Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Tanga, Ramadhan Omary Agosti 24, 2025 ameongoza kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Tanga kilichoketi kwa ajili ya masuala mbalimbali ya Jumuiya ndani ya Mkoa huo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu.
Pamoja na mambo mengine baraza liliazimia kwa kauli moja kuyapokea majina yote yaliyoteuliwa na Kamati Kuu na wao kama vijana kuhakikisha wanakitafutia kura za kutosha Chama cha Mapinduzi (CCM).
Aidha Mwenyekiti huyo amekemea vikali wale wote wanaoendelea na makundi kwa kipindi hiki ambacho majina yame rudishwa na kusema kuwa kama mtu anahisi mgombea wake alikuwa na ulazima wa kuwa mbunge anajidanganya chama kina macho na kimeamua kuleta watu kwa maslahi ya watu na sio mtu kwa maslahi yake binafsi.