RRONDO
JF-Expert Member
- Jan 3, 2010
- 55,727
- 123,094
Hakuna kitu kitanunuliwa wholesale 2,000,000 halafu kiuzwe Retail 2,050,000. Tuongelee uhalisia.Mchina aliyepo Tz Kwa Mfano,
Anauza Guta Kwa mfanyabiashara Kwa Bei ya 2000,000,
Na selling price ni 2050,000, na mchina huyo anakupa risiti iliyoandikwa 1900,000 pungufu ya Bei uliyolipia ya 2,000,000.
Ukifika dukani kwako ukauza Kwa 2050,000, mteja atadai utoe risiti halali ya 2050,000.
Haya, huyo mfanyabiashara atapeleka au hesabu yake ya vat itasomekaje.
Majibu tafadhali 🙏
Mchina ni wholesaler kwa point hii. Ana jukumu la kutoa VAT receipt kwa retailer. Kwahio kwenye hio 2m kuna VAT.
Retailer ataenda kuuza kwa mteja wa mwisho mfano atauza 2.5m ambaya itakuwa na VAT kama retailer ni VaT registered.
Sasa retailer atatakiwa kupeleka VAT TRA.
Hapa atachukua VAT amount aliotoa kwa mchina halafu ataipunguza VAT alimchaji mteja wake wa mwisho. Tofauti ndio anapeleka TRA.
Kifupi VaT analipa mteja wa mwisho.
Shida iliopo Kariakoo mtu ambaye ni VaT registered anashindana biashara na mtu ambaye hajasajiliwa VAt.
Kitu cha 100 mtu ambaye kasajiliwa VaT itabidi auze 118 wakati asiesajiliwa atauza 100 na mko mtaa mmoja.
Imagine tv 300,000 VaT ni 50,000
Hapa asiesajiliwa VaT atauza 250,000 tu huku aliesajiliwa itabidi auze 300,000. Kuna mmoja hatauza hapo.