A
Pole sana mkuu.Mama yangu anaumwa saratani anafanya clinic yake pale Muhimbili kila baada ya wiki 3 anachoma sindano zinazoitwa IV TRASTUZUMAB 440mg kwa kila baada ya week 3, hiyo dawa ukiwa na bima unachangia laki 6 na 18 kila ukienda kuchoma bila bima ni 1,230,000tsh.
Sasa yapata mwezi na week 3 kila tukienda wanasema hizo dawa hazijaletwa, hazipo pharmacy na wagonjwa wanateseka jamani tunaomba msaada kujua dawa zitakuja lini maana tumeshalipia na hawarudishi hela.
Hakika na ndio ukweriiii wenyewe umemaliza Kila kituPole sana mkuu.
Tanzania kwa sasa watu wanaishi kwa mwendo wa "namjua nani pale". Yani ukifuata mfumo rasmi utapotea, inabidi uwe na mtu wako juu wakikuzingua unapiga simu moja tu dawa zinapatikana.
Hizo stories ninezisikia sana Muhimbili, matatizo yanatokea kama hivyo, mtu anampigia Dr. Janabi, mara moja yanaisha.
Sasa hivi watu wanaishi kwa kuwa na mtu wao kila sehemu nyeti. Mtu ana mtu polisi, ana mtu Muhimbili, ana mtu TRA, ana mtu ardhi, ana mtu mahakamani, kila sehemu ana mtu.
Sasa kama huna connection, hujui au huwezi rushwa, ndiyo inakuwa tabu.
Sitetei mfumo huu, nauelezea tu.
Naam.Hakika na ndio ukweriiii wenyewe umemaliza Kila kitu
Huwezi pata.Naam.
Nimekumbuka story inayo illustrate hili jambo. Kuna aunt yangu mmoja alikuwa nje miaka mingi, akawa karudi Tanzania.
Alivyorudi akawa anatafuta nyumba sehemu nzuri Dar.
Hakuuliza utaratibu wa kutafuta nyumba Dar ukoje, aliuliza tu pale NHC tunamjua nani?
It turns out alikuwa anamjua Mkurugenzi Mkuu.
Baada ya nuda si mrefu tukawa tunaenda kwa aunt Masaki.
Sasa nilijiuliza sana, ukifuata mfumo utapata lini nyumba ya NHC Masaki?
Tatizo halijafika kwako ndio maana unaandika ujinga.Nionavyo yeye kaandika kusudi na wengine wajue yanayotokea.'Who are you' ndio matokeo yake,watu wamegoma kuchangia sasa, mnafikiri mtaweza wenyewe bila mataif ya nje kuchangia.Tia hela maana haya malalamiko hakuna wa kukusaidia popote pale kwenye hii nchi
Safi sana kwa majibu yaliyonyooka taasisi zingine ziige huu mfanoUFAFANUZI KUHUSU: UPATIKANAJI WA DAWA YA TRASTUZUMAB KWA WAGONJWA WA SARATANI
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikieleza malalamiko ya mdau kuhusu ukosefu wa dawa ya Trastuzumab kwa ajili ya matibabu ya saratani.
Hospitali inapenda kuufahamisha umma na wadau wote kuwa dawa ya Trastuzumab zinapatikana hospitalini hapo, kwa viwango vyote vinavyohitajika kimatibabu 600mg, 440mg na 150mg. Kulikuwepo na changamoto ya 440 mg kwa muda mfupi kutokana na sababu ambazo hazikuweza kuzuilika lakini kwa sasa inapatikana.
Pia Hospitali ya Taifa Muhimbili ingependa kuwasisitiza wapata huduma wetu wote kufata taratibu za Hospitali za namna ya kupata majibu sahihi kwa changamoto zote wanazopitia wakati wa kupata matibabu, ili kuepuka kuwa na taarifa zisizo sahihi
Muhimbili inaendelea kuweka mkazo katika kuhakikisha upatikanaji wa dawa muhimu za matibabu ya saratani na magonjwa mengine, kwa lengo la kutoa huduma bora na za uhakika kwa wagonjwa wote.
Ni zipi hizo Taratibu?Pia Hospitali ya Taifa Muhimbili ingependa kuwasisitiza wapata huduma wetu wote kufata taratibu za Hospitali za namna ya kupata majibu sahihi kwa changamoto zote wanazopitia wakati wa kupata matibabu, ili kuepuka kuwa na taarifa zisizo sahihi.