Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa!

Asikwambie mtu, hiki anachokifanya Mwigulu kwenye uchumi (kodi na tozo) ndicho walichokifanya wazungu na bado wanakifanya hadi leo. Hata Kasari alikusanya kodi, hata hizi zaka na sadaka kwenye dini zetu ni kodi pia. Maana Bila kodi nchi haikwendi. Kasoro yetu ni kwamba watumishi wanalipwa kidogo sana ukilinganisha na idadi ya kodi wanazotakiwa kulipa, lakini watu wetu wengi (90%) hawana ajiri na wenye ajira wanalipwa ujira kidogo sana, wale wanaolima na kufuga hawana masoko ya uhakika na bei za uhakika kwa mazao yao, hivyo ulipaji kodi ni mdogo pia. Hata hivyo nchi ina madini ya chuma mengi, makaa, madini, gesi, mbao, wanyama pori ambao hatujafanya vya kutosha kuinua vipato vya watanzania kwa kutoa ajira na ujira wa uhakika.
 
Watu wanaujua umuhimu wa kodi na tozo, wanacholalamikia ni kiwango kinachotozwa. Wangepunguza kiwango mlipaji wala asingehisi kuwa anailipa na kuchangia uchumi na uendeshaji wa nchi moja kwa moja.

Wawe wabunifu ili kodi zisiumize walipaji na wakati huo huo ziguse wengi kwa kulipa kiasi kidogo, pato litaongezeka maradufu.
 
Ulipewa bahasha ya khaki sio bure
 
Kodi ni muhimu sana lakini unwaeza kujibu haya?;
1. Kila mwezi tunakusanya tozo kiasi gani
2. Hizo tozo ni mpya je zimepangiwa eneo gani la maendeleo?
3. Miundombinu yetu imeboreshwa kuliko awamu zilizopita?

Hatupingi tozo tunapinga tozo kutotunufaishs
 
Nakubaliana na kodi 100% ila napingana na tozo 100%. Huwezi kufanya double taxation kwa kitu kile kile, mshahara unakatwa paye, then unawekwa bank kwa ajili ya matumizi yangu. Badala ya kutoa na kukatwa service charges za bank, nakatwa kodi nyingine kwa jina la tozo...hii kwangu sio sawa mkuu glenn.
 
Duuh! maswali yako yanaeleweka lakini ni dhaifu sana. Kuna mambo yametokea ambayo hayajatarajiwa kutokea. mfano, bei ya mafuta kupanda juu na serikali kulazimika kutoa ruzuku kupunguza makali kwa wananchi, kupungua kwa misaada na ahadi za nchi wahisani kwenye bajeti yetu kutokana na vita ya Ukraine kumeacha mashimo kwenye matumizi yetu, mabadiliko ya hali ya hewa na kutarajia mvua chache na mavuno kidogo yahataingia kwenye dharura zetu.
 
Acha ujinga ruzuku iliyotolewa ni sawa na kupunguza sh 100/lita.
Bado huko kwenye mafuta kuna tozo ya sh 1,100.
Hivi unajua kwanini Zanzibar mafuta ni bei chee sana chini ya 3k?
 
Sasa nimekuelewa!!
 
Hakuna ubaya wowote kwa mwana CCM yeyote kuwa na ndoto ya urais. Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa!
P
 
Nadhani utakuwa unazifaham siasa za tanzania kwa kiwango kidogo sana hata kama ni kada.

Lah basi una maslahi , ambayo kimsingi huondoa ufaham wa watz wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…