Mwenzenu lipo linalonisibu naombeni msaada...

Mwenzenu lipo linalonisibu naombeni msaada...

kwanza mwambie mumeo kinachoendelea,alafu izo sms za ma2c katoe taarifa polic,mibaba mingine ndo ilivo utakuja kuta kishamtoa mtoto shuleni kampeleka kusikojulikana ili mradi kukukomoa.Mtoto ana2nziwa alafu bado analeta ngebe!
 
aisee dada pole sana naomba ongea na mumeo asimsikilize huyo jamaa na pia hizo meseji usizifute nenda kamshitaki ushahidi wako ni hizo sms iwe fundisho kwa wengine
 
nadhani mkikaa chini wewe na mmeo mtakuwa mmefanya suala la busara sana,ila mkishindwa washirikisheni wazazi wenu.polo sana, kuna watu na viatu.
 
nawashukuru sana kwa ushauri wenu wapendwa nitaufanyia kazi,samahani kwa kuchelewa kuingia hapa ndani niko class elimu ya uzeeni hii,
 
Wewe lazima usifiwe, mana umeanza kuzaa kabla ya kufunga ndoa...Usipige kelele mana kuzaa nje ya ndoa hizo ndo zawadi zake.

asante fazaa kama makosa nilishafanya na wazazi wangu walinisamehe na kunipokea na bado wakaendelea kunipa elimu,hapa nilihitaji ushauri zaidi ,anyway nashukuru kwa mtizamo wako pia
 
Mkiambiwa zinaa mbaya hamsikii, hayo ndio matokeo ya kuwafungulia kufuli wanaume ambao hawajawaoa. Astahili yakukute.

Sasa ulitegemea nini? Uzinzi na dhambi ufanye wewe ushauri utake kwetu? kila mtu atabeba msalaba wake. Unanshangaza!
 
Hakuna kinachificha damu ya mtu si sheria wala fedha. Siku moja huyo mtoto atamfuata baba yake taka usitake. Ushauri pekee kaa na mumeo mumtafute huyo BABA halali na mpange mipango ya kumpa mtoto faraja. wEKENI HASIRA MBALI. Kama ni gharama arudishe. Kumhudumia mtoto wa Mwenzio ni ubinadamu tu haihalalishi kumnyima mwenye mbegu yake UZAZI. HUO NDIO UKWELI HATA KAMA UNAUMA. FUATA USHAURI HUU HUTAJUTIA.
 
Ofcourse zinaa ni dhambi!
Lakini hakuna dhambi isiyosamehewa!? Lazima turudishe moyo nyuma na kusamehe wenzetu. Othewise dunia haitakuwa mahali pazuri pa kuishi! Iman yangu inaweza kutofautiana na yako ie mzinzi apigwe mawe hadi afe lakini asiye na dhambi na awe wa kwanza kumtupia mawe!

Ni hayo tu!
 
liwe fundisho kwa wanawake wote kuwa ukishazaa na mwanaume ukae ukijua ata apote baadae either baba au mtoto mwenye atataka kumjua mtoto au baba yake...hivyo mkiwa mwanasa mimba mlijuwage hilo sio mwajiachia tuu
 
Mkiambiwa zinaa mbaya hamsikii, hayo ndio matokeo ya kuwafungulia kufuli wanaume ambao hawajawaoa. Astahili yakukute.

Sasa ulitegemea nini? Uzinzi na dhambi ufanye wewe ushauri utake kwetu? kila mtu atabeba msalaba wake. Unanshangaza!

FF, mhusika amekubali ya kuwa amekosa, sidhani kama huu ni muda wa kumponda mwenzetu ambaye yupo njia panda, kwani maji yalishamwagika!!! Shida yake ni ushauri tu ambao utaweza kumsaidia kwa sasa.
 
Pole sana dada,
Kaa chini na mumeo muongee kuhusiana na hayo yaliyokutokea, yakubidi uwe muwazi kwake kwa kila kitu ili muweze kusaidiana kuhusiana na suala hilo.
Pia kama ikiwezekana mkae pia kikao na baba wa huyo mtoto mjue anataka nini sasa hv baada ya kumtelekeza mtotowe kwa miaka kadhaa, baada ya hapo mfanye maamuzi sahihi kwa ushirikiano wa wewe na mumeo wa ndoa. Usimuache kumuomba Mungu akuongoze katika hili.
NB:
Haina haja ya kumjibiza matusi yake hayo.
 
FF, mhusika amekubali ya kuwa amekosa, sidhani kama huu ni muda wa kumponda mwenzetu ambaye yupo njia panda, kwani maji yalishamwagika!!! Shida yake ni ushauri tu ambao utaweza kumsaidia kwa sasa.

Ukiamuwa kufanya dhambi, uyakubali yote yatayokukuta, usituingize na sisi kwenye dhambi yako. Alipofunguwa kufuli yake nje ya ndoa alikuja kutaka ushauri humu?
 
Mkiambiwa zinaa mbaya hamsikii, hayo ndio matokeo ya kuwafungulia kufuli wanaume ambao hawajawaoa. Astahili yakukute. Sasa ulitegemea nini? Uzinzi na dhambi ufanye wewe ushauri utake kwetu? kila mtu atabeba msalaba wake. Unanshangaza!
sikujua dada FF unaroho mbaya namna hii ,wewe ni mama na kama hayakukuta kwa wanao basi yatakukuta kwa wajuuu,haya mama siku njema na imani wewe ni msafi siku zote, nawashukuru wengine wote waliojitolea kunishauri hawana uchoyo wa msaada kwani mpaka sasa nimeshapata mwanga
 
Ukiamuwa kufanya dhambi, uyakubali yote yatayokukuta, usituingize na sisi kwenye dhambi yako. Alipofunguwa kufuli yake nje ya ndoa alikuja kutaka ushauri humu?

FF sijaingia JF na kusema dada FF naomba msaada wako ,nimeomba kwa watu wote na wapo walionishauri kwa nia njema kabisa na hekima zao kama wewe haukuona umuhimu huo ungeacha tu..heri wewe uliye mkamilifu na mtimilifu siku zote
 
yale yaleeeeee nayaongeleaga kila siku humu mmu,sasa nikuulize mtoa mada,mwanao ashawahi kukuuliza babake nani? Ulimjibuje?
 
Hakuna kinachificha damu ya mtu si sheria wala fedha. Siku moja huyo mtoto atamfuata baba yake taka usitake. Ushauri pekee kaa na mumeo mumtafute huyo BABA halali na mpange mipango ya kumpa mtoto faraja. wEKENI HASIRA MBALI. Kama ni gharama arudishe. Kumhudumia mtoto wa Mwenzio ni ubinadamu tu haihalalishi kumnyima mwenye mbegu yake UZAZI. HUO NDIO UKWELI HATA KAMA UNAUMA. FUATA USHAURI HUU HUTAJUTIA.

naomba uelewe post yangu Fisi huyu mtu sijamnyima mtoto amekuja kishari kwa nn mie nimkatalie mtoto wakai najua ni damu yake na iko siku mtoto mwenyewe atamtafuta baba yake,swala hapa ni miaka 13 imepita nimekaa na mtoto mwenyewe nimetunza na familia leo ndo anaibuka na kunitolea maneno makali,ndio maana niliomba ushauri hapa kabla ya kuanza kujibizana nae na wote kuonekana tuna matatizo
 
yale yaleeeeee nayaongeleaga kila siku humu mmu,sasa nikuulize mtoa mada,mwanao ashawahi kukuuliza babake nani? Ulimjibuje?

hajawahi kuuliza na ukifika muda sahihi nitamwambia..ila hili halikuhusu Bishanga swala hapa soma mada yangu na unipe jibu baba Koku:biggrin:
 
Back
Top Bottom