Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa!

he deserve to be a next president! tatizo nchii hii uswahili mwingi sana hatapita NEC
 
Mwigulu amebeba dhamira ya kweli tatizo ni mfumo uliopo ndani ya chama chake ataweza kuufuta.

Chama kipi kisicho na mfumo wa kufumuliwa?Mwigulu ana ambitions na energy ya kuyafanya hayo.

Kumbuka vyama vyote vina mifumo ya umiliki wa watu fulani, inahitajika mtu mpya kuufumua.
 
Amekuwa gumzo kutokana na mabango aliyojiandika nchi nzima nadhani.
Tanzania will be lead by one President EL
 
Tatizo hapo sio mtu. Tatizo ukiwa ndani ya CCM ni kansa tayari. Kazi kubwa iliyopo ni kuitoa CCM madarakani. CCM ni system ambayo IMEOZA. Lazima system hiyo iondolewe kwanza. Gari likiwa na MATAIRI MABOVU, hata kama una DEREVA mzuri toka NIT, Haizuii kupata pancha njiani. Ondoa kwanza TAIRI hizo mbovu, weka mpya.Gari litafika mbali bila pancha!!!


 
Mtoa mada umeainisha kuwa gumzo hilo limechanganya wale wanaomkosoa na wale wanaomuunga mkono . How comes uulize juu ya ishara? Tupe uwiano wa hao wanaomkosoa na wanaomuunga mkono tuweze kukupa mtazamo wetu. Otherwise na hii mada yako inaongezea tu idadi ya mada zinazomzungumzia Mwigulu na sio tathmin
 
hivi 1961 nyerere alikuwa na umri gani?
Red Giant latu huwezimlinganisha Nyererr na Mwigulu.... uthubutu wao ni tofauti kabisa. Nyerere aliyethubutu kuwaface wakoloni na masilaha yao... na huyu ambaye hata kutamka atawashughulikiaje watuhumiwa wa Escrow, EPA na mafisadi wengine ndani ya chama chake ameshindwa ndio tumlinganishe na Nyerere wa wakati ule?
 
Last edited by a moderator:
ati maisha bora kwa kila mtanzania mh!! ilitakiwa iwekwe wazi maisha bora kila fisadi full stop.
subirini butwaa DR HUSSEIN MWINYI ndio atakayemrithi jk.
 
mimi nadhani Mwigulu hakujua kama atakuja kumbea urais hadi alipojiona ni maarufu ghafla,

1. angejua asingekuwa anaropoka au kutoa kauli chafu tena kana kwamba sio msomi.
mfano ccm ni ng'ombe wananchi ni ndama. mkikataa kutujagua udiwani mtakufa maana tutagoma kuwanyonyesha. Ni kazi ya srikali kumuudumia kila mwananchi bila kujali dini wala itikadi. ulitereza hapo mkuu.

2. Kama raia mwema kudai kuwa anaushahidi wa ugaidi huku akishindwa kuupeleka polisi, tena hata polisi kumuhoji ni udhaifu na kutafuta umaarufu mwepesi wa kisiasa.

3. kama Mwanasiasa mzarendo hakupaswa kuongea yale ambayo huwa anayapinga kisa kutetea ccm hashindwi kutetea mafisadi akiwa rais. Kigeugeu.

4. Herikopta ya msukuma ndio aliitumia kujitafutia umaarufu kule moro, wakati huohuo huyo jamaa ni mfuasi mkubwa wa EL. inanipa picha kuwa kuna uwezekano hawa lao ni moja.

5. Bingwa wa siasa chafu, Kutembea na Mtu aliyemwagiwa tindikali ili kuwatisha wananchi ubaya wa wapinzani wakati alipaswa kuwaeleza nini SERA zake na atatekeleza vipi.

6. Kama ukiwa na elimu ya Masters ulishindwa kubuni njia ya kisomi ya kujipatia Kipato (labda kama ulisoma elimu mbaya) ukaenda kubeba zege, nilitegemea labda ufanye kazi ya kuandika proporsals, projects, au hata kutafuta nafasi ya kufundisha ktk mamia ya shule hapo jijini,. utawezaje kubuni miradi au mawazo ya kuondoa umasikini kwa graduates hususani kipindi ambacho hata kupata internship ni kazi.(msoni ni yule anayetumia elimu yake kujikwamua kimaisha kwa mtazamo wangu mimi ambaye sijaenda shule)

7. Siku moja ukiwa umejaa jazba bungeni ulitamani kupata japo nafasi ya urais ili uwashughulikie wapinzani na watu waliokuwa na mawazo tofauti na yako. Hadi ukasiema usingekuwa waziri ungeongea maneno mabaya zaidi(jinsi nilivyokuelewa). Sasa ilinitisha kidogo kwa jaribu dogo tu lilikutoa kwenye mstari, je ukikabidhiwa nchi?? You need time to convince people that you are new Mwigulu.

Maoni yangu: Mwigulu wa leo sio kama wa miaka iliyopita. Unaonekana unakuja kama mkombozi lakni inabidi upate muda tujiridhishe vizuri kama kweli umebadilika au unatumia sifa mbaya ya USAHAULIFU wa wachache kutimiza malengo yako kisiasa.

yote kwa yoe, Nakupongeza kwa kutangaza lakini fanya marekebisho, kama unafaa siku ikifika utakuwa.
 
kuna theory ya history make the man. inasema mwigulu angekuwepo 1961 angepambana na wakooloni na Nyerere angekuwepo leo asingeweza pambana na mafisadi.
unajua sasa anatafuta kupita kura za maoni akianza kuwachokonoa EPA na ESCROW ataharibu kila kitu. mafisadi wata retaliate. mi nafikiri kuongoza na umri ni vitu tofauti. watu wenye uzoeefu kwenye serikali na umri mkubwa ndiyo wametufikisha hapa.
 
Kuajiliwa BoT sio kazi ndogo. Ukishapewa offer sio cgini ya miezi mitatu kumaliza process including vetting. Kama huna pesa utaishije miezi yote hiyo kama hujabeba zege. Tafuteni uongo wa kweli sio huo.
 
Mwigulu ni opportunistic populist tu.
I am glad someone else could see through Mwigulu, Mwigulu uses the people agenda as his main speech, however he needs to stay consistent and tell us his strategy, so far he has only been telling us ACTION PLANS, well you cant make president if you talk of action plan, that level is not for presidents, that's for DIWANI NA MBUNGE, lets talk US politics, when Obama went out to the mass with his message, it was CHANGE, , he stayed consistent with his message, but it was not built on action plans, rather long term strategies , I will await for others to see , we need to be able to draw a line between.............................1. STRATEGIES 2. INITIATIVES 3. ACTION PLANS
 

Duuh, Nakumbuka alisema pia kuwa alikuwa anamsaidia mke wake kazi ya "mama ntilie", nadhani angeitwa yeye mwenyewe atoe ufafanuzi maana mimi mwenyewe napata mashaka. Nimesoma UDSM pia na nafahamu that system ya "kubakizwa idarani" kwa wanaongoza kimasomo katika idara na ajira kwao huo ni moja kwa moja hapo hapo chuoni (Tutorial Assistant for 1st degree holder). How come waalimu waliokufundisha wakudai cheti wakati wa kukuajiri huku wanakujua nje ndani kitaaluma. Anyway, majibu ya hakika atakuwa nayo Mwigulu tumuite atuptie ufafanuzi wa hoja yake.
 
Mwigulu Nchemba aliyesuka kesi ya Ugaidi dhidi ya Lwakatare wa CHADEMA. Leo hii tumpe uraisi? Kuch nehii!
 
Hii inawezekana tanzania tu,"alisema tena bugeni anao ushahidi wa bomu kwenye mkutano wa chadema Arusha,viwanja vya soweto",mbona mpaka leo ajautoa hadharani?sembuse kuojiwa na polisi?Aiwezekani gaidi kuwa rais wa Tanzania jamani tuache maigizo,Eti kila kona ni gumzo!!kona zipi,huku niliko ata awamjui ila ukiwaambia ni yule jamaa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo arumeru alikuwa kila akipanda jukwaani ni kuporomosha matusi tu,Ahaa ndio wanamkumbuka,sasa wanashangaa eti naye awe rais
 
Watu walimkaataa hata Yesu wakaona bora Baraba achiwe...! Sishangai kuona watu wakishabikia mgawa fedha EL nakuacha watu safi..!
Tuombe MUNGU...!
 
Mbona kwenye hii kona ya huku kwetu watu bado hawana habari naye.
 
Pasco,

Kwa maneno ya Mwingulu Nchemba na ambavyo amekuwa akibehave na ambavyo anaonyesha nia ya kutenda mambo, anajaribu kujionyesha kuwa anafaa kuwa rais wa nchi hii. Ila kwa bahati mbaya sana, nia yake, mawazo na matendo yake yanaonekana ni mtu atakayetaka kufanya kazi na wachapakazi na wanaojielewa. Kwa bahati mbaya mawazo na nia yake vitamfanya asivuke hata ngazi ya kamati kuu.
Hata hivyo huwa simuamini Nchemba maana CCM hakuna hata mmoja anayeaminika. Tumesikia maneno mazuri sana toka CCM kama maisha bora kwa kila mtanzania, rushwa ni adui wa haki nk lakini Mh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…