SoC04 Mwenzako akinyolewa, zako tia maji: Sauti ya Kizazi Z ni sauti ya mabadiliko

Tanzania Tuitakayo competition threads

i_denyc

New Member
Joined
Jun 6, 2023
Posts
4
Reaction score
8
Neno "Kizazi Z" hutumika kuelezea kizazi cha vijana waliozaliwa mwishoni mwa miaka ya 1990 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2010. Sifa kuu ya rika hili la vijana ni matumizi ya teknolojia ya kisasa kwenye maisha yao ya kila siku kama vile simu za mkononi na mitandao ya kijamii. Hivi karibuni nchini Kenya Muswada wa Sheria ya Fedha wa 2024 uliwasilishwa Bungeni tarehe 9 Mei ambao ulipelekea jamii hii ya vijana kuonyesha uwezo mkubwa wa kuunganisha na kuchochea mabadiliko kupitia teknolojia ya mitandao ya kijamii.

Kizazi hiki kimeratibu mgomo ambao uliashiria kutoridhika na Muswada wa fedha wenye vipengele tata vyenye kuongeza gharama ya maisha kwa wakenya kama pendekezo la asilimia 16 ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye mkate, mafuta ya kupikia na huduma za pesa kwa simu. Kufuatia maandamano hayo yaliofanyika jijini Nairobi serikali ilikubali kurudisha nyuma nyongeza kadhaa za ushuru zilizopendekezwa. (Chanzo, Sura mpya za maandamano - Wanamapinduzi wa Kenya wa Gen Z wanaopinga kodi - BBC News Swahili)

Katika muktadha wa Tanzania, vijana wa rika la Kizazi Z tunapaswa kujitayarisha kwa hali zenye changamoto kama zilizowapata majirani zetu kwakua yanaweza kutufikia pia. Ingawa hali ngumu tunazo lakini tunazifumbia macho, siku yakitufika shingoni tunapaswa kuchukua darasa kutoka kwa vijana wenzetu. Miongoni mwa mambo machache ya kujifunza kwenye nyakati za kuchochea mabadiliko ni pamoja na;-​
  • Ufuatiliaji wa mambo (kuwa wasasa)
Kwa jamii yenye umri mdogo kama Kizazi Z kushirikiana kupinga jambo la kiserikali kwa idadi kubwa namna ile ya Kenya ni ishara ya kuwa wana ufuatiliaji mzuri wa mambo yanayoendelea. Idadi kubwa ya vijana inayofatilia mambo hupunguza ugumu wa kuelimisha kuhusu jambo fulani pindi inapobidi na ndio maana haikuwawia ugumu kuanzisha mgomo wa watu wengi na kwa muda mchache.

Wakiwa kwenye mgomo kulizuka utani wa kijirani kwenye mtandao wa kijamii(Instagram) dhidi ya Kizazi Z cha Tanzania ambapo Wakenya walidai kwamba kuna uwezekano vijana wa Tanzania hawajui nini maana ya Kizazi Z kwakua tupo bize kumpongeza msanii Diamond (wakimaanisha hatuna ufuatiliaji wa mambo ya msingi). Ukiangalia ni kweli vijana wetu wengi hawajui hata kama bunge la bajeti linaendelea ukiachilia mbali kusoma Muswada wa sheria ya fedha uliopendekezwa. Napenda kuwakumbusha vijana ufuatiliaji wa mambo ya kijamii sio jambo la hiari.
1E786155-EF4E-4F05-9BFF-3CCC115A892A.jpeg
Ukurasa wa mdau akithibitisha kukosa ufuatiliaji kwa Kizazi Z cha Tanzania (Chanzo, Instagram)
  • Kutosubiri vyama vya siasa kuanzisha hoja za mabadiliko ya kitaifa.
Kizazi Z cha Kenya kimeonesha kuwa hawasubiri vyama vya siasa kuanzisha ajenda za mabadiliko. Walitumia mitandao ya kijamii sio tuu kuhamasisha vijana kuja kuandamana bali na kuwaelimisha ni kwanini wanaandamana, pasipo kuhusisha vyama vya siasa. Hii ilisaidia vijana wote wa rika kuungana bila kujali tofauti ya kisiasa au kikabila kutekeleza lile walilokusudia.

Hali ni tofauti na kwetu Tanzania, ikiwa waanzisha midahalo ya mabadiliko huwa wanasiasa, watetezi wa haki za binadamu au asasi za kiraia. Vijana tumeachia hizi taasisi kuongoza maisha yetu ingawa jukumu hilo ni la kwetu wenyewe. Tumepata neema za kuwa na majukwaa yanayothamini mawazo yetu kama Jamii Forums tusiwaangushe, ni aibu kuona kwenye taifa lenye idadi ya vijana zaidi ya million 10 kupata maandiko ya fikra za vijana yasiozidi elfu mbili. Tujitathmini tunapoelekeza njia zetu.​
  • Umoja wetu/Sauti zetu ni silaha nzito ya kuiwajibisha serikali
Mgomo wowote unaofanyika kwenye nchi utakaomfanya amiri jeshi kuuzungumzia hadharani ni mgomo uliofanikiwa kwa asilimia 80%. Ilimbidi Rais Ruto aandae kikao na wanahabari kwa kumtumia mwenyekiti wa kamati ya fedha ya bunge Bw. Kimani kuuhutubia mgomo wa Kizazi Z cha Kenya. Hii inamaana kua umoja wa Kizazi Z cha Kenya kwa kiasi flani ulitikisa shughuli za kiserikali.

Sisemi kama Kizazi Z cha Tanzania hakina mambo mazuri yanayoivutia serikali yao bali mambo mengi mazuri tuliyonayo hayaiwajibishi serikali. Serikali inapenda kuwajibishwa, Serikali inatamani kuona vijana wenye uelewa wa mambo kama vijana wa Kenya. Rais Ruto alikisifia sana Kizazi Z cha Kenya kwa kuwa na kiu ya kutaka mabadiliko na kukiahidi kushirikiana nacho (Ruto Breaks Silence, Reveals What Next After Gen Z Protests). Vijana wa Tanzania tumeelekeza umoja wetu kwenye mambo yasio na msingi unakuta kijana yupo kwenye makundi saba ya mitandao ya kijamii lakini hamna kundi hata moja analopashwa habari za siasa na uchumi wa nchi yake, hali hii ni hatari kwa taifa katika kutengeneza umoja wenye tija.​
  • Kujitolea kuisemea Jamii
Muswada wa fedha uliokuwa unapitishwa bungeni unawahusu Wakenya wote bila kubagua rika. Kitendo cha Kizazi Z nchini humo kusimama na kuisemea jamii kwenye sheria zitakazokuwa kandamizi kinaashiria kwamba jamii inadeni kubwa kwa hicho kizazi hivyo kinatakiwa kiheshimike. Heshima ambayo isingepatikana bila kujitolea kwa moyo wao wote.

Vijana wa kitanzania wanapaswa kuelewa kwamba wanapaswa kuitumikia jamii yao, wanapaswa kuisemea pindi inapokuwa kimya kwenye maswala ya msingi yanayohusu taifa. Sio siasa na uchumi tuu, chochote kinachoendelea chenye uhalisia wa ukatili kinapaswa kukemewa na vijana kwa mfano ukatili dhidi ya albino ni janga linaloisumbua taifa kwa sasa hivyo ni kazi ya vijana kuisemea jamii (kukemea kwenye mitandao ya kijamii)kutokomeza ukatili huo.

Kama msemo wa Kiswahili usemavyo, maua mazuri hayakosi miiba. Migomo inasheria zake, hali ya vurugu mjini Nairobi ilipelekea vijana wengine kupoteza maisha ( Kenya finance bill: Anger after Rex Kanyike Masai shot dead during anti-tax protests - BBC News). Hivyo ni vema Kizazi Z cha Tanzania kikaonywa juu ya athari ya maandamano yasioratibiwa kwa kufuata sheria. Haki haipatikani barabarani haki inapatikana kwenye vyombo husika kwa kufuata utaratibu uliowekwa.
UJUMBE KWA SERIKALI YA TANZANIA
Uongozi unaotambua uwepo wa marika tofauti yaliomo ndani ya jamii inayoiongoza ni uongozi uliofanikiwa. Kizazi Z ni kizazi cha aina mpya ambayo Nchi yetu haijawahi kushuhudia (Hujifunza mambo kwa haraka sana kutokana na kasi ya sayansi na teknolojia). Mambo ambayo marika mengine walijifunza wakiwa wakubwa sisi tunajifunza tukiwa wadogo hivyo uelewa wetu wa kuchanganua mambo ni mkubwa. Mmetufunza tuwe wasikivu na tunalithamini sana hilo na ndio maana tunatumia majukwaa ya kidijitali (Stories of change, Jamii Forums) kupaza sauti zetu lakini uvumilivu utatushinda pale tutakapoona sauti zetu zinapuuzwa. Mmesema tujiajiri, tumeanza kujiajiri mitandaoni mnakuja na Muswada wa Sheria ya Fedha ya 2024 yenye tozo onevu kwa watengeneza maudhui mtandaoni, tuwaeleweje?. Serikali inapaswa kutuwekea miundombinu rafiki kwenye uchumi wetu kabla ya kuvuna jasho letu.​
 
Upvote 7
Neno "Kizazi Z" hutumika kuelezea kizazi cha vijana waliozaliwa kati ya miaka ya mwishoni mwa 1990 hadi mwanzoni mwa 2010. Sifa kuu ya rika hili la vijana ni matumizi ya teknolojia ya kisasa kwenye maisha yao ya kila siku kama vile simu za mkononi na mitandao ya kijamii. Hivi karibuni nchini Kenya Muswada wa Sheria ya Fedha wa 2024 uliwasilishwa Bungeni tarehe 9 Mei ambao ulipelekea jamii hii ya vijana kuonyesha uwezo mkubwa wa kuunganisha na kuchochea mabadiliko kupitia teknolojia ya mitandao ya kijamii.

Kizazi hiki kimeratibu mgomo ambao uliashiria kutoridhika na Muswada wa fedha wenye vipengele tata vyenye kuongeza gharama ya maisha kwa wakenya kama pendekezo la asilimia 16 ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye mkate, mafuta ya kupikia na huduma za pesa kwa simu. Kufuatia maandamano hayo yaliofanyika jijini Nairobi serikali ilikubali kurudisha nyuma nyongeza kadhaa za ushuru zilizopendekezwa. (Chanzo, Sura mpya za maandamano - Wanamapinduzi wa Kenya wa Gen Z wanaopinga kodi - BBC News Swahili)

Katika muktadha wa Tanzania, vijana wa rika la Kizazi Z tunapaswa kujitayarisha kwa hali zenye changamoto kama zilizowapata majirani zetu kwakua yanaweza kutufikia pia. Ingawa hali ngumu tunazo lakini tunazifumbia macho, siku yakitufika shingoni tunapaswa kuchukua darasa kutoka kwa vijana wenzetu. Miongoni mwa mambo machache ya kujifunza kwenye nyakati za kuchochea mabadiliko ni pamoja na;-​
  • Ufuatiliaji wa mambo (kuwa wasasa)
Kwa jamii yenye umri mdogo kama Kizazi Z kushirikiana kupinga jambo la kiserikali kwa idadi kubwa namna ile ya Kenya ni ishara ya kuwa wana ufuatiliaji mzuri wa mambo yanayoendelea. Idadi kubwa ya vijana inayofatilia mambo hupunguza ugumu wa kuelimisha kuhusu jambo fulani pindi inapobidi na ndio maana haikuwawia ugumu kuanzisha mgomo wa watu wengi na kwa muda mchache.

Wakiwa kwenye mgomo kulizuka utani wa kijirani kwenye mtandao wa kijamii(Instagram) dhidi ya Kizazi Z cha Tanzania ambapo Wakenya walidai kwamba kuna uwezekano vijana wa Tanzania hawajui nini maana ya Kizazi Z kwakua tupo bize kumpongeza msanii Diamond (wakimaanisha hatuna ufuatiliaji wa mambo ya msingi). Ukiangalia ni kweli vijana wetu wengi hawajui hata kama bunge la bajeti linaendelea ukiachilia mbali kusoma Muswada wa sheria ya fedha uliopendekezwa. Napenda kuwakumbusha vijana ufuatiliaji wa mambo ya kijamii sio jambo la hiari.
View attachment 3024989
Ukurasa wa mdau akithibitisha kukosa ufuatiliaji kwa Kizazi Z cha Tanzania (Chanzo, Instagram)
  • Kutosubiri vyama vya siasa kuanzisha hoja za mabadiliko ya kitaifa.
Kizazi Z cha Kenya kimeonesha kuwa hawasubiri vyama vya siasa kuanzisha ajenda za mabadiliko. Walitumia mitandao ya kijamii sio tuu kuhamasisha vijana kuja kuandamana bali na kuwaelimisha ni kwanini wanaandamana, pasipo kuhusisha vyama vya siasa. Hii ilisaidia vijana wote wa rika kuungana bila kujali tofauti ya kisiasa au kikabila kutekeleza lile walilokusudia.

Hali ni tofauti na kwetu Tanzania, ikiwa waanzisha midahalo ya mabadiliko huwa wanasiasa, watetezi wa haki za binadamu au asasi za kiraia. Vijana tumeachia hizi taasisi kuongoza maisha yetu ingawa jukumu hilo ni la kwetu wenyewe. Tumepata neema za kuwa na majukwaa yanayothamini mawazo yetu kama Jamii Forums tusiwaangushe, ni aibu kuona kwenye taifa lenye idadi ya vijana zaidi ya million 10 kupata maandiko ya fikra za vijana yasiozidi elfu mbili. Tujitathmini tunapoelekeza njia zetu.​
  • Umoja wetu/Sauti zetu ni silaha nzito ya kuiwajibisha serikali
Mgomo wowote unaofanyika kwenye nchi utakaomfanya amiri jeshi kuuzungumzia hadharani ni mgomo uliofanikiwa kwa asilimia 80%. Ilimbidi Rais Ruto aandae kikao na wanahabari kwa kumtumia mwenyekiti wa kamati ya fedha ya bunge Bw. Kimani kuuhutubia mgomo wa Kizazi Z cha Kenya. Hii inamaana kua umoja wa Kizazi Z cha Kenya kwa kiasi flani ulitikisa shughuli za kiserikali.

Sisemi kama Kizazi Z cha Tanzania hakina mambo mazuri yanayoivutia serikali yao bali mambo mengi mazuri tuliyonayo hayaiwajibishi serikali. Serikali inapenda kuwajibishwa, Serikali inatamani kuona vijana wenye uelewa wa mambo kama vijana wa Kenya. Rais Ruto alikisifia sana Kizazi Z cha Kenya kwa kuwa na kiu ya kutaka mabadiliko na kukiahidi kushirikiana nacho (Ruto Breaks Silence, Reveals What Next After Gen Z Protests). Vijana wa Tanzania tumeelekeza umoja wetu kwenye mambo yasio na msingi unakuta kijana yupo kwenye makundi saba ya mitandao ya kijamii lakini hamna kundi hata moja analopashwa habari za siasa na uchumi wa nchi yake, hali hii ni hatari kwa taifa katika kutengeneza umoja wenye tija.​
  • Kujitolea kuisemea Jamii
Muswada wa fedha uliokuwa unapitishwa bungeni unawahusu Wakenya wote bila kubagua rika. Kitendo cha Kizazi Z nchini humo kusimama na kuisemea jamii kwenye sheria zitakazokuwa kandamizi kinaashiria kwamba jamii inadeni kubwa kwa hicho kizazi hivyo kinatakiwa kiheshimike. Heshima ambayo isingepatikana bila kujitolea kwa moyo wao wote.

Vijana wa kitanzania wanapaswa kuelewa kwamba wanapaswa kuitumikia jamii yao, wanapaswa kuisemea pindi inapokuwa kimya kwenye maswala ya msingi yanayohusu taifa. Sio siasa na uchumi tuu, chochote kinachoendelea chenye uhalisia wa ukatili kinapaswa kukemewa na vijana kwa mfano ukatili dhidi ya albino ni janga linaloisumbua taifa kwa sasa hivyo ni kazi ya vijana kuisemea jamii (kukemea kwenye mitandao ya kijamii)kutokomeza ukatili huo.

Kama msemo wa Kiswahili usemavyo, maua mazuri hayakosi miiba. Migomo inasheria zake, hali ya vurugu mjini Nairobi ilipelekea vijana wengine kupoteza maisha ( Kenya finance bill: Anger after Rex Kanyike Masai shot dead during anti-tax protests - BBC News). Hivyo ni vema Kizazi Z cha Tanzania kikaonywa juu ya athari ya maandamano yasioratibiwa kwa kufuata sheria. Haki haipatikani barabarani haki inapatikana kwenye vyombo husika kwa kufuata utaratibu uliowekwa.
UJUMBE KWA SERIKALI YA TANZANIA
Uongozi unaotambua uwepo wa marika tofauti yaliomo ndani ya jamii inayoiongoza ni uongozi uliofanikiwa. Kizazi Z ni kizazi cha aina mpya ambayo Nchi yetu haijawahi kushuhudia (Hujifunza mambo kwa haraka sana kutokana na kasi ya sayansi na teknolojia). Mambo ambayo marika mengine walijifunza wakiwa wakubwa sisi tunajifunza tukiwa wadogo hivyo uelewa wetu wa kuchanganua mambo ni mkubwa. Mmetufunza tuwe wasikivu na tunalithamini sana hilo na ndio maana tunatumia majukwaa ya kidijitali (Stories of change, Jamii Forums) kupaza sauti zetu lakini uvumilivu utatushinda pale tutakapoona sauti zetu zinapuuzwa. Mmesema tujiajiri, tumeanza kujiajiri mitandaoni mnakuja na Muswada wa Sheria ya Fedha ya 2024 yenye tozo onevu kwa watengeneza maudhui mtandaoni, tuwaeleweje?. Serikali inapaswa kutuwekea miundombinu rafiki kwenye uchumi wetu kabla ya kuvuna jasho letu.​
such an insightful article. well articulated!
 
Back
Top Bottom