ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 937
Napita kipindi kigumu sana
Siku moja nikiwa sehemu nilihisi kama kitu kimenipiga usoni, nikapoteza nguvu ghafla, nikakaa kwa muda. Nikaomba msaada, ndugu akanisaidia.
Nikalala, asubuhi nilipoamka nikawa na homa kali, Nikaenda hospitali wakanigundua nina malaria, nikatibiwa. Baada ya Wiki, nilipomaliza tu Dozi nikaanza kujisikia tena kama malaria, nikapima, nikaambiwa nina acid nyingi tumboni, vidonda vya tumbo, nikatibiwa nikapona.
Baadae mapigo ya moyo yakaanza kwenda mbio, ukilala unatamani kuamka, ukamka unataamni kutembea, ukitembea, unatamani kukaa chini n.k... Wakati Fulani nikila baadhi ya vyakula ikiwemo asali, Tangawizi, Green Tea, mwili unavuruga sana kama mtu mwenye BP na pengine ukifanya tendo la ndoa, hali ya mwili inabadilika kama umechomwa motoni, unaugulia. Nikapima BP wakaniambia ipo kawaida, nikaenda kuangalia vipimo vyote vikubwa ikiwemo mfumo wa damu, moyo, Mkojo, tumbo n.k. Majibu yakawa "NEGATIVE" kwa vipimo vyote.
Ilifikia wakati hata kazini najisikia sitaki kwenda, siwezi, nikiamka tu kichwa kinauma, mwili unatetemeka, miguu inaishiwa nguvu. Nimekuwa mdhaifu kwa muda, sasa naendelea vizuri lakini wakati Fulani ukikaa unahisi kama kuna mzigo mzito kichwani, kichwa kinauma utosini, tumbo linavuruga na gesi nyingi...pengine unachoka sana
Naomba msaada wenu waungwana.