Mwigizaji Iniedo akiri kubebewa mimba na mwanamke mwingine

Mwigizaji Iniedo akiri kubebewa mimba na mwanamke mwingine

DeepPond

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2017
Posts
41,728
Reaction score
103,997
Mwigizaji nyota wa filamu za Nollywood nchini Nigeria, Iniedo amefunguka kwa mara ya kwanza yeye ni mzazi wa mtoto mmoja na alipata mtoto huyo kupitia kubebewa mimba na mwanamke mwingine, kisayansi njia hiyo inaitwa "Surrogacy".

Akizungumza kwenye mahojiano na kipindi cha Lilian’s Couch huko Nigeria kinacho ongozwa na mtangazaji Lilian Afegbai, Ini amesema kwamba aliamua kutumia njia hiyo ili kupata amani ya moyo wake kwani yeye ni mtu ambaye anapenda kukaa peke yake lakini aligundua kwamba kila akiamka asubuhi hajifikirii bali anafikiria mtu mwingine.

Pia amebainisha kwamba alikosolewa na wengi kwa kuamua kupata mtoto kwa njia ya kubebewa mimba ila amewaambia mashabiki kuwa yeye ndiye alitoa yai ambalo lilitumika kuunda mimba ya binti yake na hivyo wanafanana na ni mtoto wake.

“Niliamua kufuata njia hiyo (Surrogacy) ili na mimi nitimize amani ya moyo wangu pamoja na ndoto ya kuwa na familia” alisema @iniedo na kuongeza kwamba bado kuna mayai yake ambayo yamehifadhiwa ili kutumika ikiwa ataamua kubeba mimba mwenyewe au kubebewa na mtu mwingine.

Kuhusu baba wa binti yake huyo, Ini alisema kwamba alitafuta mbegu za mtu aliyejitolea kumpa ili asipate shida yoyote kimawazo siku za usoni. “Huwa ninashtuka kila mara nikiona mama na baba wakizozana hadharani kuhusu mtoto na ndiyo sababu nilitafuta mbegu tu.” alieleza Iniedo.

9ead29526ecd8a7a3f681dfe711eb6b2.jpg

 
H𝚊𝚙𝚘 𝚔𝚞𝚝𝚊𝚔𝚞𝚊 𝚑𝚊𝚔𝚞𝚗𝚊 𝚞𝚌𝚑𝚞𝚗𝚐𝚞 𝚠𝚊 𝚖𝚠𝚊𝚗𝚊 𝚊𝚞𝚓𝚞𝚊𝚢𝚎 𝚖𝚣𝚊𝚣𝚒
 
Wee nae, kwan kugegedwa na hiyo process inahusu nn? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wee gegedwa upate mtoto. Sasa unataka upate mtoto kirahisi rahisi tuu hutakuwa na uchungu nae
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] una shida wee baba wa mizagamuo khaaah.
Ndio ukweli lakini...unatakiwa ukiwa unamnyonyesha bby wako hapo ukimwamgalia unakumbuka jinsi hubby alikugaragaza mpaka kunyunyuzia mbegu kwa mbususu😜
 
Wakipima dna huyo mtoto anakua amebase kwa mtoa yai au mbeba mimba au wote??

Na mtoto hanyinyeshwi maziwa ya mama kama wataalamu wanavoshauri??
 
Hii akili ni ya hovyo kabisa,unajichukulia tu mbegu kwa mpuuzi mmoja,naye kwa kutokuelewa anakupa tu bila ya kujua kuwa unganiko la mbegu yake na yai lolote litaleta mtoto wake duniani ambaye atakuwa hana baba....
 
Back
Top Bottom