Bani Israel
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,775
- 3,593
Ndani ya CCM mpaka kufikia leo Majimbo ya Mwibara na Siha yanatazamiwa kuwa na kitimtim cha aina yake katika kile kinachotazamiwa kuwa wagombea walioomba ridhaa wote wanaeleweka huko juu.
MWIBARA mbuge wao ni Kangi Lugola na sasa hasimu na adui wake aliekuwa akitambulika kama mwanaharakati huru asiye na chama Cyprian Musiba kuchukua Fomu kuwania jimbo hilo hapa kwa upande wangu ni propaganda zimekutana.
SIHA nako ambako mbunge wake alikuwa ni Dkt. Mollel ambae alihama kutoka chama cha CHADEMA na kuhamia CCM kutangaziwa nia na Aliekuwa mkuu wa mkoa wa Tabora Mh. Mwanri.
Mwanri anaesifika kwa uongozi wake timamu wa kuchapa kazi hadi kukubalika na jamii kuchukua fomu jimbo la Siha imeonekana ni kama kumpoteza Dkt. Mollel.
Aidha wiki iliyoisha mh Rais alitoa angalizo kwamba wabunge waliounga juhudi wasisumbuliwe kupata upinzani ndani ya chama, swali la kujiuliza imekuwaje fomu ziwe zaidi ya moja? Imekuwaje fomu itolewe kwa mtu baki si angepita bila kupingwa?
Kama ikiachwa nguvu ya wanachama iamue basi inatazamiwa ndio mwisho wa Dr Mollel.
Hata Mhe. Rais naye sidhani kama anaweza mtema Agrey Mwanri mbele ya Mollel.