Mwenyezi Mungu tujaalie tupate Magufuli Mwingine

Wakuu wasalaaam,
Namshukuru Mungu muweza wa yote ningali hai hata muda huu na type.
Kwa kweli niseme kweli, Magufuli ndiye rais bora wa wakati wote kwa mujibu wangu, simaanishi wengine hawafai ila katika wawili au watatu hatuna budi kuchagua.
Kwangu mimi kila ninapoona shida ya maji najisemea kimoyomoyo maybe mzee angekuwepo hizi mambo zisingekuwepo, ninapoona umeme unakatika katika pia namkumbuka mzee,
Wadau sina maana mbaya ila namkumbuka Magufuli.
Povu ruksa. Na kazi iendelee mama kasema.
 
Huna haja ya kujitetea! Ata mimi mwenye umri wa miaka 31 kwangu Nyerere sijamuona wala Mwinyi sijamuona akiwa madarakani! Lakini Che Mkapa kioindi hicho bado akili haijakomaa kuhusu masuala ya kijamii.

Niwekee Kikwete, Magu na Samia kama kura yangu sitopepesa macho inaenda kwa Magufuli.
 

 
Ewe Mwenyezi Mungu tuepushie mbali na kiumbe dhalim kama Meko kisije kupata nafasi ya uongozi tena katika Taifa letu

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Misukule ya Mwendazake imekosa mtu wa kuwalisha unga baada ya mmiliki kuzikwa Chato mwezi Machi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…