Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
MWENYEKITI wa Wazee na mwasisi wa Chama cha NLD, Tozz Mtwanga, amemtaja Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mwanadiplomasia wa kweli.
Amesema katika historia ya Tanzania haijawahi kutokea Serikali kutoa usafiri kwa wagombea wa vyama vya upinzani, lakini chini ya uongozi wa Rais Samia jambo hilo limewezekana.
Hata hivyo, Mtwanga ameomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kushirikiana na Serikali kuangalia uwezekano wa kutoa magari kama hayo siyo tu kwa wagombea wa urais, bali pia kwa wagombea wa ubunge nchi nzima. Ameongeza kuwa wagombea hao wakipewa pia ruzuku, wataweza kufanya kampeni zao kwa ufanisi zaidi.