Mwenyekiti wa Walimu Wasio Na Ajira (NETO) Joseph Paulo anadaiwa kukamatwa na polisi mkoani Geita

Mwenyekiti wa Walimu Wasio Na Ajira (NETO) Joseph Paulo anadaiwa kukamatwa na polisi mkoani Geita

Kitu vijana tunakosa kwenye mambo yetu mengi ni mifumo. Hapo unaweza ukakuta hawa NETO kwenye safu zao wote ni waalimu wasio na ajira. Hii inafanya mara nyongi sana harakati na vuguvugu za vijana wengi kuangukia pua na kuonekana ni vikundi vya wahun waleta vurugu.

Ila siku tukiona ipo sababu ya kuwa na safu zenye fani tofauti tofauti hapo tutaweza kushauri na kushinikiza mambo mengi chanya. Ushauri na kushauriwa ni jambo muhimu sana
Hamna njia nzuri ya kuanzisha jambo cha msingi wameanza kudai wanachokiamini
 
Acheni vijana wajipambanie , Kama hauwezi kuwaunga mkono waache wengine watawaunga mkono .

Unafikiri wangekaa kimya Serikali ingefikiria kuboresha Madai yao .



Hoja zao ni za msingi Sana
Hoja ninayoona ya msingi ni
1. kusitisha uzalishaji wa walimu wapya
Kwa kuwa Bado wapo wengi mtaani wasio na ajira

Nisiyounga mkono ni

1. Walimu kuajiriwa bila interview


Pia siamini kama serikali inao uwezo wa kuwaajiri wote wanaohitimu vyuoni
 
Dereva kazoea gari ya gia6Leo apangue GIA 12lazima apitie mafunzo kidogo!
Ukweli mkuu hizo 12 nawaachia wengine 😁nabaki kwenye gear 6 baba matipa, Costa hizi, canter,

Hizo semi trailer, busses 🙌
 
Hao walimu walisoma ili wajiajiri?
Kwa apa father sikupingi! Lakini

Kuna kitu kinaitwa break through - diverging the professional

Sahivi watu wanataka digital trainees, digital managers, watu wa branding
, kuna printing, U-Mc pia unalipa

Kwa kina dada walimu kuna course za mapambo, kwanini mtu asi diverge huku🤔ni mawazo tu
 
Kwa apa father sikupingi! Lakini

Kuna kitu kinaitwa break through - diverging the professional

Sahivi watu wanataka digital trainees, digital managers, watu wa branding
, kuna printing, U-Mc pia unalipa

Kwa kina dada walimu kuna course za mapambo, kwanini mtu asi diverge huku🤔ni mawazo tu
No hatusemi utaajiri wote, hivi una akili timamu unaita kwenye interview walimu laki 2 kwa nafasi elf 12 tu? kuna shida, kwamba hakuna upungufu wa walimu now?
 
No hatusemi utaajiri wote, hivi una akili timamu unaita kwenye interview walimu laki 2 kwa nafasi elf 12 tu? kuna shida, kwamba hakuna upungufu wa walimu now?
Lest say umefungua kiwanda cha nguo tz hapa ya kuanzia,kutafta raw materials, kushona, assembling mpaka marketing nafasi 3000 je? Wakija watu 16000 utawafukuza? Hapa itabidi tu ufanye usaili mpaka upate the best

Emu give out your solutions, je nini kifanyike
 
Hakuna serikali inayogawa pesa Wala kuajiri watu Ili iqatoe kwenye njaa na jobless.

Serikali ikiamua kuwasaka Iliweza na mkapoteana.

Mlikuwa wapi kuunda hicho kiumoja chenu za Kisiasa awamu ya Magufuli ambae alikuwa haajiri ndio mje kuleta ujinga wenu awamu ya mama aliyewaonea huruma?

By the way nyie mbumbumbu mnaotumika mlipata div.3 harafu hamtaki Usaili eti mna vyeti 😂😂
Mbumbumbu ni wewe uliamua kuwa chawa wa watawala. Kuhusu enzi za MEKO alikuwa anasema anawatoa ninyi watu hewa kwamba ambao baadae mmejiajiri kwenye uchawa. Tulimpa muda tu lakini si kwamba ilishindikana kutokea organization hii. Hata kama ungekuwa wewe ndiye Rais wa nchi hii Kwa chama chochote na tatizo hili Bado lipo organization ingeundwa tu.
Hii nchi ni yetu sote hivyo tunapaswa tule wote cake ya Taifa na siyo pekee yenu Hadi mnapata Hela ya kugawa pesa Kwa timu za mpira wengine mnanunua mitungi ya Gase Kwa ajili ya kuwahadaa wachache muendelee kula cake ya Taifa pekee yenu.
Fanyeni namna suala hili likae sawa tofauti na hapo watu washaanza kujikatia tamaa na wapo tayari kufa kuliko kuendelea kushuhudia wachache wakila mema ya nchi huku wao/walio wengi wakiteseka.
Kuhusu Kada zingine, hata vugu vugu la kudai uhuru miaka ya 1950s lilikuja kufanikiwa baada ya Mwl Nyerere ni Mwl by profession kuingilia kati. Hivyo walimu wanayo historia nzuri ya kuleta mabadiliko yenye mafanikio katika nchi hii.
 
Humo humo kuna mamluki wanatakiwa wapate strategist na staunch supporters kama alivyofanya Dr Steven Ulimboka.
 
Tupo hapa tunafuatilia Kwa ukaribu Sana. Na hii njia ikifail tuna mbinu nyingine. Mpaka tule wote cake ya taifa Kwa haki na Kwa usawa.
Na sisi wa kada zingine tunafuata nyayo zenu mpaka watanzania wote tuajiriwe na serikali
 
Lest say umefungua kiwanda cha nguo tz hapa ya kuanzia,kutafta raw materials, kushona, assembling mpaka marketing nafasi 3000 je? Wakija watu 16000 utawafukuza? Hapa itabidi tu ufanye usaili mpaka upate the best

Emu give out your solutions, je nini kifanyike
Issue ni kuajiri walimu hata elf 50, upungufu wa walimu ukoje?
 
Kama ana tuhuma zinazofaa kumpeleka mahakamani wampeleke. Kumnyima dhamana na kumshikilia kwa muda mrefu haitakuwa sawa. Cha muhimu vijana wasianzishe kichwa kichwa hizi movements zao. Wazingatie sheria na sio kuropoka bila ushahidi. Vyombo vya usalama vinalinda amani ya nchi hii kwa wivu mkubwa kwahiyo kabla hujaropoka tafakari kwanza.

Hawa NETO hawakuwa na hoja nzito zaidi ya kulalamika bila sababu za msingi. Kila fani ikianzisha umoja wa majobless na kufanya press conference itakuwa ni vurugu.
wewe ni jobless mjingamjinga san
 
Kwa scenario ya jamaa ambaye amekamatwa siku chache baada ya kuilalamikia serikali

Hivi unadhani kama hoja ya kukamatwa kwake na kunyimwa dhamana ni pamoja na kuwepo kwa viashiria vya yeye kuwa hatarini, unafikiri odds zinaonesha ni nani wanaopewa nafasi ya kuhatarisha maisha ya jamaa?

Jamaa hakuwatukana majambazi, hakuwa expose wauza madawa ya kulevya kiasi cha polisi kumuweka kizuizini kulinda usalama wake.

Sasa kama kuikemea serikali kuhusu tatizo la ajira jambo hilo liende kuhatarisha maisha yake basi sioni usalama wake wowote hata akiwa hapo polisi kwasababu nao pia ni sehemu ya serikali na inaweza kupokea maagizo na ikafanya kama ilivyo tumwa.
Ndio maana nimeweka sababu zaidi ya moja hapo kwenye kukosa dhamana. Sababu ya kwanza kabisa na ambayo nimeiwekea uzito ni hiyo ya kutokuandikiwa kosa yaani anashikiliwa bila ya kuwepo kwa kosa la jinai na hili linawezekana kabisa na ni ruhusa kwenye sheria zetu.

Hapo hata ukienda polisi hapo watakuambia limefunguliwa jalada la uchunguzi tu. Naamini utanisoma Mkuu Scars
 
Back
Top Bottom