Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mwanza, Cde. Seth Bernard Masalu, anawaomba wakazi wa Mwanza wote na watanzanania kujitokeza kwa wingi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji utakaofanyika Novemba 27, 2024 kwa Kuwachaguwa Wagombea wote wa Chama cha Mapinduzi katika nafasi zote za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.
Masalu ameyasema hayo wakati akifungua kampeni wilaya ya Nyamagana kata ya Nyegezi. Pia ameowaomba wananchi wa Nyegezi kuwachagua wagombea wote wa mitaa yote 8 wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi.