Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shikamoo chosen generation,mm n mchaga ila ubahili noo kwa kweli,maisha n mafupi mnooItakuchukua miaka mingapi kuishi maisha ya namna hiyo?! Kujibana?!
Acheni kucomplicate maisha ... Mungu kakupa zawadi ya uhai kuishi hapa duniani; Ifurahie, mwabudu YEYE na U enjoy maisha (ndivyo alivyowaambia wanadamu wa kale) kwa kuwa zawadi hii ni ya muda mfupi tu..!
Mkuu leo nimejua ID yako...Uliposema tu Kitanda na HUAWEI. Ila dem wako mbona umemnunulia sofa na kodi unamlipia?Mi tangu mwaka Jana nimekuwa bahili sana kwakweli kiasi kwamba kuna watu watu wananisema vibaya sana
Halafu cha ajabu wanakuja kukopakopa kwangu kila siku na wanaboa sana hawarudishi mapema
Ubahili unalipa
Kuna watu nafahamiana nao wana madeni balaa kwa kukopAkopa ovyo bila malengo
Na ni hodari wa kuzika hela sehemu zisizo na tija
Bado sijaoa na. Kwangu kitu cha pekee cha thamani nilichonacho ni smartfoni hii ya huawei na kitanda nilichonunua pale mkata .
Lakini huko bank ni tarakimu ndefu tu.
Sijaona faida ya kuwa na makolokolo mengiii ambayo hayaniletei pesa zaidi ya kunilia pesa
Na ubahili wangu ulianza kutamalaki zaidi nilisoma kitabu cha rich dad poor dad cha kiyosaki
Tangu hapo kila senti inayoingia kwenye mfuko wangu naipa thamani mara mia zaidi
Sijui may be baada ya five years nitafunguli mbwa[emoji3]
Jamnnnn...How sad!!!Kuna kaka mmoja alisoma engineering Urusi, alipitia UK kuweka maisha sawa kwanza kabla hajarudi nyumbani. Ilikuwa miaka ya 90's huko, wakati hule Heathrow unaingia bila viza. Mtaani alipata kazi ya ujenzi, wanaofahamu kazi hizo ulaya zinalipa vizuri kidogo kulinganisha na non skilled labour nyingine.
Yule kaka alipanga chumba kidogo kuliko vyote kwenye nyumba aliyopanga, ili kubana pesa. Akiwa off luxury kubwa ilikuwa chai ya maziwa na mkate na mayai ya kukaanga. Alituma pesa nyumbani anunuliwa kiwanja, alijenga nyumba, alinunua gari akaituma kwa Dewji wakati huo. Baada ya kuweka mambo sawa amerudi nyumbani, hakukaa hata miezi mitatu alifariki, wanadai alipata TB na zile kazi ngumu za ujenzi alizofanya ziliongeza udhoofu wake.
Nilijifunza kubalance kati ya kuenjoy na kuweka, huku kujinyima sana si kuzuri.Jamnnnn...How sad!!!
Hahahahahah hakuna kitu kama hicho hapa ni mwendo Wa kubana matumizi ili nije nitusue bidae .Mkuu leo nimejua ID yako...Uliposema tu Kitanda na HUAWEI. Ila dem wako mbona umemnunulia sofa na kodi unamlipia?
Mimi whenever I get money lazma kuna percent nataka nkale bata...Nilijifunza kubalance kati ya kuenjoy na kuweka, huku kujinyima sana si kuzuri.
Maisha hayampangii mtu namna ya kujiendesha bali mtu anayapanga maisha yaendeje baada ya kukaa mda mrefu nimegundua nilikuwa mjinga sana nimechelewa mno kwa kutokuweza kuyatawala maisha lakini sasa nimejifunza nahisi sitorudia kosa.
Nilichogundua ili kufanikiwa lazima uwe bahili sana, unatakiwa ujinyime sana, kuheshimu pesa kwa kiwango cha juu, kufanya mambo ya lazima na muhimu kutotumia pesa kufanyia kitu kisicho cha lazima.
Pili ili pesa zikae jaribu kutokutafuta sifa za kijinga kama kufanya kitu kwa kutumia pesa ili uonekane unazo hapo utakuwa umepotea kabisa, ni vyema uonekane huna pesa kumbe unazo utajikuta mambo yako yanaenda vizuri.
Ogopa sana kukopa pesa zisizo na ulazima, pale unapobanwa jaribu kuvumilia changamoto unazokumbanazo
Ili kushinda yote hayo jiwekee malengo katika pesa unazopata kila mwezi au kila siku jipangie kiasi cha kuweka akiba hata kama akiba ndogo we weka na hakikisha kila mwezi unafikisha kiasi ulichojiwekea. Kama mwezi mwingine utapata na matatizo usipofikisha kile kiasi hakikisha unaongeza kiasi kwa miez ijayo ili kufidia kiasi kilichopotea.
Mafanikio yanakuja kwa kuweka akiba na kuheshimu pesa kwa kiwango cha juu, hayo yote yatawezekana ukiwa bahili wa kutupwa.
man earns money to get material welfare. Endelea tu kujifanya bahiliHahahahahah hakuna kitu kama hicho hapa ni mwendo Wa kubana matumizi ili nije nitusue bidae .
Nina miezi minne hata bia za mwendo kasi sijanywa .
Nina miezi mitatu sijachimba mgodi .
Aisee nimekuwa bahili hadj nimepauka ngozj napaka baby care mwezi Wa sita huu .
Spray yangu ya mwisho kununua ilikuwa agosti mwaka Jana na ndo imeisha hivi tarehe 6 Jana
Nikipika chakula nakula siku tatu hahahahah
Viatu vyangu vimeisha upande nguo zimefuba kichizi nywele nanyolea DORCO
Acha tu
Ila kila nikitazama Salio kwa simbanking nafsi inasuuzika barabara![emoji3]
tufanye ubahili wote ila sio mpaka kwenye kula nakwambia akiba yako utaitumia kweny matibabuHahahahahah hakuna kitu kama hicho hapa ni mwendo Wa kubana matumizi ili nije nitusue bidae .
Nina miezi minne hata bia za mwendo kasi sijanywa .
Nina miezi mitatu sijachimba mgodi .
Aisee nimekuwa bahili hadj nimepauka ngozj napaka baby care mwezi Wa sita huu .
Spray yangu ya mwisho kununua ilikuwa agosti mwaka Jana na ndo imeisha hivi tarehe 6 Jana
Nikipika chakula nakula siku tatu hahahahah
Viatu vyangu vimeisha upande nguo zimefuba kichizi nywele nanyolea DORCO
Acha tu
Ila kila nikitazama Salio kwa simbanking nafsi inasuuzika barabara![emoji3]