Mwenzenu nimegundua siri kubwa ya mafanikio ni ubahili

Hizo hela unazoziweka utakuja kuzitumia lini?? Ni lini utakapoanza kuishi maisha ya uhuru na amani?
 
Shikamoo chosen generation,mm n mchaga ila ubahili noo kwa kweli,maisha n mafupi mnoo
 
Mkuu una sifa nzuri sana, jaribu kutafuta mchumba hapa JF please!! [emoji1][emoji1][emoji1]
 
Ubahili ni lugha ya kejeli. Neno sahihi ni Budgeting (mipango sahihi ya utumiaji rasilimali fedha)
 
Ushauri mzur lkn ungetumia neno Nadhani badala ya Ubahili... hata ivo umeeleweka sana
 
Mi tangu mwaka Jana nimekuwa bahili sana kwakweli kiasi kwamba kuna watu watu wananisema vibaya sana

Halafu cha ajabu wanakuja kukopakopa kwangu kila siku na wanaboa sana hawarudishi mapema

Ubahili unalipa

Kuna watu nafahamiana nao wana madeni balaa kwa kukopAkopa ovyo bila malengo

Na ni hodari wa kuzika hela sehemu zisizo na tija


Bado sijaoa na. Kwangu kitu cha pekee cha thamani nilichonacho ni smartfoni hii ya huawei na kitanda nilichonunua pale mkata .

Lakini huko bank ni tarakimu ndefu tu.

Sijaona faida ya kuwa na makolokolo mengiii ambayo hayaniletei pesa zaidi ya kunilia pesa

Na ubahili wangu ulianza kutamalaki zaidi nilisoma kitabu cha rich dad poor dad cha kiyosaki

Tangu hapo kila senti inayoingia kwenye mfuko wangu naipa thamani mara mia zaidi

Sijui may be baada ya five years nitafunguli mbwa[emoji3]
 
"Hamtaifikia ladha ya imani mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda".
Punguza matumizi yasio na lazma ila asili ya ubahili ni roho mbaya.
 
Kuna kaka mmoja alisoma engineering Urusi, alipitia UK kuweka maisha sawa kwanza kabla hajarudi nyumbani. Ilikuwa miaka ya 90's huko, wakati hule Heathrow unaingia bila viza. Mtaani alipata kazi ya ujenzi, wanaofahamu kazi hizo ulaya zinalipa vizuri kidogo kulinganisha na non skilled labour nyingine.

Yule kaka alipanga chumba kidogo kuliko vyote kwenye nyumba aliyopanga, ili kubana pesa. Akiwa off luxury kubwa ilikuwa chai ya maziwa na mkate na mayai ya kukaanga. Alituma pesa nyumbani anunuliwa kiwanja, alijenga nyumba, alinunua gari akaituma kwa Dewji wakati huo. Baada ya kuweka mambo sawa amerudi nyumbani, hakukaa hata miezi mitatu alifariki, wanadai alipata TB na zile kazi ngumu za ujenzi alizofanya ziliongeza udhoofu wake.
 
Mkuu leo nimejua ID yako...Uliposema tu Kitanda na HUAWEI. Ila dem wako mbona umemnunulia sofa na kodi unamlipia?
 
Jamnnnn...How sad!!!
 
Mkuu leo nimejua ID yako...Uliposema tu Kitanda na HUAWEI. Ila dem wako mbona umemnunulia sofa na kodi unamlipia?
Hahahahahah hakuna kitu kama hicho hapa ni mwendo Wa kubana matumizi ili nije nitusue bidae .

Nina miezi minne hata bia za mwendo kasi sijanywa .

Nina miezi mitatu sijachimba mgodi .

Aisee nimekuwa bahili hadj nimepauka ngozj napaka baby care mwezi Wa sita huu .

Spray yangu ya mwisho kununua ilikuwa agosti mwaka Jana na ndo imeisha hivi tarehe 6 Jana

Nikipika chakula nakula siku tatu hahahahah

Viatu vyangu vimeisha upande nguo zimefuba kichizi nywele nanyolea DORCO

Acha tu


Ila kila nikitazama Salio kwa simbanking nafsi inasuuzika barabara![emoji3]
 
Nilijifunza kubalance kati ya kuenjoy na kuweka, huku kujinyima sana si kuzuri.
Mimi whenever I get money lazma kuna percent nataka nkale bata...
Habari za kusema nisev weeeeeee mpka nguo zinipaukie mwilini sinaga
Lbda hawa wenzet mabahili wataspend hizo hela kaburini that's if kuna malls down there[emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Kuna njemba mmoja ya Kijapan jina lake alikuwa ni Shigeyuki Uzu. Jamaa alikuwa mchapa kazi mzuri sana na hata siku moja hakuwahi kukosa kazini kwake. Ila Shigeyuki alikuwa bahili wa kutupa akishindia mikate mikavu na maji ya kunywa na pesa zake zote aliweka bank na kufanikiwa kuwa na account nono. Siku moja hakutokea kazini baada ya siku tatu za Shigeyuki kutoonekana kazini wenzie wakazuka nyumbani kwake na kumkuta amekufa. Mwili wa Shigeyuki ukafanyiwa uchunguzi ndipo iliposemekana kifokilisababishwa na lishe duni ya Shigeyuki pamoja na kuwa account yake ilikuwa na pesa nyingi sana. Fanya ubahili wako wote lakini usisahau kula vizuri ili usije kuwa Shigeyuki Uzu mwingine.

 
man earns money to get material welfare. Endelea tu kujifanya bahili
 
tufanye ubahili wote ila sio mpaka kwenye kula nakwambia akiba yako utaitumia kweny matibabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…