Copy and paste kutoka uzi kama huu Mwigulu anasema,
Ndg wana jf.
Salaam. Naandika kujibu uzushi wenye malengo ya kuchafuana kisiasa na usiozingatia maadili ya uongozi kwenye uzi wenye kichwa cha habari hapo juu.
Kwanza maelezo yanasema nimemtuma RC Kone akazime maazimio ya madiwani yenye lengo la kumwondoa DED. Hii sio kweli, madiwani katika kikao chao bila uwepo wangu walikubaliana kumwita RC na walimtuma Mwenyekiti wa Halmashauri Just Makala akiwa na madiwani wakiwa watatu mpaka Singida wala sio kwa simu kwenda kumwomba aende Iramba kukutana nao. Wala sio mbunge aliyemtuma RC kwenda Iramba kukutana na madiwani. Walimpomkuta RC ndipo wakapanga kikao hicho tangu jtatu kuwa wakutane ijumaa yaani leo.
Pili, madiwani walimwomba RAS kupitia kikao chao cha ijumaa aende Iramba jumapili kabla ya RC. Wala hakuwa mbunge aliyeomba RAS na RC akazime maazimio.
Tatu, mimi sina record ya kubeba wahalifu na wala sijamtisha Diwani hata mmoja.
Ninachowambia madiwani nawambia na wana jf na watanzania, mimi ni kiongozi wa kitaifa nashiriki vipi kumhamisha mtu aliyeiba? Yaani ni wilaya ipi anakofaa mtu aliyeiba? Mimi kiongozi wa Kitaifa kwanini niwapelekee wilaya mwingine mtu ambaye ni mwizi? Nawambia madiwani wangu tuweke tuhuma hadharani na ushahidi hadharani ili ikothibitika ameiba afukuzwe sio azimio la kumhamisha. Hii kuhamisha ndio inayosababisha wizi nchi nzima cos wezi wanaiba eneo wanaacha legacy wanahamia eneo lingine kwenda kusuka kikosi cha wezi na baadae wanaiba wana hama tena mwisho nchi nzima kunakwepo mtandao wa wezi. Kamahuku ni kulinda wezi basi nadhani aliyeandika hanijui vizuri yeye antumwa tu akidhani hiyo inanichafua. Msimamo wangu sio kuazimia kuhamisha mwizi bali asomewe tuhuma ushahidi utolewe ikithibitika afukuzwe.
Ndg wana jf ukimhamisha mwizi akaendelea kuwa mtumishi ataanza kutumia kodi za umma, gari la umma, mafuta na posho fedha za walipakodi kuja Iramba kujibu. Tuachane na fikra za kizamani kuwaza kuhamisha mhalifu na mwizi bali hatua zichukuliwe palepale alipoiba
Says
Mwigulu Nchemba