Mwigulu kwenye hili la kuudanganya umma ni lazima uwajibike

Mwigulu kwenye hili la kuudanganya umma ni lazima uwajibike

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
Kwa muda Mrefu Waziri Mwigulu Nchemba amekuwa akitoa kauli tata ambazo humlazimu Mh Rais kutoka hadharani na kuzitolea ufafanuzi kwenye hili Mwigulu inakupasa kuwajibika
1671619180707.jpeg
 
Covax mchango wako please.
Huyu pia tupo wote kwenye utopian world where we believe leaders should be responsible for their actions.
 
Lini na wapi ukaona kiongozi wa kiafrika akiwajibika either kwa maneno yake au matendo yake? Sisi viongozi wetu ni miungu watu, the only time they'd bow down is during election campaigns when they really need our votes.
 
Mimi si mshabiki wa Samia, si mshabiki wa Mwigulu, si mshabiki wa CCM, ni mshabiki wa ukweli na technical detail driven conversations.

Samia, Mwigulu na CCM wana makosa mengi sana, kwa hiyo siko hapa kuwatetea. Niko hapa kuhoji "gotcha politics" na simplistic jingoistic headlines.

Sasa, hebu tuangalie hili suala la "kukopa sana" likoje.

Tuanze na definitions.

Definition ya kukopa sana ni nini?

Kipimo gani kinatumika? Debt to GDP ratio? Return on Investment Projection? Uwezo wa kulipa deni?

Katika vipimo hivyo, threshold gani inatumika?

"Kukopa sana" ni dhana ndefu, inayoweza kumaanisha vitu tofauti kutokana na muktadha uliotumika. Kukopa sana kwa kuangalia Debt to GDP ratio kunaweza kuwa si sawa na kukopa sana kwa kuangalia mambo kisiasa na uwezo wa kulipa deni. Inawezekana mtu akawa hajakopa sana kwa Debt to GDP ratio, lakini akawa kakopa sana kwa sababu hawezi kulipa deni.

So, haiwezekani Waziri Mwigulu Nchemba na Rais Samia Suluhu Hassan wote wakawa sawa katika hili, na watu wanaoangalia deni la taifa kwa simplistic eyes wao ndio wakawa wanakosea kwa kutegemea suala hili liwe na jibu moja tu?

Mwigulu hawezi kusema kwamba hatujakopa sana kwa kuangalia Debt to GDP ratio, na akawa sawa .Kwa kipimo hicho bado hatujakopa sana, tupo just over 37%,hata kwa kulinganisha na jirani zetu tu, Mozambique 109%, Malawi 62%, Zambia 59%, Kenya 57%, seuze mataifa makubwa kama Marekani yaliyokopa zaidi ya 107% ya GDP, Japan wamekopa zaidi ya 237% ya GDP yao, cheki link hapo chini.

Na pia, haiwezekani rais akasema tumekopa sana, kwa kuangalia uwezo wa kulipa deni, hususan kwa kuangalia riba, na yeye akawa sawa pia?

Tunapoangalia haya maneno, je, tunaangalia muktadha mkubwa wa maelezo? Au tunataka kuangalia maneno mawili matatu tu?

Tunajadili vipi masuala ya deni la taifa bila namba na mlinganyo wa kuangalia nchi nyingine?

Which "utopian world" are you referring to?

Do not confuse "Tanzanian world" with any other world"!
Am not in utopian world the member I quoted knows perfectly well what I meant, excuse me
 
Rais Samia huwa anawapa wakati mgumu Mawaziri Wake
Sasa wewe waziri anasema mikopo tunayokopa haiwahusu wananchi na hakuna mwananchi atakayegongewa mlango kulipa hiyo mikopo halafu kesho yake boss wake anasema tunalipa mikopo ya nje ambayo tulikopa hapo awali kwahiyo tuvumilieni kwanza, bodo unasema Rais anawapa wakati mugumu mawaziri wake.
 
Sina hakika Kama Mwigulu atapona awamu hii ya Baraza la Mawaziri japo ana nafsi kubwa ya kupona maana Mara nyingi Wizara ya Fedha na Mambo ya nje huwa hazibadilishwi Mawaziri Mara kwa Mara
 
Sina hakika Kama Mwigulu atapona awamu hii ya Baraza la Mawaziri japo ana nafsi kubwa ya kupona maana Mara nyingi Wizara ya Fedha na Mambo ya nje huwa hazibadilishwi Mawaziri Mara kwa Mara
Mmeshapata mkojani mnataka kumchinjia madelu baharini, siyo?
 
Huyu alituambia GSM, Bakhresa au jamiiforums wakikopa Standard Charted au Bank of America hilo linahesabika ni deni la Taifa, muongo mkubwa huyu hajui anachoongea
 
Kwa muda Mrefu Waziri Mwigulu Nchemba amekuwa akitoa kauli tata ambazo humlazimu Mh Rais kutoka hadharani na kuzitolea ufafanuzi kwenye hili Mwigulu inakupasa kuwajibika
View attachment 2453655
🤣🤣🤣yaani mwigulu naona nyakati zinamkataa kabisa.

Kila anachofanya hata kama ni kwa usahihi anajikuta kakosea
 
Kwa muda Mrefu Waziri Mwigulu Nchemba amekuwa akitoa kauli tata ambazo humlazimu Mh Rais kutoka hadharani na kuzitolea ufafanuzi kwenye hili Mwigulu inakupasa kuwajibika
View attachment 2453655
HAKUNA WA KUMWAJIBISHA MWIGULU HUYO NI CHUMA CHA PUA MWIGULU FOR PRESIDENT 2025 MAWE YAKE NIMEPEWA TENDA YA KUREKEBISHA MWAKA KUTOKA 2015 KUWA 2025
 
HAKUNA WA KUMWAJIBISHA MWIGULU HUYO NI CHUMA CHA PUA MWIGULU FOR PRESIDENT 2025 MAWE YAKE NIMEPEWA TENDA YA KUREKEBISHA MWAKA KUTOKA 2015 KUWA 2025
Endelea kuota.Uzuri wa ndoto kama hizi unazoota hazina gharama nyingi.Ni usingizi tu na godoro la Tanfoam.
 
Back
Top Bottom