Mwenzenu nalia, naomba msaada!

Kudos my sister. Nakwambia fanya maamuzi haraka kwani yatakupa chance ku move forward. Wewe unavyomsamehe muda unaenda na si hajabu akaja oa huyo anayechiti nae; piga chini akajilize na yeye aone utamu; next time ata learn kubehave na kujua si kila msichana ni wa kuchezea.

Wasichana wengi wenye jeuri ya kupiga chini wanaume kama hao hawakosi another best candidate nina mifano kede kede; the opposite is true; wale wanao date cheaters wanaachwa kwenye mataa wanaolewa wengineeee.

Inabidi sasa niwe kama nyumba kubwa maana magonjwa ni mengi sana siku hizi kama mwenzi sio mwaminifu, naona hii ndio solution ya tatizo langu. Sidhani kama nimeumbwa wa kulia/kucheatiwa kila siku! I deserve the best.
 
Kwa wale ambao neno uaminifu hawajuhi lina maana gani.

Solution ni kuongea na kujua tatizo ni nini! Kama hatosikia ndo uchukue uwamuzi,sio umemfumania,unalia,anakubembeleza,unamsamehe halaf unasema atabadilika..wakati bado hujajua tatizo la yeye kucheat.... Ila Conclusion ni kwamba Mwanamke inawezekana akawa hana tatizo lolote ila tamaa za jamaa.. Dada kama ataendelea hvy kwa msamaha utakaompa. PIGA CHINI
 
Mpe muda na endelea na uchunguzi wa kina. Penye ukweli uongo hujitenga!
 
nyabafu!!!!
WEWE UFANYE MAAUZI ABAY ALAFU UOMBE MUNGU AKUSAIDIE!!! EBO!
LETS STOP THIS MUNU NISAIDIE THING NA TUWEKE AKILI SAWA HAPA....WEWE ALICHEAT MWANZONI TIME TO TAKE ACTION WAS THEN SASA HII IMETOKEA DUE TO UR LACK OF BEING DECISIVE.
ADVISE: WRITING IS ON THE WALL...TIME TO SAY GOODBYE.
 

Samahani kama ntakuumiza ila wewe jamani kama mtu alishacheat MARA KADHAA na ukamsamehe (meaning umekubali upungufu wakehuo) unalalamika nini akiendelea???Wakati unamsamehe mara zote hizo ulitegemea nini??Kwamba atajifunza kutokana na msamaha wako???

Ingekua hii ni mara ya pili ningeelewa malalamiko yako kwasababu ungekua ulimsamehe mara moja akaahidi kutorudia ukamwamini ila akajunja ahadi yake. Ila sasa wewe mara kadhaa....zote anatoa ahadi ya kuacha na bado haachi what did you expect???

Neway umeshajua ni mtu wa aina gani...sasa amua kama uko tayari kuishi maisha ya kuwa-cheated kila siku uendelee nae kama sio uangalie ustaarabu mwingine. Maana matumaini ya kubadilika hapo ni madogo kwakua umeshamzoesha kua utamsamehe...hivyo hajali sana matokeo ya matendo yake.
 
Jukwaa lina wenyewe! Watakuja kama huo msaada ulikwishapewa haikutoshi. Pole sana!
 
Ushauri mwingine bana, yaani huyu ni mchumba, na huyo dada nae anadai huyo ABu ni mchumba pia ! Na of all the things, yupo kwako na anathubutu kupokea hiyo simu, na anaongea zaidi ya mara moja. Then mara ohh mfanyakazi mwenzangu mara ohh ni rafiki ya dada....!!

Umsamehe kwa lipi, na what about siku ya ndoa wakitokea wengine (aibu mbele ya ndg na jamaa) ? Na leo hii duniani mtu anasema umweke chini ya uangalizi ???

Ndg yangu huyo ni straight red, it wasn't meant to be. Na haya magonjwa ukijifanya UNHCCR au Amref basi wewe ndiyo utaishia kubaya. Dunia ya leo wekeza ktk kazi yako na mambo mengine ya msingi ktk taaluma yako haya ya chini yatajipa tu, trust me wapo wanaume wengi tu na wako yupo somewhere, it's just a matter of time. Mark my words na utakuja thibitisha one day...


 
Ni kweli mkuu ni kazi na JF (kuwashauri watu) ndio vinaniweka busy ili niweze sahau masahibu yalonikuta ila nikiwa lonely hii picha yajirudia mara kwa mara na kujikuta nalia peke yangu chumbani, na kukosa raha muda wote!

Pole sana, punguza mawazo. Na pia usichukue uamuz wa haraka. Tulia kwa muda muweke huyo mchumba mtegoni, mtege na umpime kama anaweza kubadilika. Ukiona anaweza endelea nae.

Hata hvyo naweza kusema na ww pia una tatizo, why uchumba tu miaka minne? Umesema una kazi nzuri na yeye pia sasa kipi kinachowafanya msioane? Sisemi muoane kama bado hamjawa tayari ila at least angekua mume wa ndoa ile security ingekuwepo na ungejua unambana vipi ila haya mambo ya uchumba tu na kuonjana mmh kazi ipo.
Mungu Akusaidie
 

wewe ni nourmer ila mnakuaga na tabia za ubinafsi ,mm kuna demu mmoja alinipiga chini kisa kakuta condom kwenye droo na tuligaiwa oficini kwenye semina zetu,namshukuru mungu yeye kusepa coz nilipo sasa ni neema tu.
 
Huyo mwanaume siyo muoaji utakuta ana wachumba saba bado anachagua.

 
Dada kwa kweli inauma sana kumuacha itakusababishia mawazo mengi ila sasa hunajins kama ameanza kukuletea marinjirinji na magonjwa ni mengi.
 
nimeamua kuandika kwa herufi kubwa kuonyesha msisitizo. Hivi nyie watoto wa kike ni nani aliye walogaaa? Ku wapi kujitambua na kujithamini na kujiamini kwenu? Hivi mtakuwa satumwa wa wanaume kimapenzi mpaka lini?

Hivi we dada nikuulize ni nani aliyekudanganya kuwa huyo ndiye wako wa maisha umvumilie ktk hali yoyote hata ktk upumbavu kama huo? Kama hapo bado ungali mbichi kabisa hata dalili za mimba hujui zikoje, lakini anakufanyia hivyo, je akija kukuweka ndani nakisha kukuzalisha utakuwa na thamani tena kwake? Si hata nyumba yenyewe atahama?

Mshukuru Mungu amekuonyesha mapema kuwa huyo siyo mume. Daima sikio la kufa halisikii dawa. Siye humu tutabaki kukushauri tu but uamuzi wa mwisho unao mwenyewe, but daima tumia akili kuamua, usifuate moyo kwani moyo hauko smart.
 
Sometimes ni better kupeana nafasi. Hata mimi jamaa nilomuacha is now happily married so am I. Ndo maana nikasema there are people who are not meant for each other. Kumwacha mtu si curse; ila ukiangalia positively it could be a better decision kwa both parties as far as they were not husband and wife.


wewe ni nourmer ila mnakuaga na tabia za ubinafsi ,mm kuna demu mmoja alinipiga chini kisa kakuta condom kwenye droo na tuligaiwa oficini kwenye semina zetu,namshukuru mungu yeye kusepa coz nilipo sasa ni neema tu.
 
Nimependa hapo kwenye bold; smart people wana reason kutumia head not heart.

Ila mleta mada usikate tamaa; ujachelewa kufanya maamuzi magumu.
 
Huyo mwanaume siyo muoaji utakuta ana wachumba saba bado anachagua.

NK huwezi kujua, huyu awe mpole tu. Tatizo wanawake mnakimbilia kuachana na wapenz then later inakula kwenu au anapata mpenzi cheater zaidi.

May b jamaa amecheat kutokana na mzingira tu so kama amekiri tena kwa kulia machozi ni wazi hamtaki huyo mpenz wa nje.
So huyu atulie kwa muda apime then atoe uamuzi sahihi na sio kukurupuka tu.
 

Kila siku mazingira???HAYAKWEPEKI?
 

Duh mkuu wewe ndio umeua kabisaaaa.
Hakuna anaependa cheating ila hapa tuangalie reality zaidi mchumba amekiri na ameomba asamehewe, thus y tunamshauri huyu atulie afanye maamuzi sahihi asikimbilie tu kumuacha halafu baadae akaangukia kwa wale wenye nyumba ndogo kabisa.

Hapo atulize kwanza mzuka wa hasira upungue halafu apime aamue. Ushauri huu ni kutokana na jinsi alivyojieleza kuwa yupo njia panda na mchumba amekiri kwa kulia kuwa asamehewe.
Ni wazi jamaa anampenda huyu dada ila jamaa bado ana wenge si unajua ujana tena!
 
Kila siku mazingira???HAYAKWEPEKI?

haaah haah Lizzy bibie imagine dada amesema wanaishi mikoa tofauti so ktk mazingira kama hayo kweli?!
Then kama amekiri why asisamehewe?!
Dada atulie kwanza ampime kama ataelekea asemehe tu huo ndio uhalisia.
Nielewe kwamba sitetei cheating ila nataka dada afanye maamuz sahihi na aangalie mazingira ya kosa na kukiri kwa muhusika. asikurupuke tu
 
Hapa umemaliza yote. Akumulikaye mchana usiku anakuripua. Huyo wa kupiga na chini tu. Everm, ni bora uumie sasa kuliko kuja kuumia baadaye akisha kukuoa. Uko mdogo bado kuanza upya, tumia uzoefu wa huyu ili kujipanga upya. Utafanya kosa kubakia na huyu kicheche, tahamaki miaka imekwenda, umebaki Mama Majuto. Piga lapa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…