Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,536
- 7,194
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM taifa Bw. Mohammed Ali Kawaida amesema wapinzani hawajajipanga na hawana ushawishi wa kusimama na wagombea wateule wa urais CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussein Ally Mwinyi na mgombea mwenza wa urais Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi katika Uchaguzi Mkuu 2025 kwa kuanza kutafuta sababu za kujiondoa.
Amebainisha hayo jijini Dodoma mara baada ya kuzindua nyumba ya mtumishi wa UVCCM iliyojengwa na umoja huo mkoa wa Dodoma eneo la Iyumbu huku akieleza kuwa kauli yao ya “no reform, no election” haiwezi zuia CCM kushiriki Uchaguzi Mkuu mwaka huu.