Mwigulu ataruhusu nyota ya January ing'ae?

Mwigulu ataruhusu nyota ya January ing'ae?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
January ana mipango mingi inayohitaji fedha, lakini mmiliki wa fedha Ni asimu wake ambaye ni Mwigulu Nchemba, pesa ikichelewa kuidhinishwa miradi inachelewa na miradi isipopitishwa hazina na wizarani just kwa technicalities Januari anafeli.

Kimuundo hizi Ni wizara mbili zinazojitegemea ambazo zinaripoti utendaji kazi wake kwa Rais. Endapo Januari akiona mambo yanakwama hazina itamlazimu amjulishe Mwenye nchi na akimjulisha inakuwa amezalisha mgogoro hata Kama watabaki kusalimiana au kuchekeana lakini moyoni watakuwa na lao Jambo.

Lakini upande wa pili Januari akiwa na malengo makubwa zaidi ya kiasi Cha fedha kilichopo upo uwezekano akakwama. Mfano awamu iliyopita miundombinu ilielekezewa fedha nyingi na hivyo miradi ya baadhi wizara kukwama.

Naandika haya nikiwakumbusha wananzengo kwamba hapa upo mgogoro usioonekana kwa macho Ila upo rohoni. January anatamani kufanya extra na akifanya extra Mama anapata sifa kwa sababu miradi ya Januari Ina athari kubwa kiuchumi na kijaamii, ili afanye extra lazima hazina watoe extra kumwezesha kufikia malengo, na hazina wakimpa extra means Waziri lazima alazimike kumega sehemu ambako kumega huko kunaweza kuwa na athari wizara nyingine au kukahitaji signature ya Mama.

Itakapohitajika signature ya Mama na kwa kuzingatia malengo ya wawili hawa kisiasa lazima pachimbike.Kumbuka wizara ya fedha haina impact kwenye jamii kwa maono ya nje maana hakuna mradi wanaosimamia.

Hapa ndipo unaboini mgawa fedha anatakiwa awe mtu asiye na malengo ya Urais au Mwenye roho ya bifu. Mgawa fedha anapaswa awe mtu neutral ikiwezekana anayepokea shkamoo kutoka kwa wanasiasa wenye tamaa ya Urais.

Tunataka kwenda mbele lakini hatutaki kusoma alama za nyakati, tunataka kwenda mbele tukiwa na safu inayotaka ionekane ndiyo ilitufikisha huko wakati principally Tulipaswa kwenda Kama timu. Tenzi fikirisha kutokea Kanyigo Bukoba
 
Mwigulu hawezi kumfikia January hata siku moja japo wote ni wale wale fisiemu lakini January is far better than Mwigulu.

Mimi namdharau Nchemba sana kutokana na majibu yake na hata mijadala yake
 
Hujaelewa soma tena
nimeelewa, Mwigulu na January hawawezi kuelewana yani ni kama tuseme ni washindani na above all wote wana nia ya kuwania kile kiti
nikatoa jibu langu kwamba,hata kama Mwigulu akimbania January bado haitamsaidia maana Mwigulu hakubaliki kabisa
 
Kwa mfano January kafanya nini toka ulipomjua? Au we ndio wale wa mahaba?
ukisoma comment yangu utapata jibu la swali lako Boss, nimesema kabisa wote ni Hovyo yani hakuna kitu lakini nikasema bora January huwa anaongea kidogo vitu vya maana na hiko ndicho kinambeba unapomlinganisha na Mwigulu
kwangu mimi "sisiemu" hakuna kiongozi ila kuna viongozi nafuu
 
MWIGULU Mchemba ni MAFIA, Kitila Mkumbo anajua, mpaka akaacha kugombea Iramba 2020 baada ya Mwigulu kujiita " Mamba"
Na wanagroup la WhatsApp la Watanzania kumuonya sana asithubutu kugombea IRAMBA.

Kifupi Mwigulu atamfanyia tu MAGUMASHI sabotage MAKAMBA!!....

"TIME IS GOOD TEACHER "
 
Nimekuelewa..ila pengine ni kipi hicho cha maana alichosema January pengine itanipa hamasa.
 
Huyo January ni mafia pia. Alihakikisha anampoteza kabisa william shelukindo jimbo la bumbuli akalichukua yeye.
 
Nimekuelewa..ila pengine ni kipi hicho cha maana alichosema January pengine itanipa hamasa.
nimesema ki ujumla tu Mkuu,hakuna kitu specific, yani hata ukiingia Google au humu u aearch hao viongozi wawili utakuta kwamba wote ni hovyo lakini kuna bora
hivo basi nimesemea ki ujumla na hakuna jambo lolote specific
 
Mwigulu hawezi kumfikia January hata siku moja japo wote ni wale wale fisiemu lakini January is far better than Mwigulu
mimi namdharau Nchemba sana kutokana na majibu yake na hata mijadala yake
Bora mwigulu Mara 1000 kuliko huyo January. Yeye January hata hiyo mijadala haitaki. Nilimkosoa kidogo tu wiki iliyopita akanipiga ban.
January popote ulipo hutakuja kuupata uraisi
20211030_173404.jpg
 
Vyovyote iwavyo..Nia ya wananchi ni kuingiza wapinzani wengi kwenye chombo cha maamuzi ili kuweza kuequestion government! Kwa ilivosasa si muhimu kusema nani mzr why, just bcoz kipimio ni upinzani imara .Sasa je wote wakiwa kwenye wizara Chombo cha kupima na kuchallenge ubora utendaji wao kipo? Hakna bora hapo!!
 
Bora mwigulu Mara 1000 kuliko huyo January. Yeye January hata hiyo mijadala haitaki. Nilimkosoa kidogo tu wiki iliyopita akanipiga ban.
January popote ulipo hutakuja kuupata uraisi
View attachment 2000551
🤣viongozi wetu hawa ni tabu, Mwigulu nae aliwahi kupewa za uso ila anavumilia tu humu
 
Ufanisi wa serikali utatoka wapi kama mawaziri wanaanza kufanya kazi kwa malengo yao tofauti na yale waliyopewa na mteule wao, anataka afanye hivi ili aonekane na bosi anafaa zaidi siku ya mwisho akumbukwe kwenye ufalme wake.

Hangaya yupo ikulu lakini nae anafikiria 2025, Mwigulu na January nao hivyo hivyo, kwa sasa wako kwenye competition ya chini chini huku machoni wakijidai wanawatumikia watanzania, huu upuuzi unawaondolea imani kwa watanzania.
 
Bora mwigulu Mara 1000 kuliko huyo January. Yeye January hata hiyo mijadala haitaki. Nilimkosoa kidogo tu wiki iliyopita akanipiga ban.
January popote ulipo hutakuja kuupata uraisi
View attachment 2000551
Tatizo anawazia urais. Sasa kama kakupiga block maana yake angekuwa na mamlaka makubwa angekushughulikia ama kimya kimya au kwa namna yeyote ile.
 
Back
Top Bottom