Mwenzenu nimeachwa kweli!

Mamy K

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
3,154
Reaction score
11,082
Habari za jioni!

Jamani mwenzenu jana nimezinguana na baba watoto, katika purukushani nikamwambia niache nitikise kibiriti, akanijibu subiri. Sijakaa vizuri imeingia sms "Mimi baba Kidogoli nimekuacha Mamy K talaka 1, siyo mke wangu".

Yani hapa nipo nipo sijui nilie, sijui nicheke, nahisi Kisukari si Kisukari, Covid si Covid! Wanazuoni njoni mnishauri hiyo si talaka tayari? Hivi kweli mkeo unayempenda akikwambia niache unamwambia hivyo, kuna mapenzi hapo?

Nipeni ushauri maana kesho anarudi nyumbani najua ataanza kunibembeleza na kunambia hakuwa anamaanisha. Kuna mapenzi hapa?
 
Hata wewe mumeo unayempenda utamwambiaje akuache,niache?
Unapenda kujiona wewe ndio umekosewa ikiwa wewe ndio mkosaji

Kwanza tutafahamu vipi kama unampenda ?usingemtamkia
 
Tatizo kuu la wanawake almost wote ni KAULI.

Huwa mnatoa kauli ngumu sana mkiwa na hasira.. Zikishawatoka hizo hasira ndo huwa mnabaki kujuta haswa
 
Na wewe mumeo hauwezi kumwambia hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…