Mwigulu akagua Mradi wa Hospitali ya Wilaya ya Bunda

Mwigulu akagua Mradi wa Hospitali ya Wilaya ya Bunda

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
๐——๐—ž๐—ง. ๐— ๐—ช๐—œ๐—š๐—จ๐—Ÿ๐—จ ๐—”๐—ž๐—”๐—š๐—จ๐—” ๐— ๐—ฅ๐—”๐——๐—œ ๐—ช๐—” ๐—›๐—ข๐—ฆ๐—ฃ๐—œ๐—ง๐—”๐—Ÿ๐—œ ๐—ฌ๐—” ๐—ช๐—œ๐—Ÿ๐—”๐—ฌ๐—” ๐—ฌ๐—” ๐—•๐—จ๐—ก๐——๐—”

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Oktoba 03, 2026 amekagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara ambapo mpaka sasa kiasi cha shilingi bilioni 5.3 kimeshatolewa hadi sasa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo.

Akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo, Dkt. Mwigulu amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua kazi kubwa inayofanywa na watumishi katika sekta ya afya kwenye kuwahudumia Watanzania.

Aidha, Dkt. Mwigulu amesema kuwa Serikali itaendelea kuweka mkazo katika kuboresha mazingira ya huduma za afya.

โ€œLakini pia tutaendelea kuboresha na kuhakikisha kwamba watumishi hawakwamishwi na vitendea kazi wala mazingira ya kazi katika uhudumiaji katika sekta hiyo ya afyaโ€.

Lengo kuu la mradi huo ni kutoa huduma za ngazi ya Hospitali ambazo hazikua zikipatikana maeneo haya na wananchi walilazimika kuzifuata mbali kama Bunda Mjini au Mugumu-Serengeti .

IMG-20261003-WA0092.jpg
IMG-20261003-WA0102.jpg
IMG-20261003-WA0104.jpg
IMG-20261003-WA0100.jpg
IMG-20261003-WA0096.jpg
IMG-20261003-WA0094.jpg
IMG-20261003-WA0098.jpg
IMG-20261003-WA0090.jpg
IMG-20261003-WA0088.jpg
IMG-20261003-WA0086.jpg
IMG-20261003-WA0084.jpg
 
 
Back
Top Bottom