Mwenyekiti wa Walimu Wasio Na Ajira (NETO) Joseph Paulo anadaiwa kukamatwa na polisi mkoani Geita

Mwenyekiti wa Walimu Wasio Na Ajira (NETO) Joseph Paulo anadaiwa kukamatwa na polisi mkoani Geita

Unaweza kuwa na haki lkn usijue namna yakuzidai, au unajua kuzidai na bado usizipate, au ukazipata lkn usijue namna yakuzitumia. Nmeisikiliza clip ile vizuri. Yule kijana ameongea pointi za msingi sana Sana. Tena ilitakiwa apewe ajira mapema maana Ni nguvu kazi nzuri inayorandaranda mtaani kulingana na uwezo wake.
Hili ni kweli kabisa.
Watu wanatakiwa kujua dunia ya sasa hauwezi kutumia mbinu zilizotumiwa na wakina Lenin, Marx au wale wa Luddism. Hichi ni muhimu sana kujua stadi ya kudai na kupokea haki yako.
 
Itakes mtu ambae yupo serikalini or ambae alishapita huko tena kwenye vyombo husika kujua weakness ya hao watu na namna wana operate.
Wako watu walikuwa huko they know how to avoid them because walikuwa huko so mbinu wanazifaham

Ila kwa raia wa kawaida is another story
Very true
 
Hiyo sababu ya pili ni ya Ukandamizaji tu. Nsons kwa awamu hii ndiyo imeanza kuwa sababu ya kuwashikila watu kinyume cha sheria.

Watu wanaotoka hadharani kuomba ulinzi kuwa maisha yao yako hatarini huwa hawapewi huo ulinzi.
Tuishi na sababu ya kwanza tu kiongozi
 
Umejitahidi kuandika Big Up japo nawe ni wa mlengo ule
Mtu yoyote ambaye hajawahi kushiriki kuanzisha mgomo shule, hawezi kufanya hilo jambo akafanikiwa. Hiyo ni haiwezekani lazima atazingua tu maana hana alichowahi kujifunza na wala haioni hatari iliyo mbele yake.
 
Nchini Zaire (DRC)! ilikuwa ni Kosa kubwa sana kwa kufanya Kitendo cha Kumkosoa mtawala wa nchi hiyo Dikteta Mobutu Sese Seko au kuukosoa Utawala wake. Hali ipo hivyo pia nchini Urusi kwa Putin na nchini China.

Kuwakosoa Madikteta ni sawa sawa na kujikatia tiketi ya kifo.
Kwahiyo Mobout Sese seko ni sawa na chama letu pendwa sii ndio
 
Hamna njia nzuri ya kuanzisha jambo cha msingi wameanza kudai wanachokiamini
Zipo Mkuu, kwa kadiri ya imani.yako ilivyo soma vitabu vya imani yako kujifunza namna watu walizidai haki zao au kusisitiza mambo fulani fulani. Wote waliojifanya manunda walikufa vifo vya ajabu sana.

Mimi ni Mkristu, najifunza kupitia biblia namna watu waliozingua utawala walipata mapigo na namna waliotumwa na Mungu kuonya walivyoonya kwa adabu na unyenyekevu.

Huko unapata namna yakufanya stadi tofauti tofauti za maisha, mfano Yohana Mbatizaji kama sio ununda wake asingekatwa kichwa, pia manabii waliomuongoza Mfalme Daudi kama sio adabu zao basi wasingeweza kuishi muda mrefu. Walitumwa na Mungu na bado wakawa na adabu sembuse wewe mwanadamu unayetumwa na hisia zako unakosa adabu lazima ukipate kipindi kigumu cha maisha.

Ni mambo magumu.
 
Mtu hana ajira inakua ndio fursa kwao kumnyanyasa uzuri malipo yapo hapa hapa Duniani..
 
Aise, achana na taasisi inayoitwa serikali. Sio ndogo hivyo unavyowaza. Sawa hautakiwi kuiogopa serikali ila amini nakuambia unatakiwa kuiheshimu kwa.adabu zote ulizofundishwa kwenu.

Hapa unaweza ukafikiri hawakujui ila na jina lako hili wakikuamulia ni haraka sana wanakujua, na kukuchukua itakuwa ni uamuzi wao tu wala sio wako 😂😂

Unless uwe ni keyboard worrior au ubishe tu kutokana na uelewa mdogo.
Kama chawa wameshamiri kila.koma,tutapata wapi haki za kiraia
 
Naomba mfahamu mimi raisi wa chama Cha ma jobless pro max niko salama kabisa.

hao neto sijui neto ni wezi wa sera na jina letu la ma jobless pro max,

Raisi wa chama Cha ma jobless pro max ni Intelligent businessman.
makamu wake ni Bolotoba.

katibu wa ma jobless ni min -me, mratibu wa mipango ni Edo kissy.

Wakili wa ma jobless ni Selikavu
waziri wa mambo ya ndani ni Thecoder, na msemaji wa chama Cha ma jobless pro max ni makutupora.

Kidumu chama Cha ma jobless pro max.
View attachment 3248564
kidumu sana,inabidi tuibipu serikali kwa maandamano ya amani.
"haki na usawa kwa maendeleo endelevu"
 
Nina uhakika hata jalada lake hawajaliandika kosa lake ni nini?
Hii ndo Tanzania kujengea wanachi wake hofu serikali inaweza sana!

Mwenye ajira anamuonea wivu asiye na ajira hadi anaamua kumkata 😁
 

Attachments

  • IMG_6274.jpeg
    IMG_6274.jpeg
    132.8 KB · Views: 1
Mambo huanza hivi hivi - watu washajichokea na hawa CCM.
 
kUmekucha na dogo ataendelea kuwa NETO daima milele maana serikali yetu haijazoea kuona walimu wajasiri kama yeye
 
Jina lenyewe la KAHEZA unaweza kulikosa ndani ya mikoa ya Tanzania isipokuwa hapo nchi jirani.
 
Zipo Mkuu, kwa kadiri ya imani.yako ilivyo soma vitabu vya imani yako kujifunza namna watu walizidai haki zao au kusisitiza mambo fulani fulani. Wote waliojifanya manunda walikufa vifo vya ajabu sana.

Mimi ni Mkristu, najifunza kupitia biblia namna watu waliozingua utawala walipata mapigo na namna waliotumwa na Mungu kuonya walivyoonya kwa adabu na unyenyekevu.

Huko unapata namna yakufanya stadi tofauti tofauti za maisha, mfano Yohana Mbatizaji kama sio ununda wake asingekatwa kichwa, pia manabii waliomuongoza Mfalme Daudi kama sio adabu zao basi wasingeweza kuishi muda mrefu. Walitumwa na Mungu na bado wakawa na adabu sembuse wewe mwanadamu unayetumwa na hisia zako unakosa adabu lazima ukipate kipindi kigumu cha maisha.

Ni mambo magumu.
We ni mjinga sana vijana kama nyie ni hasara kwa taifa nikuulize hao waliomuua yohana mbatizaji waliishi milele
 
Wanataka wampoteze na wapote Neto. Pole sana kwake
 
Mwenyekiti wetu wa NETO Joseph Paulo Kaheza amekamatwa na police mkoani Geita. Tumethibitisha hizi taarifa kutoka kwa mjomba wake ambaye alifika katika kituo hicho cha Central Geita Mjini na kutaka kumwekea dhamana kitu ambacho kilishindikana.

Soma Pia: Umoja wa Walimu Wasio Na Ajira (NETO) wakubali wito wa Simbachawene lakini wataka kuwepo na Ulinzi kwenye kikao

Katibu Mkuu wa Umoja wa Walimu Wasio na Ajira Tanzania (NETO) Daniel Edigar Mkinga ametangaza kukamatwa kwa Mwenyekiti wa NETO, Joseph Paulo Kaheza akiwa mkoani Geita kwa kile alichodai ni vuguvugu la kupigania ajira kwa walimu wa Tanzania. Ameeleza kuwa alikamatwa na askari hao wakiwa na "silaha kali".

Akizungumza na Jambo TV Jumatatu jioni, Mkinga amesema Joseph amekamatwa mchana wa siku ya Jumatatu mkoani humo katika wakati ambao umoja huo umekubali mwaliko wa kukutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, kwa ajili ya majadiliano kuhusu ajira za walimu nchini.

"Askari hao wameahidi kukamata viongozi wote wa NETO nchini jambo ambalo tunalilaani vikali kwani sisi sio waahini, ni watoto wa kimasikini tunaoiomba serikali haki yetu ya ajira kutokana na ugumu wa maisha uliokithiri huku mtaani", ameeleza Katibu Mkuu huyo huku akilaani na kuonesha kusikitishwa kwa Joseph kunyimwa dhamana.

Jambo TV imemtafuta Barnabas Daud, ndugu wa Joseph, mkazi wa kata ya Nyankumbu Geita Mjini ambaye ameeleza kuwa Joseph alikamatwa majira ya saa 9 mchana katika mazingira ya kutatanisha kwani awali alimuacha dukani akiwa na mkewe lakini aliporudi hakumkuta. Hata hivyo baadaye gari lisiloonesha waliomo ndani lilifika dukani hapo na watu ambao hawakujitambulisha kama ni askari kutokana na kutoonesha vitambulisho wala kuvaa sare, wakiwa wamemshikilia Joseph kwa pingu mkononi.

Daud anaeleza kuwa miongoni mwa watu wale kuliwapo aliyemfahamu kuwa ni askari, na alipoulizia kosa la nduguye hakuambiwa zaidi ya kuelezwa kuwa Joseph atapelekwa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) na kupewa mawasiliano ya mmoja wa wale wati. Baadaye gari hilo liliondoka na Barnabas akachukua hatua ya kwenda ofisi ya RCO ambako huko aliambiwa nduguye hayupo, akafuatilia kituo kingine cha wilaya ambako hakumkuta, ndipo akawasiliana na askari wa namba aliyoichukua ambaye alimsisitizia kuwa nduguye yupo kwa RCO akihojiwa.

Barnabas alifika kwa RCO saa 11 jioni ambapo aliambiwa arudi saa mbili usiku, aliporudi akakutana na ndugu yake ambaye alimwambia sababu ya kukamatwa kwake ni kuwa sehemu ya kundi la NETO.

Unajidanganya Sana ndugu.

Duniani kote kabisa uzoefu unaonyesha kwamba Umma haujawahi kushindwa jambo lolote lile pale umma huo unapoamua kwa dhati kabisa ya mioyo yao kutekeleza jambo hilo.

Rejea yale machafuko yaliyotokea katika nchi za kiArab kati ya Mwaka 2011 hadi 2015 kule Tunisia, Libya, Misri, n.k.
Mlipuko wa Vuguvugu lile hatari ulianzia nchini Tunisia, sababu zikiwa ni UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA.
Rejea pia kule nchini Bangladesh, Mwaka jana wa 2024 Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hasinna lilimkuta jambo huko nchini Bangladesh hadi akalazimika kuokoa nafsi na kukimbilia nchini India, hadi leo hii tunapojadili suala hili bado yupo huko India. Sababu ya yote haya ni UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA.

Aidha, hata mlipuko wa Generation Z kwa majirani zetu wa hapo Kenya, sababu ni UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA

Hivyo Basi, suala hili la Ukosefu wa Ajira kwa Vijana MUST BE HANDLED WITH GREAT CARE!
The Regime of this country Must be very careful in dealing with this Problem of the Youth Unemployment.
Matumizi ya nguvu kubwa hayana nafasi kwenye suala la Utatuzi wa tatizo hili, badala yake AKILI KUBWA, HEKIMA na BUSARA ndiyo silaha sahihi zinazopaswa kutumika katika kutatua Mgogoro huu.
 
Back
Top Bottom