Mwezi wa tatu huu vijana wa IT wanaojimwambafai kwa misamiati ya IT wameshindwa kuni hack kwa dau la laki 3, Maneno tu

Kwa Tanzania nafahamu watu wawili wanaoweza ku hack...vile vile ku sniff wakajua nani ame hack....lakini wamekula viapo...mmoja mfupi mweupe mtu wa Tanga....mwingine mweusi mchaga wa marangu alakula SM mpaka baadae.
 
Hivi suala la Hacking huwa mnalichukuliaje?? Ku hack sio lazima uwe IT Jamani, hili neno hacking limechafua sana fani ya IT Tanzania. Tukumbuke hata wale wazee wa ile pesa tuma kwa namba hii ni hackers pia wanatumia social engineering wanakusuka unatoa mpunga na unakuta huyo hata Computer hajawahi kuonana nayo.

Wakati mwingine unakuta labda mpo ofisi moja, kuna mfumo mnaoutumia katika shughuli fulani, ili kuingia kwenye huo mfumo kwa mara ya kwanza labda mnapewa default credential, (username = jinaLaKwanza.jinaLa Mwisho, password = 12345) ukiingia kwenye mfumo hiyo mara ya kwanza labda unakutana na prompt inakuomba ubadili password default uweke password zako at the same time una option ya kuignore kubadili password, kwa hulka ya uvivu wa watu kukariri password mtu anaamua ku ignore ku change password anaendelea na default password (kwa sababu ni rahisi kuzikumbuka), anatokea mwamba mmoja anajiongeza anaona kwa uvivu wetu wa kukariri password inawezekana kabisa asilimia 80 ya watu hapa ofisini hawajabadili password na kwakuwa mfumo haumbani mtu kubadili password anaamua kusema emu ngoja nijaribu ku login kama fulani kwa default credential, anatest mara paap ameingia kwenye mfumo kama fulani, huyu tayari ni Hacker, kupuuzia kwa mtu fulani kubadili password kumemuwezesha mtu mwingine aliyewaza hatua moja mbele zaidi kupata access na kuwa hacker. Hakuna Sql injection, packet sniffing, phising, walana nini ila tayari umekuwa hacked.
 
Kwa Tanzania nafahamu watu wawili wanaoweza ku hack...vile vile ku sniff wakajua nani ame hack....lakini wamekula viapo...mmoja mfupi mweupe mtu wa Tanga....mwingine mweusi mchaga wa marangu alakula SM mpaka baadae.
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Hicho kiapo walikula kabla au baada ya website ya TCU kuwekewa picha za pilau na script kiddies??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…