HOJA Mwezi mmoja tokea taarifa ya Dkt. Nchimbi kujiuzulu: ‘Yupo wapi?’ Nani wa kulijibu swali hili

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Agosti 25, 2026, taarifa ilisambaa kupitia mitandao ya kijamii ikieleza kuwa Dkt. Emmanuel John Nchimbi amejiuzulu wadhifa wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku akitangaza pia kustaafu siasa na utumishi wa umma. Katika barua yake, Nchimbi alisema kujiuzulu kwake kungeanza rasmi Septemba 4, 2026.

Taarifa hiyo haikuwa tu “breaking news”, bali ilifungua mjadala mpana kutokana na nafasi aliyokuwa nayo Nchimbi na mazingira yaliyokuwa yamezunguka uamuzi huo.

Itakumbukwa kuwa kabla ya taarifa hiyo kulikuwa na taarifa na madai kuhusu Nchimbi kushinikizwa kujiuzulu. Gazeti la Mwanahalisi lilichapisha taarifa iliyodai kuwa mwanasiasa huyo alikuwa amegoma kujiuzulu. Gazeti hilo lilifungiwa siku chache baadaye kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuchapisha taarifa ya uongo. Baadaye, barua ya kujiuzulu kwa Nchimbi ilisambaa mitandaoni na hatimaye uamuzi huo ukathibitishwa rasmi.

Wakati mijadala hiyo ikiendelea, Ikulu ilithibitisha kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amepokea na kukubali ombi la Nchimbi kujiuzulu. Mchakato wa kumpata mrithi ukaanza kupitia CCM, ambayo ilimpendekeza Deogratius Ndejembi. Bunge baadaye lilimthibitisha Ndejembi kuwa Makamu wa Rais mpya badae aliapishwa rasmi.

Hata hivyo, kabla ya tarehe iliyotajwa kwenye barua ya Nchimbi kufika, CCM ilitangaza kumvua uanachama kwa sababu za kinidhamu na kimaadili, huku Mwanasheria Mkuu akieleza Bungeni kuwa kupoteza sifa hiyo kulifanya Nchimbi asiendelee kuwa Makamu wa Rais kuanzia Agosti 26, 2026.

MWEZI UMEPITA BILA KUONEKANA

Mwezi mmoja tangu taarifa hiyo, swali limeibuka kwa namna nyingine: Dkt. Emmanuel Nchimbi yuko wapi?

Tangu kujiuzulu kwake, Nchimbi hajaonekana hadharani katika matukio ambayo baadhi ya watu walitarajia angehudhuria. Aidha, mabadiliko ya uongozi yalifanyika na Ndejembi akaanza kutekeleza majukumu yake kama Makamu wa Rais mpya. Hata hivyo, kumekuwa na sintofahamu kuhusu kama kulifanyika au kulikuwa na sababu gani za kutofanyika kwa makabidhiano ya ofisi hadharani.

Swali hilo limeendelea kujitokeza pia katika mijadala ya viongozi na wadau mbalimbali. limeibuliwa pia na viongozi na wadau mbalimbali.

Jaji mstaafu Joseph Warioba, akizungumza Agosti 28, 2026 katika mkutano wa wadau wa masuala ya demokrasia, alisema alimtafuta Nchimbi kwa simu baada ya kuona barua ya kujiuzulu ikisambaa mitandaoni. Nchimbi alipokea simu hiyo na kuthibitisha kuwa barua hiyo ilikuwa yake.

Hata hivyo, Warioba alisema alipompigia tena siku iliyofuata, simu haikupokelewa na ujumbe aliotuma haukujibiwa. Alisema hali hiyo ilikuwa tofauti na ilivyozoeleka kwake, kwani Nchimbi alikuwa akijibu simu na ujumbe wake.

Warioba pia alisema alisikia taarifa kwamba Nchimbi alikuwa amenyang’anywa simu, ingawa hakuthibitisha taarifa hiyo mwenyewe.
Katika mjadala uliofanyika katika ukumbi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), suala la alipo Nchimbi pia liliibuliwa na wadau mbalimbali.

Kadiri siku zilivyopita, taarifa na madai mbalimbali yalianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Baadhi zilidai kuwa Nchimbi ametekwa, nyingine zikidai kuwa anashikiliwa au yuko kizuizini. Hata hivyo, hadi sasa madai hayo hayajathibitishwa na chanzo huru au mamlaka husika.

Jina la Nchimbi pia lijitokeza katika mjadala wa TCD uliofanyika takribani wiki mbili zilizopita. Kwa sasa pia imeshuhudiwa Tundu Lissu Mwenyekiti wa Chadema Taifa anayekabiliwa kesi ya uhaini naye anawataka wadau kupaza sauti kujua alipo mwanasiasa huyo, swali lake naye ni "Nchimbi yuko wapi?"

Uvumi wa kifo
Wiki kadhaa baada ya kujiuzulu kwake, taarifa nyingine ilienea mitandaoni ikidai kuwa Nchimbi amefariki dunia.

Hata hivyo, taarifa hiyo ilikanushwa. Taarifa iliyodaiwa kutolewa na Jeshi la Polisi Tanzania kuhusu kifo chake ilibainika kuwa ya uzushi na haikuwa taarifa rasmi ya Jeshi hilo.

Tukio hilo limeongeza uzito wa swali lililokuwa tayari likijitokeza: Dkt. Nchimbi yuko wapi na yuko katika hali gani?

Swali linaendelea kukua
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo na Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, alitoa wito Septemba 10, 2026 kwa Dkt. Nchimbi, familia yake na vyombo husika kutoa ufafanuzi kuhusu usalama na hali yake. Ado alisema ukimya huo unaacha nafasi kwa minong’ono na madai mbalimbali kuendelea kusambaa.

Kwa upande mwingine, baadhi ya mijadala imehusisha kuondoka kwa Nchimbi na kauli zake za kisiasa, ikiwemo kauli kuhusu umuhimu wa kuwa na Katiba mpya. Nchimbi aliwahi kuzungumzia suala hilo hadharani kabla ya kujiuzulu kwake, jambo ambalo lilitajwa pia katika taarifa mbalimbali kuhusu mazingira yaliyozunguka kuondoka kwake.

Katika mijadala ya mitandaoni, zimeibuka pia tafsiri nyingine kuhusu sababu za kuondolewa kwake, zikiwemo madai kwamba aliondolewa kutokana na matarajio yake ya kisiasa kuelekea uchaguzi wa mwaka 2030 au kwa sababu za mabadiliko ndani ya uongozi wa Serikali.

Hata hivyo, madai hayo bado ni sehemu ya mijadala ya kisiasa na hayajathibitishwa kama sababu rasmi ya kuondoka kwake.

Soma Pia: Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Kinachojulikana rasmi ni kwamba Nchimbi alitangaza kujiuzulu na kustaafu siasa na utumishi wa umma, akisema alifanya hivyo baada ya kuridhika kuwa Rais alihitaji mabadiliko katika nafasi ya Makamu wa Rais. Serikali haikutoa sababu nyingine rasmi ya kujiuzulu kwake.

SERIKALI INA WAJIBU WA KUTOA UFAFANUZI?

Wakati madai mbalimbali yakiendelea kuenea, swali si tu kuhusu alipo Nchimbi, bali pia kuhusu nani mwenye wajibu wa kutoa taarifa sahihi kwa umma pale sintofahamu inapojitokeza kuhusu aliyewahi kushika nafasi ya juu katika uongozi wa nchi.

Serikali imekuwa ikisisitiza umuhimu wa kupambana na upotoshaji kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati. Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali pia inaeleza kuwa mojawapo ya majukumu yake ni kuweka mazingira ya utoaji wa taarifa sahihi na kwa wakati kwa umma.

Katika mazingira kama haya, ukimya unaweza kuacha nafasi kwa taarifa zisizothibitishwa kuendelea kusambaa.

Hata kama Dkt. Nchimbi ameamua kwa hiari yake kutokuwa hadharani baada ya kustaafu siasa na utumishi wa umma, bado swali la msingi kwa maslahi ya umma linaweza kuwa:

Je, yuko salama?
Na kama yuko salama, je, ni yeye mwenyewe, familia yake au mamlaka husika anayepaswa kutoa uthibitisho huo?

Swali hili linakuwa muhimu zaidi kutokana na nafasi ya juu aliyowahi kushika na wingi wa taarifa zinazokinzana zinazoendelea kusambaa. Kwa sasa, kinachobaki ni sintofahamu.

Dkt. Emmanuel John Nchimbi yuko wapi?
Na katika mazingira ambayo taarifa zisizothibitishwa zinaendelea kuibuka, nani wa kulijibu swali hilo kwa taarifa rasmi, ambazo ni sahihi?
 
Hii taarifa haijatolewa leo bahati mbaya. Kuna kitu kikubwa mno kinakuja
 
Hivi mwananchi hana haki kikatiba kupewa taarifa?
 
Mimi niko hapa kwa ajiri ya kujibu swi lako. Haya uliza sasa!
 
Back
Top Bottom