Mwenzenu nalia, naomba msaada!

Mwenzenu nalia, naomba msaada!

Hapo kwenye rangi nyekundu, nimeshawahi kumuambia lakini alinijibu hayupo tayari kwanza hadi asome masters ndio utakuwa muda muafaka kwake.

Halafu bado unajiuliza mara mbili mbili kama umsamehe au lah! achana nae huyo na usikurupuke kuanzisha mahusiano mengine haraka kaa muombe Mungu akupe mume ambae amekuandalia
 
Kwanza pole kwa yaliyokukuta na utanisamehe kwa mambo nitakayoongea. Hivi uchumba wa miaka minne au zaidi huwa una malengo gani? Ina maana muda wote huo bado mnasomana tu au ni nini kinachozuia huu uhusiano usipandishwe cheo na kuwa wa mme na mke? Ukweli ni kuwa huwa siwaelewi wanawake mnaowekwa kwenye hali ya uchumba kwa muda mrefu na wakati huohuo mnatoa huduma kwa wanaume kana kwamba mmeolewa. Logic ni ndogo tu kama unaweza kupata nyama, maziwa fresh, mtindi, siagi na jibini ya nini ufuge ng'ombe na kujiongezea pressure ya ufugaji inayotokana na kutafuta malisho, tiba, magonjwa etc.? Vivo hivyo kama unaweza kupatiwa lile tendo la NDOA wakati wowote unaotaka, ukafuliwa nguo, ukapikiwa na kupewa huduma zote ambazo mke anazitoa kwa mume wake kuna incentive gani kwa huyo mchumba kuoa na kujiongezea pressure sinazoambatana na kuwa na mke halali ndani ya nyumba?
 
Kwanza pole kwa yaliyokukuta na utanisamehe kwa mambo nitakayoongea. Hivi uchumba wa miaka minne au zaidi huwa una malengo gani? Ina maana muda wote huo bado mnasomana tu au ni nini kinachozuia huu uhusiano usipandishwe cheo na kuwa wa mme na mke? Ukweli ni kuwa huwa siwaelewi wanawake mnaowekwa kwenye hali ya uchumba kwa muda mrefu na wakati huohuo mnatoa huduma kwa wanaume kana kwamba mmeolewa. Logic ni ndogo tu kama unaweza kupata nyama, maziwa fresh, mtindi, siagi na jibini ya nini ufuge ng'ombe na kujiongezea pressure ya ufugaji inayotokana na kutafuta malisho, tiba, magonjwa etc.? Vivo hivyo kama unaweza kupatiwa lile tendo la NDOA wakati wowote unaotaka, ukafuliwa nguo, ukapikiwa na kupewa huduma zote ambazo mke anazitoa kwa mume wake kuna incentive gani kwa huyo mchumba kuoa na kujiongezea pressure sinazoambatana na kuwa na mke halali ndani ya nyumba?

Ni kweli nilikuwa nafanya makosa na ninajifunza kutokana na haya makosa
 
Hapo kwenye rangi nyekundu, nimeshawahi kumuambia lakini alinijibu hayupo tayari kwanza hadi asome masters ndio utakuwa muda muafaka kwake.

duh basi kama ni hvyo huyo hana mpango wa kukuoa, then huo uchumba wenu home wanafahamu ile kiukweli kuvishana pete n.k au ni uchumba tu wa mtaani?
 
Dada pole sana,ila umekosea sana uliposema wanaume sio waaminifu,wanaume wajinga wapo tena kwa namba kubwa tu japokuwa waaminifu wapo tatizo ni wachache,mimi ndo naamini hakuna mabint waaminifu mpaka nahisi story kama hizi ni za kutunga(haya ni mawazo yangu)mpaka nimeamua kuachana na mapenzi kabisa,Ushauri wangu ni kwamba ni vigumu sana kuthibitisha kuwa hatakucheat tena,kuna tatizo mahali aidha kwako au kwake,tafuteni muda mjikague ili mmalize tofauti zenu!Huwa nawaza wakati natafuta mtu wa kumpa zawadi iliyokosa mpaji kwanini sikukutana na watu kama nyie(kama ni kweli uliyosema)ila kwa sasa sitaki mapenzi,msamehe maisha yaendelee!
 
Dada Evarm, sio wanaume tu waio waaminifu... siku hizi dunia imeisha kabisa tena sana, Mimi ni mwnaume na yaliyokukuta wewe yamenikuta pia tena yalikuwa mabaya sana... msichana wangu alikuwa anakuja nyumbani kwangu na simu zinapigwa kama zilivokuwa zinapigwa za huyo mtu wako, ukiuliza story ni zile zile ulizopewa wewe, udanganyifu..udanganyifu... baadae nikaagwa kuwa mchumba wangu anaenda kwa mjomba wake mahali fulani, alipofika huko mawasiliano yakawa mgogoro, anapatikana dk 5 au kumi tu kwa siku nzima, kumbe yupo kwa mwanaume mwingine na ni X wake wanakula raha...mungu hamfichi mnafki, siku ya sku yule mwanaume akashuku akanipigia simu kuuliza kwa nini namsumbua mtu wake? maelezo alopewa ni kuwa mimi jamaa tu flan nasoma na huyo mdada na eti ninamtaka ila yeye hanitaki, lakini akinipigia simu honey na sweete kama kawa... baada ya mambo kubumbuluka dada akajihami kwa kunipigia simu na kunitukana matusi ya nguoni kuwa mi si kitu wala nini, na wakati huo nilikuwa namsaport kulipa gharaza zake kadhaa za chuo maana alikuwa anasoma na pia nilikuwa namsomesha mdogo wake chuo nikijua naanda familia yangu ya baadae.

Yule X alipokutana na haya akamfukuza akamwambia hamtaki, akarudi kwangu akalia sana eti shetani alimpitia na sijui kwa nini alisema vile na kunitukana.... lazima niseme mimi ni mtu wa ajabu maana nilimsamehe na tukaaza upya uhusiano japo alinipunguzia kasi ya kumpenda lakini bado nilijituma kwake...

Nataka nikuambie kitu nilichojifunza, huyu dada hakubadilika hata na aliendelea kunisumbua kila kukicha na wanaume, kila siku usiku hata wa manane ni simu za wanaume zenye mandhari ya mapenzi pamoja na sms amabazo zikiingia tu zinafutwa, niliumia sana na kujitahidi kueleaza hisia zangu kwake juu ya ninavyojisikia, akiniumiza ataliaa na kusema amekosa na hatarudia lakini hazipiti siku mbili kesi ni ile ile... alinitesa na alinitesa sana maana mimi sio mtu ninayekata tamaa haraka.. kila siku nilijipa moyo labda kesho mungu atamdadilisha lakini haikuwa hivyo zaidi ya miaka 3 aliendelea kunitesa tangu nilivo mrudia baada ya kutoka kwa X wake....hatimaye mwishoni nilipiga moyo konde ni kasema IMETOSHA!!! NikaQuit.

Sasa dada amechoka umri unaenda na wale walokuwa wanamdanganya hawapo tena na hakuna wa kumuoa...ananisumbua kila siku na namwambia haitakuja kutokea mimi kumwoa hapa duniani.. analia lakini mimi moyo ni mtupu juu yake, sina feelings zozote!! Am done with her..

napenda kukuambia:-

1. kama mtu ameanza kukufanyia hayo sasa hataacha milele, maana wengine wanafanya haya ndivyo walivyoumbwa ndivyo walivyo!!! ataendelea kukudanganya tuuuu huko mbeleni, ameshaonja asali atataka kuchonga mzinga, so please usifanye kosa la kumrudia hata utajuta

2. inauma sana na najua inauma...ilinichukua mwaka mzima tangukumwacha na japo kaunza kusahau, lakini kama ukiwa na nia utaweza kumsahau...njia rahisi kata mawasilianao nae, usiruhusu akupigie simu wala akutumia email tangu sasa..

3. usiingie kwenye mahusiano mapema sasa hivi...jipe muda kuponya moyo wako na baada ya muda miezi 6 au mwaka ukiwa umepona jaribu kuanza mahusiano mapya...ukiingia sasa hutasahau mana wingu la ulichofanyiwa litakuwinda popote uendapo, so please don't make that mistake.

4. mda mwingine ukianzaisha uhusiano usijitoe kwa asilimia 100% kwa mwanaume, binadamu wote (wake kwa waume) wakijua wanapendwa ndivo walivo na wanadhani no way out for you...penda ila pia jiwekee msimamo fulani ambao mtu wako ataunote..usikubali akutese hata..


All in all pole sana, yanawakuta wengi na mimi ni mhanga mmoja wapo...katika kipindi hiki Omba sana mungu hata kama imani yako ni ndogo maana MKe/Mme bora hutoka kwa bwana... anaweza kuchelewa kujibu lakini ukiomba kwa imani atajubu..
Pole na narudia tena Pole sana..
 
Asante sana Songito, nashukuru kwa ushauri mzuri!
 
RR Sijamteea jamani natambua Men amekosea ila bado mdada hapaswi kukurupuka tu anatakiwa atulie kwanza hasira ziishe halafu apime na kuamua ataangalia mwenyewe kama men wake inawezekana ku change au haiwezekani.
sipendi uongo ktk mahusiano ukweli inaumiza. vipi jamaa anaweza kujitetea ili tujue kilichompelekea huko ni nini ili kuwepo na rational decision?
 
duh basi kama ni hvyo huyo hana mpango wa kukuoa, then huo uchumba wenu home wanafahamu ile kiukweli kuvishana pete n.k au ni uchumba tu wa mtaani?

Pande zote mbili za wazazi wanafahamu hili na ndio maana nilitaka kuongea na mamake kuhusiana na hili lakini nikahisi watabadili msimamo wangu, na ndio maana nikaomba ushauri huku kwenu wadau.
 
Kama kulia umeshalia, umeumia. Tatizo ni nini??? Unashindwa kuwa na msimamo wa maamuzi yako???? Achana nae mara moja. Humuwezi huyo haka kidogo, kama ulikuwa na mpango wa kuishi naye milele sahau mara moja. Hakufaiiiiiii!

one mistake one goal. Hiki ni kipindi kigumu cha uchaguzi wa nani awe mume wako. Ukifanya kosa tu, utalia na kubeba msalaba wako hadi unaingia kaburini.
 
Mi naomba nikushauri vitu viwili
1. Unafanya kosa kama utaamua kumuacha na uishi peke yako kwa kuwa unaamini unajimudu kikipato kama ulivyosema kwani kipato ulikuwa nacho still ukawa nae so jamaa anaumuhimu wake bwana
2. Kuwa makin kwan hujui mchumba mwenza alikuwa anaumwa nini maana kwa maelezo yako hakuulizwa na alikazania kusema kuna tatizo.........tatizo gani[mimba?] bora iwe mimba na mungu apishilie mbali janga la kisasa najua utaumia ila ndo uhalisia ebu jisumbue kapime tafadhar
 
huyo mwanaume si mwaminifu. na hapo bado ni uchumba je akisha kukuoa si ndo itakua bara. wewe tulia utapata mwingine ambae ni chaguo lako. tena unakazi.
 
dah...pole sana.....ningekuwa na uwezo ningekuazima roho yangu....ina mashokabzoba mpaka raha.....
ila kama imetokea juzi juzi jumamosi....hebu jipe muda wa kutafakari....maamuzi ya harakaharaka si mazuri....yanaweza kukugharimu.........
hebu fuata huo ushauri hapo juu unaweza kukusaidia kwani kwenye mapenzi kuna kukosana lakini mapenzi mazuri yanaendana na msamaha bila hivyo utakuwa unachukua mpya na kuacha mwishowe utajikuta used mpaka unajionea aibu.
pole sana
 
Uskurupuke,rudisha kumbukumbu kama iyo tabia na nyuma alikuwa nayo,kama sio mrudie ila kwa masharti na mikakati mikubwa,lakn wote mnafanya kazi bado tu kuoana?mhhhh...kuwa makn usje kuwa dekio
 
Pole saana kwa shock; ila ngoja nikwambia jinsi nilivyoishi maisha yangu ya ujana; Sikuwa na msamaha wala uvumilivu na the so called boyfriend wala mchumba; na imenisaidia kupata mume ambaye naweza kusema ni right for me and am not regreting my 8 years of marriage.

Kama ameanza cheating mkiwa wachumba mwanawane huyo atakuwa analala nje kabisa akikuoa am telling you; people rarely change.

Na kingine kilichonifanya nisiwe na msamaha na hao ma boyfriend (sijawahi kuwa na wachumba zaidi ya mume wangu ila angenichiti ningepiga chini fasta) ni kwa kuwa mtu huwezi jua nani kati yenu anadanganywa. Hata wewe hapo ulipo yawezekana kabisa ukawa "the other woman" ndo maana mwenzio akawa na confidence ya kukujibu hovyo.

Nyie ambao hamjaolewa mko huru kuchagua what is best for you na kupiga mtu chini ni very easy kwani hamna mkataba wowote.

Nilimwachaga boyfriend wangu baada ya kumuona AMESIMAMA na msichana kimahaba; jamaa hakuamini na mpaka kesho anasema eti nilikutana na mapedeshee ndo maana nikamuacha kwani hakuona kuwa ilikuwa ni sababu ya msingi (but it was maana walivyokuwa wamesimama hakukuwa na mjadala alikuwa anamega). Sikumpa hata muda wa kujieleza maana najua wanaume wana mashairi ya kutupumbaza. BUT the truth ni kuwa nilipiga chini wakati sikuwa na hata ninayemuwazia kichwani na nilikaa single for a year ndo nikaanza dating my hubby.

Na my way of reasoning ni kuwa wanaume wengi ni wepesi wa kuchiti wakiwa kwenye ndoa kwa kuwa kuna kuzoeana na kind of kuchokana; Sasa hainijii akilini mwanaume anaye mchiti girlfriend ambaye wanaonana kwa msimu. Hence nilipokuwa naona boyfriend anachiti nili conclude kuwa he is not into me. Sasa ya nini kumganda mtu ambaye penzi langu alijampagawisha. Hence I would rather wait for a man who was meant for me.

Wewe usimpeleke chaka mwanamke mwenzio! Biblia imeandika hivi; ''Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu''. Wakati huo ni sasa! Wanaume wote ni watoto wa baba mmoja hivyo ukishikwa shikamana.
 
Eti umesema una kazi yako? Na unajitegemea? Na huyo ni mchumba ashaonyesha udhaifu? Piga chini tena tupa kulee source. Teamo
 
Back
Top Bottom