Mwenzenu naibiwa live mimba miezi kumi na mbili inawezekana?

nanonya

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
238
Reaction score
388
Ndugu zangu wana JF nina shida ambayo nashindwa kuitatua.

Kuna msichana mmoja nilikuwa nina mahusiano nae ya kimapenzi ila tulikuja kuachana baada ya kuona tumeshindwana kitabia.

Sasa baada ya kuachana tulikaa muda mrefu bila kuwasiliana siku moja nilitaka anirudishie computer yangu nikamkuta amevaa koti huku jua linawaka nikamuuliza kulikoni umevaa koti na jua kali?

Akadai kuwa ameamua tu ila baada ya kuachana nae masaa machache akanipigia simu na kuniambia kuwa ana ujauzito wangu, nilishangaa sana kwa sababu mimi sikukutana nae kimwili yapata miezi minne iliyopita na hakuwahi niambia kitu chochote kuhusu hiyo mimba, ila mimi nilikataa, ilipita muda yule binti akajifungua mtoto wake.

Sababu za mimi kumkataa hadi leo ni hizi zifuatazo.
1.Haiwezekani ukae na mbimba muda wa miezi minne bila kuniambia chochote ila baada ya kuniona ndio akanipigia cmu kuniambia

2.Kuna kipindi akarudi kuniomba msamaha na kunieleza kuwa amejaribu kuwa na mwanaume mwingine ila nimeshindwana nae anataka turudiane.

3.Nilimkuta amevaa koti ili kuficha mimba nisijue kuwa anamimba ila niligundua.
sababu kuu.

4.Tangu nakutane nae kimwili mara ya mwisho hadi siku aliyojifungua imepita miezi 12, je?

Inawezekana kuwa na mimba ya miezi 12?
Je kama ni wewe utakubaliana nae?

Ushauri wako wako ni wa muhimu sana jamani nisaidieni hili.

Kama una Hakika Si yako na ulishaikataa,wasiwasi wa nini? Au unarandana na kababy girl hako?
Kama bado una shaka njia pekee ya kuiondoa ni DNA.
 
kwani ungetumia Condom yangekukuta yote hayo? lakini umetaka kuusikilizia utamu na raha yake sasa unauliza kama mimba inaweza fika miezi12,amekua Tembo? kama umehesabu vizuri na unahakika sio wako basi wachana nayo,la yako unazuga huwezi kujua mtoto gani atakusaidia au utapata mwengine au laa.........
 
siulishamkataa na kwa maelezo yako sijaona uliposema umeng'ang'aniwa inaonyesha na binti nae ame move on, sasa kelele za nini tena?
 
Kitanda hakizai haramu!!!
Usimkatae mwana na rudisha urafiki wa kawaida lkn usimgegede halafu mshawishi mkapime DNA utaondoa was was ulonao!!!!!!
 
ivi wakisema kitanda hakizai haramu wanamaanisa kitandani au ata sehem zingine eg sofa wengine kwenye gar, bafuni, hata vichakan ivi vyote ni kitanda???
 
poteza tu achana nae mademu ndo walivyo hapo anataka umlee mtoto!!!!
 
nakushauli ufuatilie computer ,yako tu maana tayari mimba ulisha ikataa
 
Ndugu zangu wana JF nina shida ambayo nashindwa kuitatua.

Kuna msichana mmoja nilikuwa nina mahusiano nae ya kimapenzi ila tulikuja kuachana baada ya kuona tumeshindwana kitabia.

Sasa baada ya kuachana tulikaa muda mrefu bila kuwasiliana siku moja nilitaka anirudishie computer yangu nikamkuta amevaa koti huku jua linawaka nikamuuliza kulikoni umevaa koti na jua kali?

Akadai kuwa ameamua tu ila baada ya kuachana nae masaa machache akanipigia simu na kuniambia kuwa ana ujauzito wangu, nilishangaa sana kwa sababu mimi sikukutana nae kimwili yapata miezi minne iliyopita na hakuwahi niambia kitu chochote kuhusu hiyo mimba, ila mimi nilikataa, ilipita muda yule binti akajifungua mtoto wake.

Sababu za mimi kumkataa hadi leo ni hizi zifuatazo.
1.Haiwezekani ukae na mbimba muda wa miezi minne bila kuniambia chochote ila baada ya kuniona ndio akanipigia cmu kuniambia

2.Kuna kipindi akarudi kuniomba msamaha na kunieleza kuwa amejaribu kuwa na mwanaume mwingine ila nimeshindwana nae anataka turudiane.

3.Nilimkuta amevaa koti ili kuficha mimba nisijue kuwa anamimba ila niligundua.
sababu kuu.

4.Tangu nakutane nae kimwili mara ya mwisho hadi siku aliyojifungua imepita miezi 12, je?

Inawezekana kuwa na mimba ya miezi 12?
Je kama ni wewe utakubaliana nae?

Ushauri wako wako ni wa muhimu sana jamani nisaidieni hili.

aisee,umeuziwa roba la chupa za uhai
 
Back
Top Bottom