Martin Maranja Masese
Member
- Apr 24, 2011
- 29
- 544
Waziri wa fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba, leo akifanya mazungumzo ya kimkakati na CloudsTV amesema hakuna siku mtanzania yeyote ataombwa mchango kulipa deni la Taifa.
Mwigulu Nchemba, anatajwa kuwa msomi wa uchumi labda haelewi au ana kiburi au dharau au anapotosha umma kwa makusudi kwa sababu watanzania wengi hawapendi maandishi.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inakusanya mapato yake kodi kutoka katika kodi ya mapato, kodi ya ongezeko la thamani, ushuru wa forodha, bidhaa zinazouzwa nje.
Kodi ya Mapato (mishahara, vipato vya watu binafsi, makampuni), VAT (ununuzi wa bidhaa na huduma); Ushuru wa Forodha, bidhaa zinazouzwa nje (uagizaji na usafirishaji wa bidhaa nje).
Kodi ya mapato Tanzania ni tozo kwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotokana na vyanzo vitatu ambavyo ni ajira, biashara pamoja na uwekezaji.
Kodi hii inatozwa kwa Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004, kama ilivyorekebishwa. Usimamizi wa kodi ya mapato hufanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Wanaostahili kulipa kodi ni pamoja na vyombo na watu binafsi. Chombo kinaweza kuwa shirika au mfuko. Shirika ni chombo kilichosajiliwa/kisichosajiliwa na watu au chama.
Watu binafsi ni pamoja na wafanyabiashara, wakulima, wavuvi, wafugaji (ambao wote wanalipa kodi ya ongezeko la thamani), watumishi wa umma (hawa wanalipa pia PAYE).
Mapato yasiyo ya kodi yajumuisha; faini, ada, uuzaji wa nyaraka za zabuni na mapato ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa. Mfano ni zile faini za trafiki wanazokusanya barabarani.
Misaada na Mikopo Nafuu inajumuisha Misaada ya Kibajeti, Misaada na Mikopo Nafuu ya Miradi na ya Kisekta. Hii ndiyo ile mikopo ambayo Mwigulu anakopa kila Jua likiwaka.
Mikopo ya ndani na nje ikijumuisha; mikopo ya masharti ya kibiashara ya ndani na nje ya nchi ambayo ni asilimia moja (1) ya Pato la Taifa. Huu pia ni mzigo wa walipa kodi Tanzania.
Bajeti kuu ya serikali ya CCM kwa mwaka wa fedha 2022/23 ni Sh41.48 trilioni. Mwaka huu wa fedha serikali ya CCM itatumia Sh9.09 trilioni kulipia deni pekee. Deni la taifa na mengine.
Hiyo ni asilimia 21.9 ya bajeti ya mwaka huu wa fedha (2022/2023) ambayo ni Sh41.48 Trilioni. Hii ni asilimia 50 ya mapato ya ndani ambayo ni Sh18 Trilioni (hizi ni takwimu za TRA)
Sh26.48 trilioni zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ikiwa ni 63.8% ya bajeti yote, ikijumuisha Sh11.31 trilioni kwa ajili ya ulipaji wa deni la Serikali na gharama za Mfuko Mkuu
Sh9.83 trilioni ni kwa ajili ya mishahara ikiwemo nyongeza ya mshahara, upandishaji wa madaraja kwa watumishi na ajira mpya. Serikali ya CCM hawajafanya hivyo. UTAPELI.
Sh5.34 trilioni ni kwa ajili ya matumizi mengineyo (OC) ikijumuisha Sh200.0 bilioni kwa ajili ya kulipa madeni yaliyohakikiwa ya watumishi na wazabuni. Hawajafanya. ULAGHAI
Matumizi ya Kawaida ni kulipa mishahara na marupurupu kwa watumishi wa umma, mahitaji ya ofisi na huduma, riba kwenye deni la taifa, matengenezo na ukarabati wa nyenzo na vifaa
Sh15.0 trilioni, sawa na 36.2% ya bajeti yote, matumizi ya maendeleo. Sh12.31 trilioni ni fedha za ndani, sawa na 82.0% ya bajeti ya maendeleo na Sh2.70 trilioni ni fedha za nje.
Matumizi ya Maendeleo ni pamoja na kugharamia miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa barabara, shule, hospitali, miundombinu ya maji, umeme na ununuzi wa rasilimali mpya.
Kati ya mapato hayo yanayotajwa, kiasi kitakachokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yanakadiriwa ni Sh23.65 trilioni. Maana yake watanzania watalipa kupitia kodi na tozo.
Sh28.02 trilioni ni vyanzo vya ndani. Misaada na mikopo nafuu kutoka kwa Washirika wa Maendeleo ni Sh4.65 trilioni. Vyanzo vya ndani ni pamoja na makusanyo ya kodi za raia.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanakusanya hadi fedha za watanzania kupitia kodi ya Majengo. Kila unapolipa umeme kupitia LUKU TRA wanachukua shilingi ELFU MOJA. KODI.
Mwaka wa fedha 2016/2017 TRA ilipewa jukumu la kukusanya Sh15.079 trilioni lakini ikaweza kukusanya Sh14.055 trilioni, kwa mujibu wa taarifa ya BoT kwa mwaka ulioishia Juni 2017
Waziri wa fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba unasemaje watanzania hawataombwa mchango wa deni la Taifa? Hivyo TRA haikusanyi kodi? Waziri haipendezi kuwa MUONGO!
Kutokana na kwamba Tanzania kuna walipakodi wachache (tax base) ndogo. Serikali ilipaswa ihakikishe inaongeza uzalishaji viwandani ili kukuza sekta nyingine. Serikali DHAIFU.
Badala yake waziri wa fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba anawaongezea walipa kodi wachache tozo na kodi badala ya kupanua/kuongeza wigo wa uzalishaji mali, kodi ipatikane
Ubadhirifu wa fedha za umma, Rushwa, serikali ya CCM kushindwa kubana matumizi pia ni sababu nyingine ya kuongeza tozo na kodi ili kuweza kuhudumia mabwanyenye. ACHENI!
Serikali ya CCM inatumia Sh556 bilioni kwa mwaka kununua magari kwa ajili ya mabwanyenye. Magari yanahudumiwa na kodi za mapato yatokanayo na kodi za watanzania. .
#MMM, Martin Maranja Masese