Mwenyekiti wa Wafanyabishara Kariakoo: Tunataka kugoma kwa Sababu ya TRA haitaki kutuelewa

Mwenyekiti wa Wafanyabishara Kariakoo: Tunataka kugoma kwa Sababu ya TRA haitaki kutuelewa

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Mwenyekiti wa Wafanyabishara Kariakoo anasema chanzo cha mgomo wao ni TRA kurudisha enforcement.

Malalamiko yao makubwa ni kwamba TRA inawaonea kwa sababu inawadai VAT na waziri mkuu aliagiza TRA iwasikilize.

Nachokiona ni kwamba wafanyabishara hawataki kabisa kulipa kodi nchi hii. Hii nchi itaendeleaje kama watu hawataki kulipa kodi?

View: https://www.instagram.com/reel/C8jy0vIiY4L/?igsh=MXdqMjhwZncxMzhxbg==
 
Bidhaa viwandani au bandarini ziwekewe vat direct.

Kumdai vat mtu wa pili Kutoka mwisho ni uonevu na kutengeza ugumu wa kuikusanya Kodi hiyo.
Vat inakua na ugumu gani kukusanywa wakati sio wewe mfanyabiashara unaeilipa? Kodi alipe mwingine wewe ukusanye kisha usipeleke serikalini ndio uone ni ngumu?
 
Mfumo wa kodi una shida gani inahitaji mjadala wa ki taifa wabunge wasikilize maoni ya watu wote
 
Vat inakua na ugumu gani kukusanywa wakati sio wewe mfanyabiashara unaeilipa? Kodi alipe mwingine wewe ukusanye kisha usipeleke serikalini ndio uone ni ngumu?
Hivi unaakili kweli wewe?? Hebu rudia mara mbili mbili ulichoandika mwehu wewe
 
Mgeni anauziwa na VAT 18% wakati bidhaa hatumii Tanzania na hatuna utaratibu wowote wa kuwarudishia VAT zao kama wao wanavyoturudishia sisi VAT zao...
Wafanyabiashara wanalipa kodi nyingi sana na bado wanasumbuliwa..
 
Mwenyekiti wa Wafanyabishara Kariakoo anasema chanzo cha mgomo wao ni TRA kurudisha enforcement.

Malalamiko yao makubwa ni kwamba TRA inawaonea kwa sababu inawadai VAT na waziri mkuu aliagiza TRA iwasikilize.

Nachokiona ni kwamba wafanyabishara hawataki kabisa kulipa kodi nchi hii. Hii nchi itaendeleaje kama watu hawataki kulipa kodi?

View: https://www.instagram.com/reel/C8jy0vIiY4L/?igsh=MXdqMjhwZncxMzhxbg==

Mbona TRA wakiwaacha wafanyabiashara bila kuwafuatilia hawatalipa kodi.
Hakuna mfanyabiashara aliyetayari kulipa Kodi kwa hiari.
 
Vat inakua na ugumu gani kukusanywa wakati sio wewe mfanyabiashara unaeilipa? Kodi alipe mwingine wewe ukusanye kisha usipeleke serikalini ndio uone ni ngumu?
Mchina aliyepo Tz Kwa Mfano,

Anauza Guta Kwa mfanyabiashara Kwa Bei ya 2000,000,

Na selling price ni 2050,000, na mchina huyo anakupa risiti iliyoandikwa 1900,000 pungufu ya Bei uliyolipia ya 2,000,000.

Ukifika dukani kwako ukauza Kwa 2050,000, mteja atadai utoe risiti halali ya 2050,000.

Haya, huyo mfanyabiashara atapeleka au hesabu yake ya vat itasomekaje.

Majibu tafadhali 🙏
 
Mfumo wa kodi una shida gani inahitaji mjadala wa ki taifa wabunge wasikilize maoni ya watu wote
Wabunge hawa amabo hawataki kujadili suala la sukari, kuna kodi billioni ngapi zimesamehewa hapo? Hivi kuna suala gani la maana bunge limefanya?
 
Mwenyekiti wa Wafanyabishara Kariakoo anasema chanzo cha mgomo wao ni TRA kurudisha enforcement.

Malalamiko yao makubwa ni kwamba TRA inawaonea kwa sababu inawadai VAT na waziri mkuu aliagiza TRA iwasikilize.

Nachokiona ni kwamba wafanyabishara hawataki kabisa kulipa kodi nchi hii. Hii nchi itaendeleaje kama watu hawataki kulipa kodi?

View: https://www.instagram.com/reel/C8jy0vIiY4L/?igsh=MXdqMjhwZncxMzhxbg==

Kodi zikishakusanywa wanampelekea mama anazichezea na mwanawe watakavyo
 
Wafanyabiashara duniani kote ni wakulindwa na serikali...marekani kwa nini wanaongoza kwa mabilionea wengi? Wanalindwa...wanaheshimiwa...wanatengenezewa mazingira mazuri ya kutanua biashara zao...na pia uhakika wa mauzo ya biashara zao upo...ndio maana hata mfanyabiashara akikwepa kodi hatua kali dhidi yake itachukuliwa...

Wachina wanakuja bongo hawana kitu...wanachuma hapapa Tz..na mikopo wanapewa hapa hapa Tz...wanakuwa mabilionea hapa hapq Tz na kuendeleza kwao...wana bank yao ipo hapo posta...wanapewa support vizur tuu...

Kazi ni kweli wanajituma...ni wajanja na pia ni wanyonyaji...pombe..kamari..wanawake ndio starehe zao...lakin pesa ni sisi tunawapa...mchawi wa bongo ni wabongo wenzie...

Sio kwamba wafanya biashara hawataki kulipa kodi...wanalipa sana...kuna muda unapambana na mchina kwenye soko unaamua kunyoosha mikono juu...kule kwao huwez fanya ivo hata kidogo...lakin serikali haioni hili...
 
Naamin kabisaa bungeni pale...hawazidi wabunge 50...wanao jua maswala ya kodi...elimu ya kodi ni pana haswa...sheria za zaman bado zinafanya kazi kwa nn?
 
Hebu angalia...zinasaidia nini hizi?
 
Attachments

  • 3B0D9D5F-C3D6-4E51-A4FE-32CA3E628F62.jpeg
    3B0D9D5F-C3D6-4E51-A4FE-32CA3E628F62.jpeg
    30.9 KB · Views: 5
Bidhaa viwandani au bandarini ziwekewe vat direct.

Kumdai vat mtu wa pili Kutoka mwisho ni uonevu na kutengeza ugumu wa kuikusanya Kodi hiyo.
Mbona lile bonge nyanya kipindi cha mgomo wa kwanza liliisifia serikali? Tanzania ni nchi yenye vituko vingi na maigizo ya kijinga. Mpaka wananchi tutakapojua CCM ni kundi la wahuni, hakuna kitakachobadilika.
 
Mchina aliyepo Tz Kwa Mfano,

Anauza Guta Kwa mfanyabiashara Kwa Bei ya 2000,000,

Na selling price ni 2050,000, na mchina huyo anakupa risiti iliyoandikwa 1900,000 pungufu ya Bei uliyolipia ya 2,000,000.

Ukifika dukani kwako ukauza Kwa 2050,000, mteja atadai utoe risiti halali ya 2050,000.

Haya, huyo mfanyabiashara atapeleka au hesabu yake ya vat itasomekaje.

Majibu tafadhali 🙏
Kwanini akupe listi ya 190000?
 
Nafikiri ni Jambo zuri sana kwa wafanyabiashara Kugoma.Ni moja kati ya njia ya kufikisha malalamiko kwa wtawala.Hata hivyo kabla ya kutangaza Mgomo wahakikishe kwamba Tatizo wanalogomea ni tatizo kweli,Pili wahakikishe kwamba wameshamaliza njia mbadala ya kutafuta suluhu.Hii ni muhimu hasa kwa sababu kwenye Masuala ya kodi kuna mambo mengi sana ambayo yanahitaji elimu,utaalamu na uzoefu ili uweze kufahamu ni nini unapaswa kulipia na ni nini ambacho hupaswi kulipia.

Tatizo ninaloona hapani wa fanyabiasha kutaka kutatua matatizo ya kibiashara,kikodi na kisheria kwa njia ya Kisiasa.

Ushauri wangu.Kwanza wahakikishwe wana cases ambazo ziko clear,Wafungue kesi katika mahakama za kikodi kwa kuzingatia sheria na taratibu za kikodi na kisheria.Wakimaliza humo na wakaona hawapati usaidizi basa wasigome bali wafunge kabisa Biashara zao yaani wahame kariakoo waende Burundi kama alivyosema Nchemba
 
Back
Top Bottom