DOKEZO Mwezi wa pili sasa Mama amekosa Dawa ya Saratani (IV TRASTUZUMAB 440mg) Muhimbili Upanga

DOKEZO Mwezi wa pili sasa Mama amekosa Dawa ya Saratani (IV TRASTUZUMAB 440mg) Muhimbili Upanga

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mama yangu anaumwa Saratani anafanya clinic yake pale Muhimbili kila baada ya wiki 3 anachoma sindano zinazoitwa IV TRASTUZUMAB 440mg kwa kila baada ya wiki 3, hiyo dawa ukiwa na bima unachangia Shilingi 618,000 kila ukienda kuchoma bila bima ni Shilingi 1,230,000.

Sasa yapata mwezi na wiki 3 kila tukienda wanasema hizo dawa hazijaletwa, hazipo pharmacy na wagonjwa wanateseka, jamani tunaomba msaada kujua dawa zitakuja lini maana tumeshalipia na hawarudishi hela.

Kinachotuuma zaidi ni kuwa hata hicho kiasi kidogo cha fedha tunachotoa ni kwa kujichanga ndugu na jamaa, baadhi yao wakianza kusuasua, sasa kiasi kidogo tulichopata nacho tunazungushwa kupata huduma, hali ambayo si nzuri kwa mgonjwa wetu na wengine wote wanaotegemea huduma hiyo.

Majibu ya Muhimbili ~ Ufafanuzi kuhusu: Upatikanaji wa Dawa ya Trastuzumab kwa Wagonjwa wa Saratani
 
Mama yangu anaumwa saratani anafanya clinic yake pale Muhimbili kila baada ya wiki 3 anachoma sindano zinazoitwa IV TRASTUZUMAB 440mg kwa kila baada ya week 3, hiyo dawa ukiwa na bima unachangia laki 6 na 18 kila ukienda kuchoma bila bima ni 1,230,000tsh.

Sasa yapata mwezi na week 3 kila tukienda wanasema hizo dawa hazijaletwa, hazipo pharmacy na wagonjwa wanateseka jamani tunaomba msaada kujua dawa zitakuja lini maana tumeshalipia na hawarudishi hela.
Pole sana mkuu.

Tanzania kwa sasa watu wanaishi kwa mwendo wa "namjua nani pale". Yani ukifuata mfumo rasmi utapotea, inabidi uwe na mtu wako juu wakikuzingua unapiga simu moja tu dawa zinapatikana.

Hizo stories nimezisikia sana Muhimbili, matatizo yanatokea kama hivyo, mtu anampigia Dr. Janabi, mara moja yanaisha.

Sasa hivi watu wanaishi kwa kuwa na mtu wao kila sehemu nyeti. Mtu ana mtu polisi, ana mtu Muhimbili, ana mtu TRA, ana mtu ardhi, ana mtu mahakamani, kila sehemu ana mtu.

Sasa kama huna connection, hujui au huwezi rushwa, ndiyo inakuwa tabu.

Sitetei mfumo huu, nauelezea tu.
 
Pole sana mkuu.

Tanzania kwa sasa watu wanaishi kwa mwendo wa "namjua nani pale". Yani ukifuata mfumo rasmi utapotea, inabidi uwe na mtu wako juu wakikuzingua unapiga simu moja tu dawa zinapatikana.

Hizo stories ninezisikia sana Muhimbili, matatizo yanatokea kama hivyo, mtu anampigia Dr. Janabi, mara moja yanaisha.

Sasa hivi watu wanaishi kwa kuwa na mtu wao kila sehemu nyeti. Mtu ana mtu polisi, ana mtu Muhimbili, ana mtu TRA, ana mtu ardhi, ana mtu mahakamani, kila sehemu ana mtu.

Sasa kama huna connection, hujui au huwezi rushwa, ndiyo inakuwa tabu.

Sitetei mfumo huu, nauelezea tu.
Hakika na ndio ukweriiii wenyewe umemaliza Kila kitu
 
Hakika na ndio ukweriiii wenyewe umemaliza Kila kitu
Naam.

Nimekumbuka story inayo illustrate hili jambo. Kuna aunt yangu mmoja alikuwa nje miaka mingi, akawa karudi Tanzania.

Alivyorudi akawa anatafuta nyumba sehemu nzuri Dar.

Hakuuliza utaratibu wa kutafuta nyumba Dar ukoje, aliuliza tu pale NHC tunamjua nani?

It turns out alikuwa anamjua Mkurugenzi Mkuu.

Baada ya muda si mrefu tukawa tunaenda kwa aunt Masaki.

Sasa nilijiuliza sana, ukifuata mfumo utapata lini nyumba ya NHC Masaki?
 
Naam.

Nimekumbuka story inayo illustrate hili jambo. Kuna aunt yangu mmoja alikuwa nje miaka mingi, akawa karudi Tanzania.

Alivyorudi akawa anatafuta nyumba sehemu nzuri Dar.

Hakuuliza utaratibu wa kutafuta nyumba Dar ukoje, aliuliza tu pale NHC tunamjua nani?

It turns out alikuwa anamjua Mkurugenzi Mkuu.

Baada ya nuda si mrefu tukawa tunaenda kwa aunt Masaki.

Sasa nilijiuliza sana, ukifuata mfumo utapata lini nyumba ya NHC Masaki?
Huwezi pata.
Popote pale Tanzania bila KUMJUA au kujuana ni ngumu sana as well as pesaaa ndio vile kwenye uzia penyeza RUPIA
 
Tia hela maana haya malalamiko hakuna wa kukusaidia popote pale kwenye hii nchi
Tatizo halijafika kwako ndio maana unaandika ujinga.Nionavyo yeye kaandika kusudi na wengine wajue yanayotokea.'Who are you' ndio matokeo yake,watu wamegoma kuchangia sasa, mnafikiri mtaweza wenyewe bila mataif ya nje kuchangia.
 
UFAFANUZI KUHUSU: UPATIKANAJI WA DAWA YA TRASTUZUMAB KWA WAGONJWA WA SARATANI

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikieleza malalamiko ya mdau kuhusu ukosefu wa dawa ya Trastuzumab kwa ajili ya matibabu ya saratani.

Hospitali inapenda kuufahamisha umma na wadau wote kuwa dawa ya Trastuzumab zinapatikana hospitalini hapo, kwa viwango vyote vinavyohitajika kimatibabu 600mg, 440mg na 150mg. Kulikuwepo na changamoto ya 440 mg kwa muda mfupi kutokana na sababu ambazo hazikuweza kuzuilika lakini kwa sasa inapatikana.

Pia Hospitali ya Taifa Muhimbili ingependa kuwasisitiza wapata huduma wetu wote kufata taratibu za Hospitali za namna ya kupata majibu sahihi kwa changamoto zote wanazopitia wakati wa kupata matibabu, ili kuepuka kuwa na taarifa zisizo sahihi

Muhimbili inaendelea kuweka mkazo katika kuhakikisha upatikanaji wa dawa muhimu za matibabu ya saratani na magonjwa mengine, kwa lengo la kutoa huduma bora na za uhakika kwa wagonjwa wote.
 
Safi sana kwa majibu yaliyonyooka taasisi zingine ziige huu mfano
 
Pia Hospitali ya Taifa Muhimbili ingependa kuwasisitiza wapata huduma wetu wote kufata taratibu za Hospitali za namna ya kupata majibu sahihi kwa changamoto zote wanazopitia wakati wa kupata matibabu, ili kuepuka kuwa na taarifa zisizo sahihi.
Ni zipi hizo Taratibu?

Ni vyema kama mngeziainisha, pia mtoe taarifa kama wataalamu sio wanasiasa.
 
Back
Top Bottom