Mimi si mshabiki wa Samia, si mshabiki wa Mwigulu, si mshabiki wa CCM, ni mshabiki wa ukweli na technical detail driven conversations.
Samia, Mwigulu na CCM wana makosa mengi sana, kwa hiyo siko hapa kuwatetea. Niko hapa kuhoji "gotcha politics" na simplistic jingoistic headlines.
Sasa, hebu tuangalie hili suala la "kukopa sana" likoje.
Tuanze na definitions.
Definition ya kukopa sana ni nini?
Kipimo gani kinatumika? Debt to GDP ratio? Return on Investment Projection? Uwezo wa kulipa deni?
Katika vipimo hivyo, threshold gani inatumika?
"Kukopa sana" ni dhana ndefu, inayoweza kumaanisha vitu tofauti kutokana na muktadha uliotumika. Kukopa sana kwa kuangalia Debt to GDP ratio kunaweza kuwa si sawa na kukopa sana kwa kuangalia mambo kisiasa na uwezo wa kulipa deni. Inawezekana mtu akawa hajakopa sana kwa Debt to GDP ratio, lakini akawa kakopa sana kwa sababu hawezi kulipa deni.
So, haiwezekani Waziri Mwigulu Nchemba na Rais Samia Suluhu Hassan wote wakawa sawa katika hili, na watu wanaoangalia deni la taifa kwa simplistic eyes wao ndio wakawa wanakosea kwa kutegemea suala hili liwe na jibu moja tu?
Mwigulu hawezi kusema kwamba hatujakopa sana kwa kuangalia Debt to GDP ratio, na akawa sawa .Kwa kipimo hicho bado hatujakopa sana, tupo just over 37%,hata kwa kulinganisha na jirani zetu tu, Mozambique 109%, Malawi 62%, Zambia 59%, Kenya 57%, seuze mataifa makubwa kama Marekani yaliyokopa zaidi ya 107% ya GDP, Japan wamekopa zaidi ya 237% ya GDP yao, cheki link hapo chini.
Na pia, haiwezekani rais akasema tumekopa sana, kwa kuangalia uwezo wa kulipa deni, hususan kwa kuangalia riba, na yeye akawa sawa pia?
Tunapoangalia haya maneno, je, tunaangalia muktadha mkubwa wa maelezo? Au tunataka kuangalia maneno mawili matatu tu?
Tunajadili vipi masuala ya deni la taifa bila namba na mlinganyo wa kuangalia nchi nyingine?
worldpopulationreview.com