ChescoMatunda
JF-Expert Member
- Jan 7, 2009
- 1,232
- 442
Tulipambana wote
Tuliumia wote
Tukajikomboa wote
Wewe mwenzangu ni mzungu?
Tulililia usawa pamoja
Tulitaka elimu ya umoja
Tulilitaka taifa letu liwe moja
wewe mwenzangu umekuwa mzungu?
Umoja wetu ulianzia nyumbani
Tukapeleka na kwa majirani
Hatukuchoka hata tuwe vitani
Wewe sasa umegeuka mzungu?
Tulikubaliana tuweke usawa
Kuanzia kabwela mpaka kawawa
Mfanyakazi mpaka mlima kahawa
mwenzangu umegeuka mzungu?
Tuliweka lugha moja bayana
Kiswahili lugha taifa bila hiyana
Na wageni waizungumze kiugwana
Vipi mwenzangu umegekia kizungu
Ukweli tuliusema bila Haya
Tuwe nyumbani ama ulaya
Hatutaki uongo mwingi usohaya
mwenzangu umekuwa mzungu?
Mgeni Njoo lakini wenyeji tupone
Tufurahi wote Usije tuacha tujikune
Wengine waja wewe uje kivingine
Kwani mwenzangu umeshakuwa mzungu?
Kumbuka tulikotoka mwenzangu
Usije sema sababu ya malimwengu
Nyumbani ni kwetu hata tule dengu
Angalia mwenzangu tusijekulia kwa kizungu.
Tuliumia wote
Tukajikomboa wote
Wewe mwenzangu ni mzungu?
Tulililia usawa pamoja
Tulitaka elimu ya umoja
Tulilitaka taifa letu liwe moja
wewe mwenzangu umekuwa mzungu?
Umoja wetu ulianzia nyumbani
Tukapeleka na kwa majirani
Hatukuchoka hata tuwe vitani
Wewe sasa umegeuka mzungu?
Tulikubaliana tuweke usawa
Kuanzia kabwela mpaka kawawa
Mfanyakazi mpaka mlima kahawa
mwenzangu umegeuka mzungu?
Tuliweka lugha moja bayana
Kiswahili lugha taifa bila hiyana
Na wageni waizungumze kiugwana
Vipi mwenzangu umegekia kizungu
Ukweli tuliusema bila Haya
Tuwe nyumbani ama ulaya
Hatutaki uongo mwingi usohaya
mwenzangu umekuwa mzungu?
Mgeni Njoo lakini wenyeji tupone
Tufurahi wote Usije tuacha tujikune
Wengine waja wewe uje kivingine
Kwani mwenzangu umeshakuwa mzungu?
Kumbuka tulikotoka mwenzangu
Usije sema sababu ya malimwengu
Nyumbani ni kwetu hata tule dengu
Angalia mwenzangu tusijekulia kwa kizungu.