Mwenza wako anapokataa kufunga ndoa lakini anataka muendelee kuwa pamoja nini maana yake?

mwanamke akikuambia hawez kuolewa nawe huwa ana maanisha kweli.
Huyo mwanamke atakuwa na jamaa yake huko sasa kaona jamaa haeleweki ndio karud kwa jamaa.
Huyo jamaa ajitambui kbs mwanamke anafikia hatua ya kukudharirisha kias hicho halaf unamkubali.
Jamas apige chin huyo sio mwanamke.
Ni kweli kabisa kwa sabau mshikaji baada ya kubanwa sana na familia yameibuka mengine kuwa huyu mdada ni mara ya nne kutoroka kwa nyakati tofauti tofauti n kurudi lakini jamaa alikuwa akimalizana naye kimya kimya. Mbaya zaidi mshikaji anaona kama bado anastahili msamaha. mkuu sasa sijui huyu mwanamke alikuwa akitumia mbinu gani.
 
Jamaa inabid ajitathimin sana anaweza akalea watoto wa mwanaume mwenzie.
Hakuna kitu anachopenda mwanamke km kufunga ndoa tena kwa kufanya harusi. Na mwanamke akikupenda hawez kukataa kufanya harusi hata siku 1.
Ndoa ni maisha. Jamaa ajitafakari anaweza kulia huko mbelen.
Huyo mwanamke kuna mwanaume anayempa kiburi na ndio anayempenda sana kuliko huyo jamaa yenu
 
Kuishi na mwanamke kama huyo ni dhambi ata kwa mungu yani hataki ndoa anataka sogea tukae dunia inamambo
 
Wakuu nisaidieni mawazo kidogo,

Nina jamaa yangu hivi majuzi kalazimika kurudisha pesa za michango ya harusi yake baada ya mwenza wake kugoma kufunga ndoa. Ishu iko hivi jamaa anafanya kazi Shinyanga maeneo ya Kahama lakini familia maana ya mke na watoto wake wawili wanaishi Mwanza ambako wamejenga.

Baada ya kupanga na mwenzake waliyeishi nae miaka tisa kuwa sasa ni wakati wa kuhalalisha ndoa wakakubaliana vizuri. Kijana kaanza michakato na mambo yakaanza kwa kasi sana ikiwa ni taarifa kwa ndugu jamaa na marafiki am apo vikao vilianza na taratibu zingine za kikanisa.

Hivyo jamaa akawa kila anapopata likizo ni kufuatili kamati ya vikao imefikia wapi na kwa bahati hakuna kilicho haribika mpaka tarehe ikawa imeshajulikana na ikawa imebaki mambo ya kusubiri tarehe.

Ikiwa imebaki mwenzi mmoja kufika tarehe husika, ikatokea ishu ya ajabu sana yaani huyu akapata likizo kama kawaida kamtaarifu mwenzake kuwa anakuja lakini kabla ya kufika Mwanza akamwambia mwenzie kuwa atapita kwanza kwao (kwa kijana) amboko shughuli ingefanyika.

Lakini mke akamwambia aache tu kuwasumbua ndugu zake kwasababu yeye hayuko tayari kuishi nae. Kijana hakuamini ikabidi kweli aache kwenda kwao na kuelekea Mwanza ambako mbaya zaidi hakumkuta mkewe na akakuta watoto wameachwa kwa jirani. Alipouliza majirani walimjibu huyu kasema kaenda hospitali. Kijana alipojaribu kuwasiliana nae simu yake haikujibiwa.

Kijana hakuhamaki akabuy time mpaka siku iliyofuata. Baada ya hapo ilimchuku siku kama 5 bila mawasiliano na alipoona muda wa kurudi kazini umewadia na mdada hapatikani kwenye simu aliwasiliana na ukweni nako hawakuwa wanajua chochote. Jamaa akatoa ripoti polisi na ustawi wa jamii.

Hivo akachukuwa watoto wake akapeleka kwa dada yake nje kabisa ya mwanzani nyumba akaweka mlinzi yeye akarudi zake kazini. Akiwa huko baada familia yake kuchanganyikiwa walianza kumtafuta yule mdada kila sehemu waliloamini anaweza kuwepo bila mafanikio.

Baada ya wiki mbili hivi mdada akaibuka na kudai ni kweli hana mpango wa kuuishi na mshikaji kisa anadai ajisikiii tu. Basi vikao mbli mbali vya familia viakaamua hiyo mipango ya ndoa ife na jamaa akalazimika kuanza kurudisha hela za watu. Baada ya muda huyu msichana kaanza kurudi kwa jamaa eti anaomba msamaha hii ni halali jamani?.

Kisa ni cha kweli.
Huyu Dada si bure kuna mtu anamsumbua! Labda kwa vile upo mbali nae na je Ukisafiri hua unarudi nyumban upatapo likizo tuu au?
 
Ndugu yangu,huyo sio mwanamke wa kuoa,inawezekana anayo mume mwingine,jamaa yako akienda kazini na yy anaenda kwa mume wake wa kweli,mwambie jamaa yako asimsogelee tena huyo dada.
 
Dah....Mie ngoja niwe wazi maana imekuwa too much..... Kwa akili za kawaida kabisa siyo vibaya ukaomba ushauri juu ya namna Bora ya kusimamia biashara yako ili upate faida....au ukaomba ushauri jinsi ya kuvaa ukiwa unaenda harusini..au hata juu ya tatizo fulani la afya ...nasema si vibaya kwa sababu wataalam wa hayo mambo wapo .....Lakini ni UJINGA kuja hapa kuomba ushauri wa kumpenda mtu au kutompenda kwa sababu hilo jambo linahusu moyo wa mtu..ambao ndiyo mwamuzi..mtu wa pili hana ushauri wowote juu la hili kwa sababu ni jambo la KUUSIKILIZA MOYO WAKO. Kama kweli kama wangekuwepo wataalam wa haya mambo basi wangekuwa wamejaza wanawake au wanaume katika majumba yao... Mapenzi yanataka muendane ....Bila ya hivyo ni utumwa ..[emoji41] [emoji41]
 
Hapana mkuu siyo mimi ni jamaa yangu wa karibu sana. Sasa cha ajabu sana ni kuwa jamaa amefikia hatu anaonesha dalili za kulegeza uzi make familia ilipiga marufuku kwa wanafamili wote kutojihusisha na yule mdada. Lakini juzi mshikaji kaaja kwao anaomba kuitisha kikoa ili familia ione namna ya kumsamehe lakini familia imechomoa. Kwa kuwa alishindwa kueleza kama anafahamu alikokuwa kajichimbia kwa kipindi chote cha wiki mbili. Kwa sasa mdada yuko kwao.
Huyo jamaa jinga kabisa hana msimamo. Huyo si mwanamke wa kufaa kuoa tena.

Ni wale wanawake ambao huwa wanakuwa na wanaume zaidi ya mmoja na wanaweka malengo kwa wanaume wote hao, anamtingishia kiberiti jamaa na atamtawala sana mwanaume.

Kwanza nahisi kichwani mwake si mzima kbs na amejaa kiburi.
 
Hapo hamna mapenzi bora jamaa afwate ustarabu wake apige zake kazi ale watoto wake wanawake sasahivi hawa eleweki sio wake za watu wala wasichana
 
Huyu dada kakutana n tapeli za mapenzi la speed ya 4G
Hili ndio jibu la swali kwa mtoa mada.
Huyo kuna mahali alidanganywa na kupewa ahadi hewa zikamchanganya akili na kumsahau mme wake sasa baada ya kutumika kwa hizo siku alizokuwa hayupo hewani baadae kaachwa mitini ndio akili zimemrudi.
Kwa kifupi huyo hafai kuwa mke akili zake ni fupi mno yaani pamoja na kuzalishwa watoto wawili ila bado akili zake hazijamkaa sawa,kuishi na mwanamke wa aina hiyo ni hatari sana maana huko mbele ya safari akishawishiwa na mtu akuwekee sumu ili ufe kwa maslahi fulani atafanya kweli maana hajui kutumia akili
 
Wakuu nisaidieni mawazo kidogo,

Nina jamaa yangu hivi majuzi kalazimika kurudisha pesa za michango ya harusi yake baada ya mwenza wake kugoma kufunga ndoa. Ishu iko hivi jamaa anafanya kazi Shinyanga maeneo ya Kahama lakini familia maana ya mke na watoto wake wawili wanaishi Mwanza ambako wamejenga.

Baada ya kupanga na mwenzake waliyeishi nae miaka tisa kuwa sasa ni wakati wa kuhalalisha ndoa wakakubaliana vizuri. Kijana kaanza michakato na mambo yakaanza kwa kasi sana ikiwa ni taarifa kwa ndugu jamaa na marafiki am apo vikao vilianza na taratibu zingine za kikanisa.

Hivyo jamaa akawa kila anapopata likizo ni kufuatili kamati ya vikao imefikia wapi na kwa bahati hakuna kilicho haribika mpaka tarehe ikawa imeshajulikana na ikawa imebaki mambo ya kusubiri tarehe.

Ikiwa imebaki mwenzi mmoja kufika tarehe husika, ikatokea ishu ya ajabu sana yaani huyu akapata likizo kama kawaida kamtaarifu mwenzake kuwa anakuja lakini kabla ya kufika Mwanza akamwambia mwenzie kuwa atapita kwanza kwao (kwa kijana) amboko shughuli ingefanyika.

Lakini mke akamwambia aache tu kuwasumbua ndugu zake kwasababu yeye hayuko tayari kuishi nae. Kijana hakuamini ikabidi kweli aache kwenda kwao na kuelekea Mwanza ambako mbaya zaidi hakumkuta mkewe na akakuta watoto wameachwa kwa jirani. Alipouliza majirani walimjibu huyu kasema kaenda hospitali. Kijana alipojaribu kuwasiliana nae simu yake haikujibiwa.

Kijana hakuhamaki akabuy time mpaka siku iliyofuata. Baada ya hapo ilimchuku siku kama 5 bila mawasiliano na alipoona muda wa kurudi kazini umewadia na mdada hapatikani kwenye simu aliwasiliana na ukweni nako hawakuwa wanajua chochote. Jamaa akatoa ripoti polisi na ustawi wa jamii.

Hivo akachukuwa watoto wake akapeleka kwa dada yake nje kabisa ya mwanzani nyumba akaweka mlinzi yeye akarudi zake kazini. Akiwa huko baada familia yake kuchanganyikiwa walianza kumtafuta yule mdada kila sehemu waliloamini anaweza kuwepo bila mafanikio.

Baada ya wiki mbili hivi mdada akaibuka na kudai ni kweli hana mpango wa kuuishi na mshikaji kisa anadai ajisikiii tu. Basi vikao mbli mbali vya familia viakaamua hiyo mipango ya ndoa ife na jamaa akalazimika kuanza kurudisha hela za watu. Baada ya muda huyu msichana kaanza kurudi kwa jamaa eti anaomba msamaha hii ni halali jamani?.

Kisa ni cha kweli.
Anataka uendelee kuwa mchepuko , hiyo ni massive disrespect. Kama anajielewa hawez kukubali kuwa backup, ni upumbavu
 
Anrudishe ila asifunge nae ndoa awe anajipigia tu kama mlupo
 
Back
Top Bottom