Pre GE2025 Mwenyekiti wa UVCCM Songwe: Nakerwa na baadhi ya wanasiasa ambao wanaifanya Tanzania kama ‘gheto"

Pre GE2025 Mwenyekiti wa UVCCM Songwe: Nakerwa na baadhi ya wanasiasa ambao wanaifanya Tanzania kama ‘gheto"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Eh kumbe kuna wanasiasa wanaifanya Tanzania kama geto? Hawa si wa vyama vya upinzani kweli?

Mh namuona kama Lissu, Lema na wengineo linawahusu sana
===============

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Songwe, Fatma Hussein, anasema anakerwa na baadhi ya wanasiasa ambao wanaifanya Tanzania kama ‘gheto’ na siyo makazi rasmi kutokana na familia zao kuishi nje ya nchi.

Fatma ameyasema hayo leo Februari Mosi, 2025 alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari mjini Songwe, kwa lengo la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha mkutano ulimalizika hivi karibuni wa Nishati Afrika.

Amesema wanasiasa hao ndio vinara wa kuchochea na kutoa lugha zinazolenga kudhoofisha utulivu wa nchi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Soma Pia: Songwe: Matukio Yanayojiri Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025


Ameeleza wanapozungumzia suala la uchaguzi, wanazungumzia amani na utulivu wa nchi, "Mtu asiye kuwa na familia hapa nchini anajua hata akivuruga mambo, yeye familia yake ipo salama na kesho ataka tiketi anaondoka, ndio maana nasema lazima Watanzania tuwe makini na hawa watu," amesisitiza Fatma.

 
Muulize kama anaijua walipo Familia ya viongozi wafuatayo
1. Wasira Masatu
2. Majaliwa Majaliwa
3. Nchimbi Emmanuel
4. Amos Makala
5. Kinana Abdul

Kwahiyo wanafungwa kuongelea mambo ya uchaguzi. UVCCM ndiyo taasisi mufilisi kuliko taasisi yoyote hapa Tanzania, wanajenga hoja iliyokaa kunyenyekea wa watu kuliko kujenga watu.
 
Back
Top Bottom