Mgeni wa Jiji
JF-Expert Member
- Jul 27, 2017
- 9,758
- 18,431
Hili ni kweli kabisa.Unaweza kuwa na haki lkn usijue namna yakuzidai, au unajua kuzidai na bado usizipate, au ukazipata lkn usijue namna yakuzitumia. Nmeisikiliza clip ile vizuri. Yule kijana ameongea pointi za msingi sana Sana. Tena ilitakiwa apewe ajira mapema maana Ni nguvu kazi nzuri inayorandaranda mtaani kulingana na uwezo wake.
Very trueItakes mtu ambae yupo serikalini or ambae alishapita huko tena kwenye vyombo husika kujua weakness ya hao watu na namna wana operate.
Wako watu walikuwa huko they know how to avoid them because walikuwa huko so mbinu wanazifaham
Ila kwa raia wa kawaida is another story
Tuishi na sababu ya kwanza tu kiongoziHiyo sababu ya pili ni ya Ukandamizaji tu. Nsons kwa awamu hii ndiyo imeanza kuwa sababu ya kuwashikila watu kinyume cha sheria.
Watu wanaotoka hadharani kuomba ulinzi kuwa maisha yao yako hatarini huwa hawapewi huo ulinzi.
Mtu yoyote ambaye hajawahi kushiriki kuanzisha mgomo shule, hawezi kufanya hilo jambo akafanikiwa. Hiyo ni haiwezekani lazima atazingua tu maana hana alichowahi kujifunza na wala haioni hatari iliyo mbele yake.Umejitahidi kuandika Big Up japo nawe ni wa mlengo ule
Kwahiyo Mobout Sese seko ni sawa na chama letu pendwa sii ndioNchini Zaire (DRC)! ilikuwa ni Kosa kubwa sana kwa kufanya Kitendo cha Kumkosoa mtawala wa nchi hiyo Dikteta Mobutu Sese Seko au kuukosoa Utawala wake. Hali ipo hivyo pia nchini Urusi kwa Putin na nchini China.
Kuwakosoa Madikteta ni sawa sawa na kujikatia tiketi ya kifo.
Zipo Mkuu, kwa kadiri ya imani.yako ilivyo soma vitabu vya imani yako kujifunza namna watu walizidai haki zao au kusisitiza mambo fulani fulani. Wote waliojifanya manunda walikufa vifo vya ajabu sana.Hamna njia nzuri ya kuanzisha jambo cha msingi wameanza kudai wanachokiamini
Kama chawa wameshamiri kila.koma,tutapata wapi haki za kiraiaAise, achana na taasisi inayoitwa serikali. Sio ndogo hivyo unavyowaza. Sawa hautakiwi kuiogopa serikali ila amini nakuambia unatakiwa kuiheshimu kwa.adabu zote ulizofundishwa kwenu.
Hapa unaweza ukafikiri hawakujui ila na jina lako hili wakikuamulia ni haraka sana wanakujua, na kukuchukua itakuwa ni uamuzi wao tu wala sio wako 😂😂
Unless uwe ni keyboard worrior au ubishe tu kutokana na uelewa mdogo.
kidumu sana,inabidi tuibipu serikali kwa maandamano ya amani.Naomba mfahamu mimi raisi wa chama Cha ma jobless pro max niko salama kabisa.
hao neto sijui neto ni wezi wa sera na jina letu la ma jobless pro max,
Raisi wa chama Cha ma jobless pro max ni Intelligent businessman.
makamu wake ni Bolotoba.
katibu wa ma jobless ni min -me, mratibu wa mipango ni Edo kissy.
Wakili wa ma jobless ni Selikavu
waziri wa mambo ya ndani ni Thecoder, na msemaji wa chama Cha ma jobless pro max ni makutupora.
Kidumu chama Cha ma jobless pro max.
View attachment 3248564
We ni mjinga sana vijana kama nyie ni hasara kwa taifa nikuulize hao waliomuua yohana mbatizaji waliishi mileleZipo Mkuu, kwa kadiri ya imani.yako ilivyo soma vitabu vya imani yako kujifunza namna watu walizidai haki zao au kusisitiza mambo fulani fulani. Wote waliojifanya manunda walikufa vifo vya ajabu sana.
Mimi ni Mkristu, najifunza kupitia biblia namna watu waliozingua utawala walipata mapigo na namna waliotumwa na Mungu kuonya walivyoonya kwa adabu na unyenyekevu.
Huko unapata namna yakufanya stadi tofauti tofauti za maisha, mfano Yohana Mbatizaji kama sio ununda wake asingekatwa kichwa, pia manabii waliomuongoza Mfalme Daudi kama sio adabu zao basi wasingeweza kuishi muda mrefu. Walitumwa na Mungu na bado wakawa na adabu sembuse wewe mwanadamu unayetumwa na hisia zako unakosa adabu lazima ukipate kipindi kigumu cha maisha.
Ni mambo magumu.
Tuishi na sababu ya kwanza tu kiongozi
Mwenyekiti wetu wa NETO Joseph Paulo Kaheza amekamatwa na police mkoani Geita. Tumethibitisha hizi taarifa kutoka kwa mjomba wake ambaye alifika katika kituo hicho cha Central Geita Mjini na kutaka kumwekea dhamana kitu ambacho kilishindikana.
Soma Pia: Umoja wa Walimu Wasio Na Ajira (NETO) wakubali wito wa Simbachawene lakini wataka kuwepo na Ulinzi kwenye kikao
Katibu Mkuu wa Umoja wa Walimu Wasio na Ajira Tanzania (NETO) Daniel Edigar Mkinga ametangaza kukamatwa kwa Mwenyekiti wa NETO, Joseph Paulo Kaheza akiwa mkoani Geita kwa kile alichodai ni vuguvugu la kupigania ajira kwa walimu wa Tanzania. Ameeleza kuwa alikamatwa na askari hao wakiwa na "silaha kali".
Akizungumza na Jambo TV Jumatatu jioni, Mkinga amesema Joseph amekamatwa mchana wa siku ya Jumatatu mkoani humo katika wakati ambao umoja huo umekubali mwaliko wa kukutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, kwa ajili ya majadiliano kuhusu ajira za walimu nchini.
"Askari hao wameahidi kukamata viongozi wote wa NETO nchini jambo ambalo tunalilaani vikali kwani sisi sio waahini, ni watoto wa kimasikini tunaoiomba serikali haki yetu ya ajira kutokana na ugumu wa maisha uliokithiri huku mtaani", ameeleza Katibu Mkuu huyo huku akilaani na kuonesha kusikitishwa kwa Joseph kunyimwa dhamana.
Jambo TV imemtafuta Barnabas Daud, ndugu wa Joseph, mkazi wa kata ya Nyankumbu Geita Mjini ambaye ameeleza kuwa Joseph alikamatwa majira ya saa 9 mchana katika mazingira ya kutatanisha kwani awali alimuacha dukani akiwa na mkewe lakini aliporudi hakumkuta. Hata hivyo baadaye gari lisiloonesha waliomo ndani lilifika dukani hapo na watu ambao hawakujitambulisha kama ni askari kutokana na kutoonesha vitambulisho wala kuvaa sare, wakiwa wamemshikilia Joseph kwa pingu mkononi.
Daud anaeleza kuwa miongoni mwa watu wale kuliwapo aliyemfahamu kuwa ni askari, na alipoulizia kosa la nduguye hakuambiwa zaidi ya kuelezwa kuwa Joseph atapelekwa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) na kupewa mawasiliano ya mmoja wa wale wati. Baadaye gari hilo liliondoka na Barnabas akachukua hatua ya kwenda ofisi ya RCO ambako huko aliambiwa nduguye hayupo, akafuatilia kituo kingine cha wilaya ambako hakumkuta, ndipo akawasiliana na askari wa namba aliyoichukua ambaye alimsisitizia kuwa nduguye yupo kwa RCO akihojiwa.
Barnabas alifika kwa RCO saa 11 jioni ambapo aliambiwa arudi saa mbili usiku, aliporudi akakutana na ndugu yake ambaye alimwambia sababu ya kukamatwa kwake ni kuwa sehemu ya kundi la NETO.