Mwigulu Nchemba anajitahidi sana ila anakabiliana na upinzani mkali mno

Mwigulu Nchemba anajitahidi sana ila anakabiliana na upinzani mkali mno

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Nilianza kumfuatilia sana huyu mwamba nilipoona jina lake limeshika kasi, barabara za mikoani kwenye mawe makubwa na miti mikubwa waliandika jina la mwigulu wakimtaja kama Rais ajaye! binafsi nimewahi kumtembelea ofisini kwake.

Ni msikivu sana na hana kiburi wala dharau. Tuliongea mengi nakumbuka wakati huo alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Kuna shida kubwa nilikuwa nayo kipindi hicho, nakumbuka alimtuma msaidizi wake mpaka ofisini kwangu. Yule jamaa kwa sasa ni mbunge wa jimbo moja huko Tanga. Alifika ila alichopewa aniletee hakuwahi nifikishia mpaka leo!

Bado nampenda sana Mwigulu natamani siku moja nimuone mbali zaidi ya hapo.
 
Yeye anapanga na Allah anapanga samahan ntakupa mfano ukmfwatilia mwigulu utaona ana jitahid saan kutuaminisha kuwa yeye ni mzalendo na agenda ya kuchora mabango nchi nzima kuwa yeye ndo rais ajaye ilionyesha jins gan anatak urais kwa nguv lakin wakongwe wanasema:

A KING DOES NOT SAY I AM THE KING BUT HE LEADS AND U CAN SAY HE IS THE KING THROUGH HIS ACTIONS

Kwa mimi nadhan Mwigulu is too greedy na mtu ambaye kwa kupata madaraka na nakusema kama hutak kutoa tozo hama amia burundi unajiuliza vip kama akiwa rais na kila kit kiko chin yako hamna bunge la kumwajibisha wala mahakam ya kukosoa matendo yake unapata picha maisha yatakuwaje pindi akiwa kiongozi.

Na kwa hao watawala nadhan wakat wa mwenda zake walionja tamu chungu hivyo kuwa na katiba nzur ni ulinzi kwao na sisi pia lakin wakidhan kuwa kila siku wataweka watu wao wajue kuwa watu wanabadilika na mungu hatawapa tena nafas ya kurekebisha makosa yao kwan atakuja kuja mtu wataomba mwisho wa dunia ufike na hakuna ayakae kuja kuwasaidia ila majuto ni mjukuu.
 
Waziri mzee wa cheap tozo and easy tax, zenye kuleta ukakasi mkubwa kiuchumi huyu Waziri ni shida kubwa.
 
Mwigulu baki kua rais wa mawe tu ndugu yangu, Tanzania huipati ng'o
 
Angekuwa hana jeuri, kiburi na ulevi wa madaraka asingewaambia wanaopinga tozo waende Burundi 🇧🇮
Wewe ni chawa tu kama chawa wengine
 
Ila ni muuaji. Alitaka kumuua ndugu yake i.e Lisu. Pia Yuko tayari kuua ili mradi tu apate nafasi. Rejea mpinzani wake wa chadema alivyofanywa. Yule ni zaidi ya jp. Huwa hajali mtu anajali maslahi yake tu. Nina wasiwasi hata mke wake Hana mapenzi naye ispokuwa source of income tu.
 
hayo yote ya tozo nk,sio ya mwigulu ni ya serikali nzima ndio maana yalipitishwa bungeni ,tozo sio wazo la mwigulu ni wazo la serikali nzima
 
Back
Top Bottom