Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema kuzunguka nchi nzima kumnadi Rais Magufuli

Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema kuzunguka nchi nzima kumnadi Rais Magufuli

Mwenyekiti wa Chama Cha TLP Augustine Mrema amesema atazunguka nchi nzima kumnadi Rais Dkt John Magufuli kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kwamba haya si maamuzi yake binafsi bali ni ya mkutano mkuu wa TLP
Huyu anaomba hela kijanja kwa JPM, mzee anazeeka vibaya, hivi CCM ina shida gani ya kupigiwa debe na huyu chokambaya ilhali kuna NEC, wakurugenzi na polisccm? Atuondolee kifaduro chake hapa.
 
Hapo washa mfunga mdomo kwa remote
CCM na TLP wamevunja sheria ya uchaguzi kwa kutangaza hadharani ushirikiano wao bila makubaliano maamum ya kisheria..... Msajili wa vyama huu ni ushahidi tosha kwamba wanastahili kufutwa wote wawili.

Kama hawafutwi basi na sisi tukianza kumdadi mgombea wa chama X usinune maana sheria huwa haili upande mmoja.
 
Tangu Jiwe ameingia madarakani sikumbuki kama Lyatonga au kiongozi yeyote wa TLP aliwahi kukamatwa na vyombo vya dola
utashangaa wajumbe wa mkutano mkuu wapo ndani ya payroll ya lumumba.....Tanzania ina maajabu mengi kuliko tunavyodhani..Kuna wakati nilifikiri maajabu haya yatapungua kumbe ndiyo kwanza yanazidi kuongezeka.
 
Atakuwa analetewa watu na mafuso kwa hisani ya watu wa Lumumba.
Uwezekano huo ni mkubwa, ila sasa hiyo hotuba nayo atasaidiwa?

Kuongea mwenyewe ni kama kindergarten
 
Uwezekano huo ni mkubwa, ila sasa hiyo hotuba nayo atasaidiwa?

Kuongea mwenyewe ni kama kindergarten
Watu wa aina hiyo ndo mzee anawakubali, wewe unadhani kwenye kampeni anaweza kukubali kuambatana na watu kama kina January et all??
Jibu ni hapana.
 
Hichi kibabu kipumzishe mwili wake kiandike urithi...
Ni kichaa tu ndiye anayeweza kumsikiliza huyo mgonjwa wa mwili na akili.
 

Ni jambo jema na Maamuzi yao ila nadhani kwa Uchanga wa Chama chao nilidhani hiyo Gharama ya Kuzunguka nchi nzima ingetumika Kukijenga na Kukiimarisha zaidi Chama chake ili ikiwezekana hata wakati Kipenzi chao akitoka Madarakani kwa Kumaliza muda wake basi ama Yeye Mrema au Mtu ambaye watakuwa wamshamuandaa mwenye aina ya Uongozi alionao Rais Magufuli aweze Kushika hatamu ya Urais.
 
Chama cha tlp hakuna uwezo huo kiuchumi kufanya hivyo kwa wagombea wake lakini kumnadi Magufuli wanaweza kuzunguka Tanzania hata Mara mbili mbili na ikawezekana,wataenda kwa nchi kavu,anga na/au baharini ikibidi.
Haya mambo utayapata Tanzania tu hapa duniani.CCM mpya ina matawi mengi!!!
Tunaiona ofisi ya Msajili wa Vyama,TAKUKURU,POLICE,TISS,NEC &DED's +WEO/VEO's wanavyojiandaa kukandamiza na kuvuruga kura zote ziende CCM mpya bila kujali wapiga kura/Wananchi wanamtaka kiongozi yupi.Kama siyo wa CCM mpya na wachumba wake hawamtangazi.Huo ndiyo mkakati wao.
Tuchukue hatua,kura yako moja na yangu moja zinakuwa mbili,na wazalendo wengine wakifanya hivyo CCM mpya ni nyepesi kulikoni tunavyoaminishwa.Tuepukane na rushwa ya uchaguzi,tupigie kura ukweli na tuzilinde kura zetu ili watangazwe viongozi tuliowachagua.Hapo tutakuwa tumetimiza wajibu wetu kwa nchi yetu.
CCM isijaribu kupanga mbinu za kubadili matokeo ya uchaguzi,acheni kuchakachua na ruhusuni maoni ya Watanzania bila kujali ni wa chama gani,tunajenga nyumbani moja/yetu sote.Kwa nini tugombee fito?
 
Back
Top Bottom