Mwenzangu amepata kazi Tanzania

Daah mkuu
Wacha nijilazimishe kuheshimu mtazamo wako
😅😅Yaani people 5 wasile kg 12 za Michele Kwa mwezi
Wastan Kwa kujibana kg 1 ya Michele ni watu 1
Bado bei ya mafuta, mkaa au gas.
Bado sabuni ya kufua, kuoga na kuosha vyombo, ka loshen ka shem
😅😅 Yaani budget yako hata dharula ya Pedi ya mwanamke au pampas ya mtoto hujaweka.

Ngoja nikupe budget ya kujibana ya watu 5

Michele kg 30 x2200 = 66,000
Unga kg 30 × 1500= 45,000
Mafuta ya kupika lita 5 = 25, 000
Mkaa 2000@ siku = 60,000
Maharage 2500 kg 15= 37500
Sabuni= 10,000
Maji Kwa mwezi= 10,000
Kodi Kwa mwezi = 80,000
Nauli Kwa mwezi= 30,000
Watoto shule nauli na kula labda 2
@ 1 mpe 2000= 120,000
Dharula Kwa maana mtu akiumwa, pampas, Pedi ya shem, n. K
= 50,000

Yaani hapo umejibana hata soda hujanywa,
 
Kaniacha hoi, hapo kwenye kg 12 kwa mwezi😅.
 
gari atoe wapi hata gharama ya mafuta iko juu sana
 
Akitumia huo mshahara kama mtaji anatajirika, akikamata vijana 10 wa jf akawapa biria la kahawa watembeze kila mmoja, jioni kwa siku anakusanya laki.
 
Mke na watoto awaache kijijini,aje apambane mwenyewe anachokipata anawatumia!

Kama ni 400k Tsh. Ni ndogo sana kukidh mahitaji ya familia ya watu watano.

angekuja kwanza mwenyewe aone mazingira. Na apange budget yake.
Ila pia ajitafakar. Una hama nchi ww na familia yako kisa mshahara wa laki 4?.
Watoto utawasomesha wap? kayumba? Watavaa na kula nin?.

Hiyo ni hela ya entry Level.
 
Yupo na watoto watatu na mke anataka kuja Tanzania mshahara ni 400,000 Tsh anaeza ishi wapi Dar kwa mhindi
Kwa huo mshahara na hiyo familia yake kwa dar es salaam hatoboi hata afanyaje na asipokua na akili atadanganywa analogwa.. mwambie abaki huko huko au aombe ahamishiwe rombo vijijini,simiyu,tabora, mtwara na huko lindi labda
 

Bro Budget yako haina uhalisia.
anyway tusikupangie jinsi unavyoishi.
 
Hiyo hela uloweka hapa ni nauli ya dar kwenda na kurudi kazini, chakula cha mchana kazini, maji ya kunywa kazini pamoja na pango . Hapo familia hakuna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…