Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa!

Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa!

Nchemba kagusa sehemu muhimu sana amenishawishi kwa kiasi fulani kuwa CCM wanajembe la kusimamisha urais

tatizo watu kama nchemba hawatapendekezwa na sisiemu, take my word
 
Bila kujali itikadi za kichama, Mwigulu Nchemba ndo mtia nia pekee katika chama cha kijani (CCM) ambae anaongelewa kila kona ya nchi, magazeti na mitandao ya kijamii yameandika juu ya huyu mtia nia kwa kiwango cha juu kuliko mtia nia yoyote ndani ya chama hicho.
Katika jamii forum pekee zaidi ya michango takribani 2000 imelekezwa juu ya Nchemba toka jana siku ambayo mtia nia huyu alikuwa anatangaza nia yake ya kuusaka " unyerere" katika nchi hii. Michango hii inajumuisha michango yote inayomuunga mkono na ile yenye kumkosoa.
Swali: Je, hii ni ishara kuwa Nchemba ndo atapewa kuipeperusha bendera ya CCM kuelekea ikulu?
Mi niko kijijini hakuna mtu anaemfahamu mwigulu.au umemchanganya edo na mwigulu?
 
Huyu hafai hata kidogo, maana yote aliyokuwa akiongea jana yameongelewa sana na wapinzani bungeni na yeye ndiye alikuwa kinara wa kuyapinga.
 
Hana chochote!!Ni walewale,anajisifia ili apate huruma ya wananchi
 
tatizo la mwigulu alijiharibia mwanzo na siasa zake za chuki kwa wapinzani
ila yupo vizuri kwenye kujeeleza
 
Hii hoja ya umri ni nyepesi sana kaka kumbuka Nyerere alikabidhiwa nchi akiwa na umri gani na mambo aliyoyafanya to be honest hakuna Raisi yeyote aliyoyafikia isipokuwa kuyabomoa kaka.swala la umri sio hoja wala hakuna uzoefu unaohitajika kwenye kufanya mambo yaende isipokuwa ni dhamira ya dhati ya mtu huyo ya kuwatumikia watu kwa haki na usawa.

Umri sio dili, hata Makamu wa Rais Bilali ni mzee lakini mambo ni yale yale tu ndani ya serikali. Uawadilifu wa mgombea na timu yake inayomzunguuka na chama anachotoka ni muhimu sana
 
Mimi ni mpinzani hasa,Upinzani upo ndani ya damu yangu. Nilianza kuichukia CCM na serikali yake enzi zile za Lyatonga yupo ktk wizara ya mambo ya ndani,alipomkamata mke wa bosi wake na vipande vya madini ya dhahabu ktk uwanja wa ndege.Lyatonga enzi zake alikuwa kaa la moto kwa wahalifu wa aina zote.Ile kauli mbiu yake ya 'nakupa siku saba muwe mmesalimisha silaha zenu' ilifanya majambazi wengi na wahalifu wengi kukosa raha.
Mimi ni mpinzani tangu nilipokuwa sekondari,no one followed me and convinced me to join politics, just the political environment influenced me to like politics.
Ila linapokuja jambo linalostahili kupewa heshima yake mimi huwa nalipa heshima hiyo.Ktk watu wote walioko CCM ni Mwigulu pamoja na wale makada wengine ambao ama walikuwemo ktk tume ya katiba mpya au waliunga mkono rasimu ya katiba mpya ya Jaji Warioba.So ndani ya CCM pia wapo watu safi.Mwigulu pamoja na dosari zake lkn ni miongoni mwao.
Watu hubadilika.
 
Ccm are the party that says government will make you smarter, taller, richer, and remove the crabgrass on your lawn. Ukawa are the party that says government doesn't work and then they get elected and prove it.
 
Hivi ule ushahidi slio sema atautoa hata mbinguni kuhusu Mh Lwakatare amesha utoa? Ina kuwaje mnamshabikia gaidi? Hii nchi haiwezi kuongozwa na magaidi.
Aliwahi kuhusishwa na mauaji Arusha je mbona hakukanusha? Uzinzi Igunga, leo awe rais? Hivi kweli Watanzania tumelogwa?

We hujawahi kuzini?. Kwanza kumbuka umezaliwa Nje ya ndoa, wadanganye wasiokujua
 
We hujawahi kuzini?. Kwanza kumbuka umezaliwa Nje ya ndoa, wadanganye wasiokujua

Viongozi wetu ndio wanareflect picha ya wananchi na tabia zao ndio hata mtu akiwa mzinzi mbakaji muuaji sisi tunaona ni sawa tu coz hata sisi ni tunafanya hayo lakini kwa binadamu mwenye akili nzuri na kujua thamani yake hawezi tetea mtu mchafu aje aongoze coz anajua nchi itachukua muda sana kusonga mbele maana rais atakuwa anazongwa na mawazo ya kulala na kila mrembo na kusahau kuivusha nchi kwenye umaskini kwenda utajiri. Nikiona comments za kushabikia viongozi wasio na maadili ndio naona bado tuko na safari ndefu sana ya kuwa binadamu kamili
 
Mwigulu amebeba dhamira ya kweli tatizo ni mfumo uliopo ndani ya chama chake ataweza kuufuta.
 
Usiishie kusema tu mkuu, tusaidie tutoke huko kwenye akili za panzi. Vinginevyo utakuja kuongozwa na viongozi hao hao wenye akili za panzi.

Viongozi ni zao la jamii.....kama watanzania ni jamii ya panzi obvious viongozi wetu watakua hivyo hivyo tu
 
Niko sehem moja hapa mjini kati. Wazee flani wako pembeni yangu wanamponda mbaya. Eti hotuba yake ilikua kama kafocus kwa Lowassa m sijui mana sikuisikiliza.
 
Mpakabsasa hakuna kiongozi aliyeni sisismua ngozi yngu na pia naangalia yupi kati ya hawa wataokuja .lakini kidogo mwigulu akitaka kunisisimua japo bado .na mpaka sasa kati ya waliotoa hotuba yeye ataweza
 
ANAFAA KUWA RAIS LAKINI MUDA BADO STILL 2 YOUNG/ asubirie 2025
apate uzoefu ndani ya serekali kwanza!!!

nje ya siasa na itikadi yangu kuwa chadema, bila kujadili kama mwigulu ana uwezo ama hafai.

mimi huwa sikubaliani kabisa na hoja dhaifu ya kutukandamiza vijana kwa sababu ya ujana wetu.

mtu yeyote anaweza kufanya jambo kubwa ama dogo kutokana na uwezo wake na si umri wake wa ujana ama uzee.

hata hivyo mwigulu siyo kijana kwa kuwa ana miaka zaidi ya 35. hivyo hana sifa hata kidogo ya kuwa kijana ama kuitwa kijana.

kwa mujibu wa sera na sheria inayohusu vijana, kijana ni kati ya miaka 18 mpaka 35.

kwa mujibu wa sayansi ya biolojia uzee huanza kumwingia binadamu kuanzia miaka 40.

hivyo kwa vigezo vyote hivyo, mwigulu si kijana. ila ndo kaingia mwanzoni mwa uzee, ujana ashaumaliza. msimwite kijana tena kama kikwete alivyohadaa watanzania kuwa ni kijana wakati alikuwa mzee wa miaka 55.

mwigulu msimjadili kwa hoja ya umri.

na mimi sipaswi kujadili mgombea asiyenihusu. japo najua mwaka huu CCM haina mgombea hata mmoja anaefaa kuwa rais wala atakaeikoa CCM na anguko kuu
 
Back
Top Bottom