Mwenyekiti wa zamani wa CCM Maswa afariki dunia.

Mwenyekiti wa zamani wa CCM Maswa afariki dunia.

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
157
Reaction score
155
MWENYEKITI WA ZAMANI WA CCM WILAYA YA MASWA AFARIKI.

Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mzee Paul Jidayi (pichani) aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Maswa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Maswa,Mwl Onesmo Makota imesema kuwa amepatwa na mauti hayo leo Mei 12,2025 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya wilaya ya Maswa.

Namkumbuka wakati wa uhai wake akiwa Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Maswa,alikuwa kiongozi mwenye hekima, mzalendo na mchapakazi aliyeitumikia CCM kwa moyo wa dhati na uaminifu mkubwa.

Alitoa mchango mkubwa katika kujenga mshikamano ndani ya chama na kuhakikisha maadili ya uongozi yanazingatiwa.

Natoa pole kwa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Maswa,familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wanachama wote wa CCM walioguswa na msiba huu mzito.

Namuombea apumzike kwa amani na Mwenyezi Mungu awape faraja wote walioguswa na msiba huu.

"Bwana alitoa, Bwana ametwaa; jina la Bwana lihimidiwe."

Amina.
 

Attachments

  • 20250512_164526.jpg
    20250512_164526.jpg
    141.4 KB · Views: 40
Mungu amuweke panapo mstahili.
 
Back
Top Bottom