carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Mwenyekiti wa Jukwaa la Vijana Taifa kupitia Chama cha Wakulima (AAFP), Yusuph, amempa onyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Faris Burhan, akimtaka kuhakikisha ushindani wa kisiasa unafanyika kwa hoja badala ya vitendo vya utekaji.
Yusuph ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Chamwino, mkoani Dodoma, ambako AAFP inaendelea na kampeni za kumnadi mgombea wake katika uchaguzi mdogo wa ubunge.
Amesema kuwa iwapo viongozi wa UVCCM wako tayari kushindana kisiasa, wanapaswa kufanya hivyo kwa kujenga hoja na kujibu hoja za wapinzani, badala ya kutumia vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa watu.
Amesisitiza kuwa tofauti za kisiasa zinapaswa kutatuliwa kwa mijadala ya hoja, akiwataka viongozi wa vyama vya siasa kuzingatia misingi ya demokrasia na kuepuka vitendo vya utekaji.
Chanzo : Mwana habari