia ndani , ukakutana na Max Nzengeli , mchezaji wa kiwango cha dunia akaupiga tena golini kwa shuti kali lililomshinda Kapombe na kwa kiwewe Kelvin Kijiri akajifunga. Kama kawaida goli la Max Nzengeli huwa limetumwa na mizimu ya kwao Congo DR kuja Kwa Mkapa huwezi kurudisha kamwe!!

Naamini kolo umeridhika kujua goli lilivyofungwa maana ulikuwepo kwa Mkapa jana badala ya kuangalia magoli ya Yanga we kazi kubishana tu na refa , refa anakwambia Ateba kaotea japo kashindwa kufunga, wewe unabisha tu hata baada ya Azam TV kukuchorea mstari wakionesha Ateba yuko offside na kibendera katangulia mbele kusubiri Ateba akose yeye amalizie kufunga!!
Ile ya Ateba, wala waamuzi hawakuamua kama ni offside bali tu ni Diara kaiokoa. Kama Ateba angefunga lingehesabiwa japo alikuwa kwenye eneo la kuotea
 
Kafunga Kelvin Kijili, akitumia vizuri assist ya wachezaji watatu! Chama, Camara na Nzengeli. Yaani kiufupi ni goli zuri na la kitaalam kabisa, lililo wahusisha wachezaji wa timu zote mbili.
yanga na ubora wao wote wameshindwa kufunga goli?
 
RIP

Derby ya kariakoo ni vizuri ifutwe kama ndo hayo, Yanga baada ya kunywa supu leo tutangaze mpinzani wetu ni Real Madrid maana Simba haituwezi tena, hii si haki kwa Simba kujilinganisha uwezo na kuivimbia Yanga yenye ubora mkubwa sana.

Sasa hawa Simba kitimu chao kidogo ila kila tukikifunga kinaona tumebahatisha wakati level zetu na wao si sawa tena kwasasa, wao Simba wako kombe la mademu ndondo cup shirikisho sisi tuko kombe la wanaume klabu bingwa Africa wapi na wapi .

Simba ni wakati sasa watangaze kuwa wao ni underdog na wajiweke kundi moja na KMC, Namungo na Kagera sugar ili kunusuru mashabiki wake, kuendelea kuwaaminisha mashabiki kuwa wataifunga Yanga wakati ubavu hawana matokeo yake ndo hayo!! Wengi wanaumwa sana kwasasa raha imekata miaka inaenda tu Yanga bingwa!!
Acha mbwembwe msibani.

Apumzike kwa amani mwanasoka.
 
yanga na ubora wao wote wameshindwa kufunga goli?
Wameshindwaje tena kufunga goli, na wakati mechi imeisha kwa Yanga kupata ushindi wa goli 1-0! Haijalishi amefunga nani! Maana zisingetokea purukushani, huyo Kijili asingeweza kujifunga.
 
Kuna upunguani mwingine siyo wa kusema jina la bwana lihimidiwe.
Hivi mnawezaje kuwaza mambo ya mpira hadi mtu unapata presha ya kufa?
Ushabiki uliopitiliza Mzee[emoji23]
 
Wameshindwaje tena kufunga goli, na wakati mechi imeisha kwa Yanga kupata ushindi wa goli 1-0! Haijalishi amefunga nani! Maana zisingetokea purukushani, huyo Kijili asingeweza kujifunga.
Hao ndo Mbu mbu Mbu
 
Kafariki dunia wapi wewe acha fix huyo kafariki kiwalani

Kufariki dunia ina maana unakuwa umekufa kila nchi dunia nzima,umekufa Kenya Uganda,Marekani nk

Huyo kafariki Kiwalani hakuna cha kufariki dunia
 
Back
Top Bottom