KILIMANJARO: Wakati Joto la Siasa likiendelea kupanda kwakasi hapa nchini kuelekea uchaguzi mkuu Octobar 2025, Mwenyekiti wa UVCCM Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro Chifu Yuvenal Ole Shirima ameeleza kuwa na yeye tayari ameshakiandikia chama chake barua yakuomba ridhaa yakutia nia ya kugombea kwenye uchaguzi huo.
Shirima hajaweka wazi kuwa anataka kugombea nafasi gani na jimbo gani ila ameeleza kuwa akipata nafasi yakugombea Udiwani sawa, Ubunge Pia Sawa na yuko tayari kuwatumikia wananchi.