Mwenzenu Napita kipindi kigumu sana

Mwenzenu Napita kipindi kigumu sana

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,131
Reaction score
937
Napita kipindi kigumu sana

Siku moja nikiwa sehemu nilihisi kama kitu kimenipiga usoni, nikapoteza nguvu ghafla, nikakaa kwa muda. Nikaomba msaada, ndugu akanisaidia.

Nikalala, asubuhi nilipoamka nikawa na homa kali, Nikaenda hospitali wakanigundua nina malaria, nikatibiwa. Baada ya Wiki, nilipomaliza tu Dozi nikaanza kujisikia tena kama malaria, nikapima, nikaambiwa nina acid nyingi tumboni, vidonda vya tumbo, nikatibiwa nikapona.

Baadae mapigo ya moyo yakaanza kwenda mbio, ukilala unatamani kuamka, ukamka unataamni kutembea, ukitembea, unatamani kukaa chini n.k... Wakati Fulani nikila baadhi ya vyakula ikiwemo asali, Tangawizi, Green Tea, mwili unavuruga sana kama mtu mwenye BP na pengine ukifanya tendo la ndoa, hali ya mwili inabadilika kama umechomwa motoni, unaugulia. Nikapima BP wakaniambia ipo kawaida, nikaenda kuangalia vipimo vyote vikubwa ikiwemo mfumo wa damu, moyo, Mkojo, tumbo n.k. Majibu yakawa "NEGATIVE" kwa vipimo vyote.

Ilifikia wakati hata kazini najisikia sitaki kwenda, siwezi, nikiamka tu kichwa kinauma, mwili unatetemeka, miguu inaishiwa nguvu. Nimekuwa mdhaifu kwa muda, sasa naendelea vizuri lakini wakati Fulani ukikaa unahisi kama kuna mzigo mzito kichwani, kichwa kinauma utosini, tumbo linavuruga na gesi nyingi...pengine unachoka sana

Naomba msaada wenu waungwana.
 
Mh pole sana mkuu, hapo inawezekana hata mambo ya 'kiswahili' yanahusika, hebu kama ww ni mkiristo nenda kafanyiwe maombi kanisani!
 
ngoshwe

Ndugu yangu usupoteze muda huko mahospitali, yashanikuta hayo
Nenda kwa watalaam wa kiswahili aisee mungu atakufanyia wepesi.pole sana
 
Last edited by a moderator:
ngoshwe , habari za kutwa na maisha... POLE tena pole sana Moula Kareem akuponye!! Jaribu kutumia tiba, Tiba ya kunywa maji ya moto (3 glasses of warm water x 3 a day) ! Natumai itakusaidia.
 
Last edited by a moderator:
Mungu kawapa kalama ya kuwaokoa wanadam katika mitihani mbali mbali kama madaktari kama uamini subiri yakukute ndo utajua kuwa wao ni nani ndugu.

Amewapa karama kwa kutumia majini kuwaokoa wanadamu!!!! kwani chanzo cha tatizo la ngoshwe si inaweza kuwa ni hao hao waswahili?
 
Last edited by a moderator:
Amewapa karama kwa kutumia majini kuwaokoa wanadamu!!!! kwani chanzo cha tatizo la ngoshwe si inaweza kuwa ni hao hao waswahili?

Kama vipimo vyote havioneshi ugonjwa sasa watatibu nn, mi nina ushuuda hayo mambo na yalishanikuta mwaka jana ndo maana namshauri aende akacheki na huko, hapa duniani tunaishi na viumbe wengi wema na wabaya usiombe yakukute, na nilishaleta uzi hapa
 
Last edited by a moderator:
Kama vipimo vyote havioneshi ugonjwa sasa watatibu nn, mi nina ushuuda hayo mambo na yalishanikuta mwaka jana ndo maana namshauri aende akacheki na huko, hapa duniani tunaishi na viumbe wengi wema na wabaya usiombe yakukute, na nilishaleta uzi hapa
Sasa kwa kuwa wewe yalikukuta na ukatibiwa huko ndio uje useme kuwa mungu kakusaidia? au unataka kuleta kufuru tu? wewe ulienda huko na unaweza kumshauri aende au asiende lakini msaada wa huko mungu hausiki, ni nguvu za giza tu, na ndio hao hao wanaosababisha albino wanakatwa mikono na miguu.
 
ngoshwe

Lazima utakuwa umerogwa, ni pm nitakupa contact ya mganga atakusaidia sana
 
Last edited by a moderator:
Pole. Nenda hapo kkkt kimara korogwe. Hasa jumamosi. Pana maombi.

Usisahau kufuata masharti ya matabibu.
 
Back
Top Bottom