GE2025 Mwenyekiti wa tume huru ya taifa ya uchaguzi INEC akagua maandalizi ya uchaguzi mkuu Mbeya

GE2025 Mwenyekiti wa tume huru ya taifa ya uchaguzi INEC akagua maandalizi ya uchaguzi mkuu Mbeya

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele jana Septemba 19, 2025 alitembelea Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika Majimbo ya Uchaguzi ya Mbeya Mjini na Uyole na kupokea taarifa ya mkoa kutoka kwa wasimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025 na kisha kukagua vifaa ambavyo tayari vimepokelewa katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Jaji Mwambegele pia alipata fursa ya kutembelea kampeni za wagombea ubunge wa chama cha CUF na CCM katika majimbo hayo.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na Tume,Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.​
1758358025369.png


1758358124388.png


1758358144807.png
 
Hii nchi pesa zinatumika kwenye mambo ya kipuuzi sana.

Hapo anakula posho kufanya huu upuuzi!!
 
Hivi hii ikiwa tume huru ya uchaguzi halafu ile ya Malawi tutaiitaje?
hii ni tume ya Rais wa Tanzania ambaye ni mwanachama wa CCM na ndiye anayewachagua Viongozi wa Tume ya Uchaguzi halafu mnaita tume huru,ujingaujina tu,
 
Hii nchi pesa zinatumika kwenye mambo ya kipuuzi sana.

Hapo anakula posho kufanya huu upuuzi!!
Na ukiuangalia hata huo mdomo wake, unasema mengi sana.. yaani wenyewe ni kubugia bugia tu, kwa kweli , kwa maneno ya polepole, wahusika watunze data tu. lazima wazitapike siku ikifika.
 
Na ukiuangalia hata huo mdomo wake, unasema mengi sana.. yaani wenyewe ni kubugia bugia tu, kwa kweli , kwa maneno ya polepole, wahusika watunze data tu. lazima wazitapike siku ikifika.
Hii nchi ilipofika ni lazima siku ikifika hawa watu tuwashughulikie vilivyo ili yanayofanyika sasa kutufanya Wananchi mazwazwa yasifanyike tena.

Ni suala la muda tu. Ila kumbukumbu lazima ziwekwe vizuri sana.
 
Nilidhani uchaguzi wa mwaka 2020 ungekuwa ndio mbovu zaidi kwenye historia ya TZ lakini huu wa 2025 umevunja rekodi zote mbovu.
 
Nilidhani uchaguzi wa mwaka 2020 ungekuwa ndio mbovu zaidi kwenye historia ya TZ lakini huu wa 2025 umevunja rekodi zote mbovu.
Unaofuata unaweza kuwa wa hovyo zaidi. Ndivyo ilivyo, mwanao akiiba buku akamchekea kesho ataiba buku mbili. Baada ya miaka kumi anakuwa jambazi kabisa.
 
Back
Top Bottom