Mwigizaji wa Bongo Movies Esha Buheti Akiri Kuchepuka Nje ya Ndoa

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Mwigizaji Bongo, Esha Buheti, licha ya kuwa ndani ya ndoa, amekiri kuchepuka na mcheza mpira mmoja ambaye hakutaka kuweka wazi jina lake.

Akizungumza na na gazeti la Ijumaa, Esha aliweka wazi hisia zake kuwa kwa sasa ana kifaa kipya chenye hadhi na amekuwa akitupia picha zake mitandaoni kisha anazitoa.

“Najua wambeya watataka kumchunguza mpenzi wangu wa sasa ndiyo maana namuweka mtandaoni kisha nafuta harakaharaka,” alisema Esha.

Esha alifunguka kuwa, pamoja na ‘kidumu’ alichonacho bado yuko kwenye ndoa yake na anamheshimu mumewe aliyezaa naye mtoto mmoja.
 
wanaume wakiwa na michepuko ni sawa lakini upande wa pili ni vibaya, hahaa
 
Mh anasema kabisa yumo ndani ya ndoa na anachepuka nahis nati zitakua zimelegea kichwani mwake
 
Eeh kuna watu utoto unawasumbua " eti namuweka mtandaoni kisha nafuta haraka haraka". Kwani umeombwa umuweke au kisebengo chako? Hawa ndo wanaofanya wanawake wa bongo movies wote waonekane hawajitambui
 
Wakati mwingine huwa nadhani kuwa kama wanandoa wana VVU hawaoni shida hata mmoja kati yao akitoka nje ya ndoa, ila sijui kwa huyo muigizaji.
 
Hapa mume atakuwa ni boya tu! Mwanamme makini akiona post kama hii anazimia kwanza, akiamka balaa ni la kutuliza kwa bulldozer!
 
Money Stunna

Huyu anafahamu maana ya kuheshimu mumewe na ndoa?gonjwa hili jike eh?
 
Last edited by a moderator:
Kabla hujaoa msanii unapaswa kupima kwanza kama BP ziko sawa na zinaweza kuhimili mishtuko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…