Mwigulu amenilazimu niweke mafuta ya elfu 10,000 kwenye pikipiki ili nipeleke Tsh 2,000,000 Kijiji jirani

gimmy's

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2011
Posts
3,312
Reaction score
3,345
Nawasalimu wanajamvi wote hapa javini,

Kwanza naomba nianze kwa kunukuu maneno ya waziri wa fedha Mr Mwigulu alietuambia watanzania kwamba,"kama mtu anataka kuhamia Burundi kwasababu ya tozo kwenye miamala na ahame".

Ndugu zangu leo nimelazimika kupoteza muda wangu ili mradi tu nikwepe kulipa kodi ya dhuluma iliowekwa na serikali kwenye miamala ya simu ili kuumiza wananchi.

Japo najua Mr mwigulu hakuniona ili aone kwamba sitahama nchi kwenda Burundi lakini najipa moyo hata kama sio direct lakini ujumbe utafika na nimesusia kulipa hii kodi ya dhuluma,haiwezekani na haitawezekana kwa mtanzania wa kawaida kulipa pesa nyingi kiasi hiki,

Mr Mwigulu wewe baki na kiburi chako na sisi tuache na umasikini wetu,

Ninyi wanasiasa mnatuambia sisi tulipe kodi zenye kuumiza wakati ninyi kuanzia spika,raisi,waziri mkuu,wabunge,majaji wote hamlipi kodi.

Mnatuhamasisha tulipe hizi tozo ili mjenge barabara halafu kesho wabunge wanakuja kutafutia kura barabara tulizojenga wenyewe kwa tozo za kuumiza ilihali wabunge hawalipi kodi kabisa.

Nataka ujumbe huu ufike kwa mama mh Samia, kama kweli aliwapima mawaziri wake urefu wa mabega kama alivyosema pindi anawaapisha,basi ampime Mr mwigulu leo aone namna mabega yake yalivyo panda juu.
Asante.
 
Write your reply...mafuta ya teni kwa pikipiku ni umbali Wa misungwi kwenda nyegezi, nenda rudi.
 
Sasa hivi nimetoka kisesa kumpelekea dogo hela ya matumizi elfu 50 nimepiga mahesabu ya makato nkaona nipande gari niende nikamuone na kumuona kabisa nauli nimetumia buku,wakati juzi tu kabla miamala haijapanda nilkuwa natuma m pesa,
 
Mi ninachoamini hata yeye mwigulu anaipuka tozo hii sema anataka kutuekeleza tu si hatujui pa kutokea.
 
Huu utaratibu ni wa nchi nzima ukitaka kujua hilo waulize watoa huduma za kimtandao watakwambia wanapata wateja wangapi kwa siku toka tozo mpya zianze, binafsi nilitaka mtu anirushie hela lkn nikaona bora nimwelekeze benki
 
Nawasalimu wanajamvi wote hapa javini,
Kwanza naomba nianze kwa kunukuu maneno ya waziri wa fedha Mr Mwigulu alietuambia watanzania kwamba,"kama mtu anataka kuhamia Burundi kwasababu ya tozo kwenye miamala na ahame".

Ndugu zangu leo nimelazimika kupoteza muda wangu ili mradi tu nikwepe kulipa kodi ya dhuluma iliowekwa na serikali kwenye miamala ya simu ili kuumiza wananchi.

Japo najua Mr mwigulu hakuniona ili aone kwamba sitahama nchi kwenda Burundi lakini najipa moyo hata kama sio direct lakini ujumbe utafika na nimesusia kulipa hii kodi ya dhuluma,haiwezekani na haitawezekana kwa mtanzania wa kawaida kulipa pesa nyingi kiasi hiki,

Mr Mwigulu wewe baki na kiburi chako na sisi tuache na umasikini wetu,

Ninyi wanasiasa mnatuambia sisi tulipe kodi zenye kuumiza wakati ninyi kuanzia spika,raisi,waziri mkuu,wabunge,majaji wote hamlipi kodi.

Mnatuhamasisha tulipe hizi tozo ili mjenge barabara halafu kesho wabunge wanakuja kutafutia kura barabara tulizojenga wenyewe kwa tozo za kuumiza ilihali wabunge hawalipi kodi kabisa.

Nataka ujumbe huu ufike kwa mama mh Samia, kama kweli aliwapima mawaziri wake urefu wa mabega kama alivyosema pindi anawaapisha,basi ampime Mr mwigulu leo aone namna mabega yake yalivyo panda juu.
Asante.
Mkuu kama ubber inafika siku ingine unachukua ubber, gharama yake ni ndogo kuliko makato ya mwingulu
 
Penye uzia penyeza rupia.

Sasa hivi kuna Bank wameanza kutuma jumbe za kuhimiza matumizi ya huduma zao na wanahimiza kuwa hazin makato.

Bank wanazitamani sana hizi huduma,na hali ikibaki hivi mitandao chali.
 
Hizi tozo kwenye miamala zimeleta faida pia.

Maana watu sasa huonana na kuzungumza ana kwa ana.

Hakuna jambo lisilo na wema.

Zamani tulimazana kwenye miamala tu. Hizi 50,laki unione ili iweje.
 
Ila kodi ya kwenye mafuta umelipa!!! Asante.
Hoja ya msingi kwa
Penye uzia penyeza rupia.

Sasa hivi kuna Bank wameanza kutuma jumbe za kuhimiza matumizi ya huduma zao na wanahimiza kuwa hazin makato.

Bank wanazitamani sana hizi huduma,na hali ikibaki hivi mitandao chali.
Akili za mwigulu,mitandao ikifanya Vibaya watapoteza ajira kiasi gani?
 
Back
Top Bottom